Mama Salma Kikwete, Wewe Ni Mtumishi wa Serikali?


BelindaJacob

BelindaJacob

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2008
Messages
6,111
Points
2,000
BelindaJacob

BelindaJacob

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2008
6,111 2,000
Nyinyi watu mnapiga sana kelele, lakini watanzania ni viumbe wa ajabu sana!!! Hata wakisikia na kushuhudia wanavyoibiwa, ni waoga tu. WEZI WETU hawana wasiwasi katu!! Mama endelea kutafuna vya mabwege.., usitie shaka. Nenepa mama!!! Hahahahaaaaa!:confused2:
Watu wangapi?wewe ni mkongo? Akili za ovyoo kwenye jambo muhimu!
 
MAMA POROJO

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
4,979
Points
1,225
MAMA POROJO

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
4,979 1,225
Msemaji wa Ikulu Salva naye yuko kwenye kampeni?
 
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,207
Points
1,500
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
Joined May 19, 2009
13,207 1,500
Mwaka huu mpaka kieleweke!
 
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
8,618
Points
2,000
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
8,618 2,000


Ni kutokana na kutumia raslimali za Serikali wakati wa kumnadi mumewe kuingia Ikulu wakati yeye si mtumishi wa serikali!

KAMPENI za uchaguzi mkuu zimezidi kunoga baada ya mgombea urais wa Chadema, Dk Slaa kumgeukia mke wa Rais Jakaya Kikwete akieleza kuwa anatumia vibaya rasilimali za nchi kumpigia kampeni mumewe huku akimtaka katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba aeleze kisa cha kufukuzwa ualimu mkuu wa shule ya msingi.

Kwa muda mrefu Salma Kikwete, mke wa Rais Kikwete na ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), amekuwa katika ziara kwenye mikoa mbalimbali, jambo ambalo limekuwa likitafsiriwa kuwa anafanya ziara za kampeni kwa ajili ya mumewe. Kwa sasa yuko mkoani Manyara.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni, Dk Slaa ambaye ameripotiwa kuwa na makombora 20 kwa ajili ya kuimaliza CCM, alisema kitendo cha mke huyo wa rais kumpigia kampeni kwa kutumia rasilimali za umma ni ufisadi.

“Mke wa rais si rais," alisema Dk Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwara ulio Babati Mjini.

"Mama Salma anatembea na askari wa serikali; magari ya serikali na wakuu wa mikoa na wilaya. Anatumia fedha za Ikulu kwa sababu walinzi wake wanalipwa na Ikulu. Huu ni ufisadi.”

Dk Slaa, ambaye alikuwa mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema), aliongeza kusema: “Nimepita huko nimeambiwa (mke wa rais) anatembea na msafara wa magari 20 na kila gari moja lina thamani ya Sh200 milioni ambayo pia yanatembea kwa mafuta ya serikali. Ni ufisadi.

“Kama mke wa rais anatembea na msafara wa magari 20, je rais mwenyewe atatembea na msafara wa magari mangapi? Wakati mgombea urais wa Chadema akitembea kwa basi, mke wa rais anatembelea magari ya serikali. Ni ufisadi mkubwa kutumia magari hayo kwa maslahi binafsi.”

Aliyeanza kumlipua Mama Kikwete katika mkutano huo ni mkurugenzi wa kampeni wa Chadema, Suzan Kiwanga ambaye alidai kuwa kama mke huyo wa rais anataka kushiriki kwenye siasa angesajili chama na kuchukua fomu ya kugombea badala ya kutumia Wama.

Kiwanga alidai kuwa Mama Kikwete anafanya ziara hizo bila ya ratiba iliyoidhinishwa na Tume ya Uchaguzi (Nec), akimpigia debe mumuwe jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Nataka nimwambie huyu mtu aitwaye Mama Salma kwamba kiherehere chako kitakufikisha mahali pabaya. Unatumia fedha za wanawake za Wama kwa maslahi yako... ni kinyume cha sheria,” alisema Kiwanga huku akishangiliwa.


Kwa habari zaidi soma: MWANANCHI.
Bila haya Ms. Kibanga anasema huwa anafanya official government activities, hivi ni zipi hizo activities; je, hizo shughuli za kiserikali anazifanya yeye kama nani? Na sheria gani inamtambua na kuzitambua hizo kazi za kiserikali? Hivi kupingia kampeni CCM ndio official government activities? (The Citizen, 3/9/10)
 
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,207
Points
1,500
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
Joined May 19, 2009
13,207 1,500
Bila haya Ms. Kibanga anasema huwa anafanya official government activities, hivi ni zipi hizo activities; je, hizo shughuli za kiserikali anazifanya yeye kama nani? Na sheria gani inamtambua na kuzitambua hizo kazi za kiserikali? Hivi kupingia kampeni CCM ndio official government activities? (The Citizen, 3/9/10)
Anapotumia magari ya Serikali kumfanyia kampeni mumewe?
 
Z

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
875
Points
1,000
Z

Zygot

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
875 1,000


Ni kutokana na kutumia raslimali za Serikali wakati wa kumnadi mumewe kuingia Ikulu wakati yeye si mtumishi wa serikali!

KAMPENI za uchaguzi mkuu zimezidi kunoga baada ya mgombea urais wa Chadema, Dk Slaa kumgeukia mke wa Rais Jakaya Kikwete akieleza kuwa anatumia vibaya rasilimali za nchi kumpigia kampeni mumewe huku akimtaka katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba aeleze kisa cha kufukuzwa ualimu mkuu wa shule ya msingi.
Kwa habari zaidi soma: MWANANCHI.
Hivi huyu Makamba aliwahi kujibu au kueleza sababu ya kufukuzwa ualimu?
 

Forum statistics

Threads 1,284,203
Members 493,978
Posts 30,817,141
Top