Mama Samia Suluhu: Niwaombe sana jikingeni, wakingeni wanaowategemea kwasababu kila tukiamka huyu kalala, huyu kalala inatusikitisha

Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
7,301
5,529
Hii ni kudhihirisha ukubwa wa tatizo lililopo.
95488908_225363645414476_878234559330467727_n.jpeg
 
MACC,M YANASHANGAA KUONA MAMA NA KASIMU MAJALIWA WANAFUNGUKUA UKWELI JUU YA CORONA WALKATI BWANA WALE WENGINE HAWATAKI
 
Mama samia,

Raia tunakuelewa sana, tatizo mfalme wenu ndio anawaangusha. Mungu akuongoze ukatae "UMAKAMO WA RAIS" kwenye uchaguzi ujao. Linda heshima na utu wako. Waachie watapia "TUMBO" wagombanie vyeo serikalini.

Nchi ina "MAABARA" moja tu ya COVID-19, ni aibu kubwa sana. Watawala wanatumia mabavu kupeleka hela nyingi kwenye kujenga SGR, ila sio kupambana na kuokoa maisha ya raia.

Tumesikia kule "CHATTLE" imepigwa "LOCKDOWN" ya maana, hakuna hata baiskeli kuingia wala kutoka, achilia mbali magari na pikipiki. Ila nchi inaangamia kweli kweli, raia wanakufa bila kuchagua watoto wala wajawazito, Mfalme anatuambia sisi raia na mawaziri tuendelee na wala tusiogope "COVID-19" haina madhara (Cha ajabu yeye kakimbia ofisi zake kule Magogoni & Chamwino, licha ya kumlipa mshahara kutoka kwenye "KODI" zetu walala hoi).

Tunaambiwa tusiogope COVID-19 na tusiache kufanya kazi sawa sawa, eti kisa tutashindwa kujenga SGR. Au labda sisi ni "WANYAMA" haiwezi kutudhuru, ila yeye pekee ni "BINAADAMU" ndio maana amekimbia. Katika nchi yetu utawala huu tumegeuka kuwa "WATUMWA", pesa inathaminiwa kuliko "UHAI".

Je, COVID-19 ikiendelea mpaka mwakani, ina maana ofisi itahamia Chatto mpaka mwakani?

Mungu ibariki tanzania, waadhibu madhalimu.
 
hao kila siku wanaoanguka wapo katika wale 17 au sasa hivi officially kwa data alizonazo yeye ni wangapi, na kama ni yeye kweli katoa huu ushauri angeanza kwanza kuwashauri jamaa zake kule bungeni na kuwauliza wanafanya nini huko ?
 
Busara angeionyesha kwa kuwataka wabunge wa ccm waji carantini ili kuepuka kuwaambukiza wananchi kwa kuwa tayari kwenye group lao wenzao wamelazwa na covid-19
 
Hii ni kudhihirisha ukubwa wa tatizo lililopo.View attachment 1437816

Hizi kauli za hawa wamama ni fikirishi. Mwingine alisema, "sasa tumeamua kusema ukweli". Mwisho wa kumnukuu.

Makonda naye kiasi alijitahidi, "Dar es Salaam watu wana pukutika ...." Mwisho wa kumnukuu.

Ingependeza kama sote tungekuwa wawazi hivi kwenye changamoto moto zote tunazopitia zikiwamo za haka ka upepo.
 
Mama samia,

Raia tunakuelewa sana, tatizo mfalme wenu ndio anawaangusha. Mungu akuongoze ukatae "UMAKAMO WA RAIS" kwenye uchaguzi ujao. Linda heshima na utu wako. Waachie watapia "TUMBO" wagombanie vyeo serikalini.

Nchi ina "MAABARA" moja tu ya COVID-19, ni aibu kubwa sana. Watawala wanatumia mabavu kupeleka hela nyingi kwenye kujenga SGR, ila sio kupambana na kuokoa maisha ya raia.

Tumesikia kule "CHATTLE" imepigwa "LOCKDOWN" ya maana, hakuna hata baiskeli kuingia wala kutoka, achilia mbali magari na pikipiki. Ila nchi inaangamia kweli kweli, raia wanakufa bila kuchagua watoto wala wajawazito, Mfalme anatuambia sisi raia na mawaziri tuendelee na wala tusiogope "COVID-19" haina madhara (Cha ajabu yeye kakimbia ofisi yake, licha ya kumlipa mshahara kutoka kwenye "KODI" zetu walala hoi).

Tunaambiwa tusiogope kufanya kazi, eti kisa tutashindwa kujenga SGR. Katika nchi yetu utawala huu tumegeuka kuwa "WATUMWA", pesa inathaminiwa kuliko "UHAI".

Mungu ibariki tanzania, waadhibu madhalimu.

"CHATTLE kuna LOCKDOWN" ?!!!

Hapana! Huo ni uwongo na uzushi.

Hakuna Lockdown yoyote CHATTLE.

Nasema hili kwa uhakika asilimia mia, hakuna Lockdown yoyote CHATTLE.

Don't believe everything you read on internet.

'Hearsay' is always inadmissible!!

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom