Mama wa Askari polisi aliyeshushwa cheo amlilia Rais Samia

Ila huu upuuzi wa kupeana TU vyeo kwa aiili ya jambo fulan ndyo imeathir had elimu yetu

Vyeo vya jeshi vpo katika mtiririko maalumu lazma uhenye na kusomea hicho cheo

Huu mtindo alileta bwana Magufuli ukifanya Jambo likimpendeza bas kupewa nyota n suala la kawaida

Kumbuka mkuu wa jkt aliyepita nadhan hata cdf hakupendezewa na aliyofanya bwana Magufuli
Acha kuwa kama mchawi wewe... vyeo vya heshima hutolewa na ni jambo la kawaida duniani kote. Mm sijui wewe ni mtu wa wapi na hata smart phone cjui umepata wap wakat hamna kitu. Kila siku mnalia kupingapinga tu bila hata kufanya reasoning kdg... kila jambo Magufuli,,,, una mimba yake uzae yaishe... mwache shujaa wetu apumzike kwa amani...
 
Kwakweli tunahitaji polisi waadilifu, bora wapewe vyeo waadilifu kuliko hao waliosomea wakati uadilifu zero, hakuna haja ya kumshusha cheo! Mlipomtunuku mlimwambia lazima akasomee, angejuwa singekubali hiyo tunuku ya masharti!
Mkuu huo ndio utaratibu wa majeshi yetu yote, wa miaka yote, kuwa unapopewa cheo kwa njia hiyo lazima ukakisomee chuoni, pindi nafasi inapopatikana, nashangaa sana kwa huyo askari kwa nyie wengine na huyo mama yake, mnaweza kuona ni jambo geni lakini kwake na kila askari analifahamu.
Hizo ni taratibu za kazi , sasa nyie mnaanza kuingiza siasa kutokana na kutojua taratibu!!!inatakiwa wamhoji sana kwanini hataki kwenda kozi, wakati kozi zenyewe ni za kawaida tu, labda angetolewa kwenye u sajenti na kwenda kozi za urakibu msaidizi, hapo shughuri ingekuwepo!!lakini huwa haziwezi kuvukishwa hivyo, ametoka usajenti anaenda kozi ya u staff sajenti!!au kitengo alichopo ndio kizuri ana hofia akienda kusoma akirudi anaweza asiwe hapo tena!!kwani ni sawa na kumwambia trafiki akasomee V, akirudi awe Ffu, au abakie bila cheo hapo hapo trafic, lazima aseme bnana niache hapa hapa.
 
Huyu watakuwa wamemuonea imagine certificate zote za utendaji kazi, Kuna mtu anachukizwa na utendaji wake.
C.c Simbachawene
C.c Rais Samia
C.c Mchengerwa
 
Siku Moja Mara Baada ya jeshi la polisi nchini kutoa karipio Kali Kwa askari wake, Meshack Laizer baada ya kukiuka maadili ya jeshi hilo ,mama mzazi wa askari huyo,Rebecca Laizer ameibuka na kuiomba Serikali iingilie katika suala hilo ili haki ya mwanaye iweze kutendeka.

Akiongea nyumbani kwake katika kijiji Cha Nambare,wilaya ya Arumeru,mama huyo ambaye ni kikongwe mwenye umri wa miaka 85 ,amedai kusikitishwa na taarifa hiyo akidai inalenga kumkosesha haki ya utumishi uliotukuka askari huyo.

Akiongea huku akionyesha barua kadhaa za pongezi ambazo Meshack aliwahi kutunukiwa na jeshi Hilo baada ya kukataa Rushwa ikiwemo ya sh,milioni 10 ,alisema suala hilo linapaswa kutazamwa Kwa mapana yake Kwa kuwa anaamini linatokana na chuki na wivu dhidi ya mwanaye kipenzi

Mama huyo amemlilia Rais Samia Suluhu akimwomba aingilie Kati ili mwanaye huyo wa pekee ambaye ndio tegemeo lake la maisha aweze kurudishiwa cheo alichopokonywa na asipewe adhabu nyingine ikiwemo kufukuzwa kazi.

"Nimesikia wanataka kufukuzwa kazi wasifanye hivyo hizo ni chuki tu za askari wenzake hawampendi Kwa sababu anatenda haki"alisemaView attachment 2055925View attachment 2055927View attachment 2055928View attachment 2055929
@tanpol watajuana huko wao wenyewe
 
Acha mihemuko wewe, yule askari aliyepambana kwenye tukio la majambazi waliopora pesa za Benki pale Ubungo hakupandishwa cheo?

Rais aliyekuwa madarakani naye ni Hayati Magufuli?

Wakati mwingine muwe mnapunguza chuki ili mruhusu bongo kuzichakata akili zenu kiufasaha zaidi.
Iwe Mara moja na sio kama sadaka
 
Jamaa ni kiazi kwani kozi shi ngapi!?

Si anasomeshwa na jeshi !?

Sidhani hio kozi inaenda zaidi ya mwaka mmoja

Au anahofia atafeli!?

Polisi kumejaa vilaza and maser
 
Huyu watakuwa wamemuonea imagine certificate zote za utendaji kazi, Kuna mtu anachukizwa na utendaji wake.
C.c Simbachawene
C.c Rais Samia
C.c Mchengerwa
Kupewa nafasi ya kusomtea cheo ni kuonewa wivu?

Hizo certificate ni tuzo TU za utendaji wa cheo alichonacho wakati huo

Cheo kipya hajui hata majukumu ya hicho cheo sababu hajasomea ataishia TU kufanya kazi kiubabaishaji TU sababu hajui kitu kuhusiana na hicho cheo kipya
Kukataa kusomtea hicho cheo kunashangaza Kwa Nini akatae?
 
Siku Moja Mara Baada ya jeshi la polisi nchini kutoa karipio Kali Kwa askari wake, Meshack Laizer baada ya kukiuka maadili ya jeshi hilo ,mama mzazi wa askari huyo,Rebecca Laizer ameibuka na kuiomba Serikali iingilie katika suala hilo ili haki ya mwanaye iweze kutendeka.

Akiongea nyumbani kwake katika kijiji Cha Nambare,wilaya ya Arumeru,mama huyo ambaye ni kikongwe mwenye umri wa miaka 85 ,amedai kusikitishwa na taarifa hiyo akidai inalenga kumkosesha haki ya utumishi uliotukuka askari huyo.

Akiongea huku akionyesha barua kadhaa za pongezi ambazo Meshack aliwahi kutunukiwa na jeshi Hilo baada ya kukataa Rushwa ikiwemo ya sh,milioni 10 ,alisema suala hilo linapaswa kutazamwa Kwa mapana yake Kwa kuwa anaamini linatokana na chuki na wivu dhidi ya mwanaye kipenzi

Mama huyo amemlilia Rais Samia Suluhu akimwomba aingilie Kati ili mwanaye huyo wa pekee ambaye ndio tegemeo lake la maisha aweze kurudishiwa cheo alichopokonywa na asipewe adhabu nyingine ikiwemo kufukuzwa kazi.

"Nimesikia wanataka kufukuzwa kazi wasifanye hivyo hizo ni chuki tu za askari wenzake hawampendi Kwa sababu anatenda haki"alisemaView attachment 2055925View attachment 2055927View attachment 2055928View attachment 2055929
Wamama wa Kitanzania ( baadhi yenu ) muwe mnatumia Akili tusianze Kuwadharau na kuhisi kuwa huenda matatizo ya Watoto zenu wameyarithi Kwenu.

Jana kupitia Morning Magic ya Magic FM nilimsikiliza vyema kabisa Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime ambapo alisema wazi kabisa kuwa Askari huyu alitakiwa kwenda Mafunzo ya hicho Cheo kama inavyotakiwa Kijeshi ila Yeye kila mara alikuwa akizembea tu.

Tena nadhani huyu Mama alipaswa awashukuru Jeshi la Polisi nchini kwani kwa Utovu wa Nidhamu na Kukiuka Maadili ya Kijeshi alitakiwa ashushwe Vyeo vingi tu ila Jeshi la Polisi Kiungwana limemshusha Cheo Kimoja hicho.

Halafu huyu Mama atambue kuwa huyo Mwanae ( Askari Polisi ) hicho Cheo hajapewa na IGP Sirro ila amepewa na Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan isipokuwa 'Kiitifaki' anayempa kwa Niaba ni IGP.

Kinachonishangaza na sasa kuamini kuwa Watanzania tuna Ubarikio wa Kutosha wa tabia ya Unafiki leo hii huyu Mama Mwanae huyu Kashushwa Cheo anataka Rais Samia amsaidie Mwanae mbona wakati Mwanae anapandishwa Cheo hakujitokeza Kumshukuru Rais Samia au hata tu kutaka Kuonana nae?

Yaani Rais Samia Suluhu Hassan aache kufanya Kazi za maana za Watanzania za kuwaletea Maendeleo yao na ahangaike Kupigania Haki ya Askari Polisi Mpuuzi ambaye amekiuka Mwenyewe Sheria na Kanuni za Jeshi la Polisi?

Na ni nani aliyemdanganya huyu Mama kuwa Tanzania nzima Mzazi mwenye Changamoto au Tegemeo kwa Mtoto ni Yeye peke yake tu?

Kuna Vitu vinakera na havivumiliki pia!!!
 
Back
Top Bottom