beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya kutuma na kutoa Fedha na kupunguza viwango vya tozo kwa 30%

Pia Serikali imejadiliana na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%

Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi Septemba 01, 2021

Taarifa Kamili:

1BB2B4FA-BB0A-4F2F-9374-4A93FB979630.jpeg
 
Kwahio Punguzo hilo, litakuwa ni Ongezeko la Asilimia ngapi kutoka tulipokuwepo Awali....

Hii inanikumbusha story ya ukitaka kumchemsha chura ongeza moto kidogo kidogo..., ila huenda hapa ni kuweka moto mkali kuliko ili ukipunguza kidogo mtu aone ahueni ila kumbe bado ni moto mkali
 
30% bado ndogo sana.. punguzo lilipaswa kuwa chini ya 50%.. kinachoendelea ni ujambazi wa mchana kweupe.
 
kumbe walikuwa wanafanya makusudi.

2025 kura yangu bora nimpe mwanangu chadema
 
Naona kama kigongo cha wimbo wa Nay Wamitego al-maaruf Rais Wa kitaa! Kimesaidia kushusha presha.
 
Back
Top Bottom