Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,185
- 18,513
Watu wengi wameshangazwa na kauli za mabishano kati ya yule afisa wa airport na magufuli na Magufuli kudai amedanganywa.
Lakini tujiulize kudanganya kulianzia wapi?Kwanini watanzania ni waongo sana hadi kumdanganya Rais wakati ukweli unajulikana?
Kama baba unamtuma mtoto amwambie mtu umesafiri wakati anajua upo ndani, unadhani ni kosa kwa huyo mtoto siku moja kukudanganya mchana kweupe?
Swali la kujiuliza ni mara ngapi Magufuli akiwa waziri amedanganya juu ya matumizi ya fedha za barabara hali akijua kabisa kuwa hiyo ilikua ni miradi ya wakubwa ikulu.
Kudanganya kumeanzia ikulu na serikali yenyewe kwa ujumla ndio maana kila mwananchi anajiona anahaki ya kudanganya bila kujali nanai anadanganywa.
Kuna uwongo mwingi sana ambao serikali ya Magufuli inaufanya kwa wananchi, kwa nini yeye hataki kudanganywa?
Kama kweli anadhamira ya kweli na hataki uwongo basi ikulu iwe ya kwanza na watubu uongo wote walio ufanya kama serikali na chama chake cha mapinduzi na wasiwe waongo tena.
Nchi nyingine duniani huko waziri akiambiwa na wabunge amedanganya hapo hapo anajiuzuru kwa sababu ni aibu na fedheha katika jamii. Lakini huku kwetu mawaziri wanadanganya na bado wapo na vyeo vyao hata kama imejulikana kweli kadanganya
Kwa hiyo Magufuli alikua na haki ya kudanganywa kwa sababu Tanzania kudanganya sio kosa, na kama ni kosa basi ikulu na serikali yote itaenda jela.
Ondoa boriti yako kwanza..
Kutoka bungeni by Zitto .K Kabwe
''Mwaka 2011 tulipohoji kifungu chenye Fedha tshs 252bn kwenye Wizara ya Ujenzi, Naibu Waziri Harrison Mwakyembe alijibu "Hizi Ni Fedha za miradi maalumu ya barabara ambapo tukipata misaada ya wafadhili hizi ndio michango yetu Kwa miradi". Bunge likapitisha. Hazina ikatoa pesa zote kwenda Wizara ya Ujenzi. Mwaka huu tumehoji, hizi Fedha zilitumika namna gani? Waziri John Magufuli akasema "tulilipa Madeni".
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema kwenye taarifa yake "Ilitengenezwa miradi hewa ya barabara yenye namba ya mradi hewa. Pia hakuna uthibitisho kuwa Madeni yalilipwa kwani hakuna nyaraka za kuonyesha malipo". Tumehoji kutaka majibu, tumepigwa chenga. Kweli? Tshs 252 bilioni hazina maelezo? Tutahakikisha Uwajibikaji katika hili.