Mkuu, Inawezekana Shelukindo anauhakika hao aliowataja hawa-qualify kwenye hizo nafasi na hivyo kumweka mahali pagumu Luhanjo. Naamini pia nimuhimu kuweka maneno/sentensi zetu vizuri ili isieleweke tuna-sound too general e.g. Kabila fulani hawana uwezo. Personally naona kama mtu ana-qualify kwenye position huwezi kumnyima nafasi eti kwavile kuna Wa-Iringa, Chagga, Haya etc wengi kwenye hiyo ofisi. Lakini pia utakapompa hiyo nafasi hakikisha ana something extra compared to other candidates or else, itakuwa ngumu ku-prove why you chose Mr/Miss "A' and not "B".
On a different note; Nataka nikukumbushe kilichomtokea Anna Tibaijuka alipokuwa UN, na Getrude Mongela alipopata ile position as " President of Pan Africa Parliament ". Pamoja na mambo/matatizo mengine, ukabila ni moja ya sababu iliyowafanya wapoteze nafasi zao i.e. kupendelea/recommend watu wa kabila lao wachukue open position hata pale ambapo hawa-qualify.
Tukumbuke Tibaijuka alihamishiwa "Habitat of Humanity" baada ya hapo and it was a demotion of some sort. Getrude Mongela alishinikizwa kujiuzulu na ilikuwa vuta nikuvute maana alikuwa hayuko tayari kuachia post however, there were some serious ethical issues raised about her including financial mismanagement. Ilikuwa ni either aondoke na dignity or else angeondolewa kwa mpango maalumu na wajumbe wa PAP maana walishakosa imani naye). Ingawa matukio yao yalikuwa vipindi tofauti; lakini ukabila ulikuwa one of the problem waliyokuwa nayo. Ilifika wakati co-bosses/workers wa Tibaijuka walikuwa wanajiuliza: kwanini hata wafanyakazi wa chini e.g. wafagizi lazima atoke Bukoba and not locally "kwenye ofisi zao huko huko?" I have no doubt hawa wawili ni smart lakini pia ukabila ulitia doa kwenye kazi zao.
Mashirika mengi ya kimataifa yana-prefer diversity kwenye kazi i.e. kuajiri watu wa sehemu tofauti tofauti(different cultures) ilikuleta mtizamo tofauti tofauti as well as different strategies for the strength of the organization.
Kumbukumbu zako kuhusu Tibaijuka kwenye utumishi wake UN haujakaa sawa. Mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa "United Nations Centre for Human Settlements" Miaka miwili baadaye kituo hiki kilipandishwa hadhi na kuwa mpanga wa makazi wa umoja wa mataifa (UN-HABITAT, "United Nations Human Settlements Programme) na yeye kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mtendaji. Kofi Anan alimteua kuwa UN-Under-Secretary General wa ofisi ya UN Nairobi na wakati huohuo akiendelea kuwa Mkurugenzi mtendaji wa UN-HABITAT.
Banki-Moon alimbadilisha kwa nafasi ya under-secretary general mwaka 2010, lakini pia ukumbuke muda wake wa kutumikia UN-HABITAT ulikuwa umekwisha, japo alikuwa na nafasi ya kugombe tena nafasi hiyo.