Mama Samia anza kwa kuboresha Baraza la Mawaziri

Hapo mwisho penye kumalizia hiyo miradi mikubwa(white elephant projects),umenikumbusha hali ya mwananchi wa chini alivovamiwa na UMASIKINI wa kutisha kisa hiyo MIRADI!!!

Naamini JK karudi madarakani,huu upuuzi hautojirudia!!!
 
Mama usiingie kichwa kichwa ktk kuongoza nchi yetu kuna mabadiliko makubwa ya kufanya katika baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya. La sivyo utateseka sana kufanya maamuzi peke yako na itakuwa one man show leadership kama iliyopita. Katika teuzi zako uwe sana makini na haya makundi 3 ya mawaziri walioko madarakani maana wengi walikuwa remote tu na hawakumsaidia rais aliyepita kwa kuogopa kufukuzwa kazi:

KUNDI LA KWANZA: MAWAZIRI BENDERA FUATA UPEPO NA KUJIPENDEKEZA A.K.A WALAMBA VIATU

Kwenye kundi hili wapo wafuatao ambao sifa yao kubwa ni tabia ya UOGA na kumsifia rais tu na hawana jipya wala ubunifu wowote
  • Palamagamba Kabudi( ameidhalilisha UDSM inaitwa JALALANI, mganga njaa)
  • Jumaa Aweso : waziri wa Maji(huyu ana mihemko mingi kama mpiga gitaa za reggae, pia anakurupuka)
  • Joyce Ndalichako( anakurupuka kufanya maamuzi bila utafiti
  • Jenister mhagama (hajiamini hata kufanya maamuzi ambayo ni obvious)
  • Ummy Mwalimu(ana nidhamu ya uoga na kutojiamini)
  • Innocent Bashungwa(hafai hata kuwa hata mwalimu mkuu wa Primary school)
  • Damas Ndumbaro(mnafiki na mjuaji)
  • Geofrey Mwambe ( hana jipya , siyo mbunifu)
  • Dkt Leonard Chamuliho( ana nidhamu ya uoga na kutokujiamini sio mtu wa vitendo
  • Dkt Philip Mpango( ana tabia yaku -cook data za uchumi kumfurahisha rais)
  • Dr. Godwin Mollel ( Huyu ana skendo nyingi, nendeni Mirerani mtajua, pia ameharibu gari la mtu hataki kulipa mil 20, pia ni mwongo mkubwa na mpenda sifa za kijinga; hana weledi hata kidogo)
  • George Mkuchika ( mzee huyu akapumzike huyu tafuteni damu mpya hana jipya ni walewale wa kulamba viatu)
  • Mwigulu Nchemba( arrogant, jeuri anapenda kutisha watu , huyu ana spirit ya udikteta na tabia za uongo hafai kwenye nchi ya demokrasia, busara ni zero)
  • Dotto Biteko (ameumiza sana sekta ya madini halafu sio mwaminifu, ni mtu wa deal

KUNDI LA PILI: MAWAZIRI MAJASIRI NA WANAOJIAMINI
  • Prof .Adolph Mkenda( Strong , decisive, technical, objective and problem solver
  • Husein Bashe( quick to act, bold, intelligent, technical, objective and problem solver
  • Simbachawene ( anafanya mambo objectively bila papara)
  • Medadi Kalemani(Pamoja na kubebwa na homeboy lakini amejiongeza sana)
  • Dorothy Gwajima( Ni mbunifu na jasiri ila mwoga kuchukua hatua kali)
  • Wiliam Lukuvi ( Hapendi uonevu, anajiamini, hana longolongo ana address tatizo na kutoa ufumbuzi, tunahitaji akina Lukuvi wengi)
  • Sulemani Jaffo( Huyu anafaa ni mjasiri na decision maker mzuri)
NB: NASHAURI HUSEIN BASHE APEWE WIZARA BADALA YA KUWA NAIBU WAZIRI

KUNDI LA TATU: MAWAZIRI WA KUJENGEWA UWEZO

  • Kitila Mkumbo
  • Mashimba Ndaki
  • John Kwandikwa
  • Faustine Ndungulile
MANAIBU MAWAZIRI

Naibu Waziri anayekubalika na anayejua anachokifanya ni Huseini Bashe na kufuatiwa kwa mbaaali na Angelina Mabula wengine wote waliobaki ni kama wacheza ngoma tu maana hata JD zao hawazielewi

MAKATIBU WAKUU WA KUFYEKWA MAPEMA:


  • Doto James: Mama Samia anza na huyu bila huruma mapeema nafikiri unaelewa kwa nini nasema hivi
  • Katibu Mkuu wizara ya afya: huyu aondoke maana ni mwongo mkubwa hana weledi wa kukaa ktk hiyo Wizara
Kwa hiyo mama na dada yetu tunakusihi usiingie kuongoza serikali na watu mizigo tunahitaji mabadiliko makubwa na speed ya utendaji, zaidi sana kkundeleza na kumalizia ile miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ule wa bwawa la Nyerere, bomba la mafuta na STD gauge railways.

Makada wa chama wabakie kutekeleza majukumu ya chama na watu wenye uwezo wao(professionals) wa kiutendaji wapewe nafasi za kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi mbele. Kimsingi ndio wengi wameachwa benchi kwa sababu walikataa tabia ya NDIYO MZEE
Umetisha mkuu, Mama ashindwe mwenyewe tu sasa
 
Back
Top Bottom