Mama Samia Suluhu: Kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
wavivu.jpg

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka serikalini.

Samia ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa maafa mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa serikalini.

Amewahimiza wananchi kote nchini kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na pindi wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza mazao yote wanayovuna ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia zao.

Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.

Chanzo: Mwananchi
 
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka Serikalini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa maafa mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa Serikali.

Amewahimiza wananchi kote nchini kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na pindi wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza mazao yote wanayovuka ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia zao.

Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wa mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kufanya misako ya hali na mali katika kupambana na tatizo hilo ambalo limechangia kupunguza samaki katika maeneo mbalimbali nchini.

Ametoa mfano kwa mkoa wa Mara kuwa ulikuwa na viwanda Vinne vya kuchakata samaki lakini kutokana na shughuli za uvuvi haramu na wa kutumia sumu umepelekea viwanda Vitatu kukosa malighafi hiyo na kusitisha uzalishaji.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema jambo hilo ni baya kwa sababu limeikosesha Serikali mapato na kusababisha wananchi wakose ajira kutoka kwenye viwanda hivyo jitihada za makusudi lazima zifanyike katika kukomesha uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika Ziwa Victoria.

Aidha, Makamu wa Rais ameeleza kufurahishwa na kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Musoma ambao umetekelezwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa na kusema kuwa mradi huo utaondoa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya ya Musoma.

Amewataka wananchi wa Manispaa ya Musoma kuulinda na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa miaka mingi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Manispaa hiyo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mara Dakta Charles Mlingwa amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mara kuweka itikadi zao kando na washirikiane katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom