Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,586
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu ameanza rasmi ziara ya siku 6 mkoani Tanga akianzia wilaya ya Handeni ambako anapewa taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri za wilaya ya Handeni.

Tuko mubashara TBC.

Updates:

Madhumuni ya ziara yangu ni kuangalia miradi ya maendeleo, miradi yote ambayo tumeiahidi kwenye ilani ya uchaguzi, jinsi inavyotekelezwa, fedha zinavyotumika, nani anasimamia nini na ndio maana tupo na waheshimiwa mawaziri hapa, naibu mawaziri lakini pia wenyeji wetu wa huku pamoja na uongozi wetu wa chama kwasababu chama ndio kimetutuma muende mkafanye hili na hili na lile.

Niwashukuru kwamba nimeweza kusimama tumesalimiana, ninalotaka kuwahakikishia ndugu zangu, Tanzania tuko salama, Tanzania tuko salama. Ni kawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa, mara mafua, mara homa mara chochote kile.

Lakini nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja, ni wakati huu. Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa.

Nawaomba wote tushikane kwa umoja kwa mshikamano wetu kama watanzania, tuendelee kuchapa kazi kama sisi tulivyokuja tunachapa kazi, tunaangalia miradi, watu wote shughulikeni na mambo yenu, jengeni Taifa lenu tujenge umoja na mshikamano wetu ili Tanzania yetu iwe Taifa Imara.

Na hichi ndicho kinachotuchongea, uimara wa Taifa letu unaleta maneno mengi.

 
Lakini nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja, ni wakati huu. Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa.
Sawa kabisa. Tunakuelewa Mh Makamu wa Rais.
 
Back
Top Bottom