Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema kukithiri kwa rushwa nchini kumewafanya wananchi kuichukia Serikali.
Akizungumza leo (Alhamisi) katika mkutano wa kimataifa unaohusu mapambano dhidi ya rushwa jijini Dar es Salaam, Suluhu amesema Serikali imejidhatiti vilivyo na kwamba itaendelea kupambana na rushwa kwa nguvu zake zote.
Amesema kwa kuwa rushwa hufanyika kwa siri, mapambano dhidi yake yanahitaji ushirikiano mkubwa baina ya Serikali, wadau wengine na wananchi katika kuitokomeza.
"Serikali yetu chini ya Rais John Magufuli imepania kupambana na rushwa kwa namna yoyote ile na tayari ipo mikakati tuliyoiweka kwa ajili ya suala hili, " amesema.