Mama Salma Kikwete ulifikiria mara mbili kabla ya kutamka ulichokitamka siku ya Mtoto wa Kike?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Naomba tufanye tafakuri tunduizi ( critical thinking ) kabisa juu ya hii Kauli ' Tata 'kabisa ambayo Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu na Nne Mama Salma Kikwete aliisema / aliitoa katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike duniani wiki iliyoisha.

Mama Salma Kikwete ( ambaye sasa ni Mheshimiwa Mbunge wa Kuteuliwa pia ) aliwaambia Mabinti Tanzania nzima kuwa ' Wajitahidi kubana Mapaja yao ' dhidi ya wale ambao wanapenda ' Kuyapanua ' kwani hao ' Wapanuaji ' wa hayo ' Mapaja ' yao huwa hawana nia nzuri na njema Kwao.

Katika Headline yangu hapo juu nimeuliza kwamba je Mama Salma Kikwete kabla ya kutamka hiyo ' Kauli ' yake alifikiria mara mbili mbili kwa kuzingatia hasa tabia au mienendo ya Watoto wa Kike wa siku hizi nchini Tanzania au alikurupuka tu kuisema ili kuwachafua hao ' Wapanuaji ' wa hayo ' Mapaja ' ya hao Mabinti / Watoto wa Kike?

Hivi Mama Salma Kikwete anatambua kwamba hao ' Wapanuaji ' hayo ' Mapaja ' huwa wanashawishiwa vibaya sana na Wabanaji Mapaja aliowahusia ili ' Wapanuliwe ' vizuri? Hivi Mama Salma Kikwete anatambua kwamba kwa sasa kuna tofauti kubwa sana kati ya Wao ( Mabinti wa zamani ) na hawa Mabinti wa leo hasa Kimaadili?

Siku zingine nyie akina Mama mnapoalikwa katika ' matamasha ' kama haya ya Wanawake / Watoto wa Kike muwe mnajitahidi kuwa makini na kauli zenu / matamko yenu ili msije mkajikuta mnatudhalilisha / mnatutukana Sisi Wanaume badala yake mjikite sana ' Kuwafunda ' hawa Watoto wenu wa Kike ambao kiukweli Sisi wengine huwa tunajitahidi mno ' Kutowapanua ' hayo ' Mapaja ' yao ila kuna muda Uzalendo unatushinda kutokana kwamba hata nasi ni ' Marijali ' vile vile.

Acheni kutulaumu Sisi Wanaume kila uchao na makosa yanayotokana na Upumbavu / Upopoma wa hao Mabinti / Wanafunzi wenu ambao mnawazaa halafu nyie nyie wakiwa bado na Umri mdogo tu mnaanza kuwavalisha ' Vimini ' huku mkiwasifia na hadi kuwataka wapige ' Selfie ' na waweke katika Simu zao na katika mitandao yao ya Kijamii.

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambayo siku zote huwa haikai na uchafu hivyo ni imani yangu kubwa kuwa message sent and delivered.

Mwanamume nawasilisha.
 
Wanaume yatupasa kutumia nguvu zetu kulinda usafi wa moyo na majikatalio.
Dada zetu ni kweli kidogo wanatupa wakati mgumu na kutufanya tutumie nguvu kubwa kujikatalia yapendwayo na mwili.
Dunia nikijiji tunajikuta tunamaadili ya kijiji hiki Dunia na yatupasa tuenende na wakati kwa usahihi ila dada zetu pia mtuonee huruma mtupe ahueni.
Miaka 30 ni mingi sana ipunguzwe kidogo
 
Mi si shangai walimu wale wa UPE,wote akiri zao huwaga hivi.....wanapenda kuongea na mabinti ijumaaa shuleni
Katika maongezi yake akiwa First Lady alisema alifaulu darasa la saba na kwenda kidato cha kwanza mpaka cha nne na baadae chuo cha ualimu, hivyo ni mwalimu wa daraja III A.

Sijawahi kuona wasifu wa maisha yake ukiekezea shule alizosima ana familia aliyozaliwa hata akiwa First Lady.
 
Katika maongezi yake akiwa First Lady alisema alifaulu darasa la saba na kwenda kidato cha kwanza mpaka cha nne na baadae chuo cha ualimu, hivyo ni mwalimu wa darasa III A.

Sijawahi kuona wasifu wa maisha yake ukiekezea shule alizosima ana familia aliyozaliwa hata akiwa First Lady.

Ulitaka kuona wasifu wa mke wa rais ili iweje? Ulishawahi kuona wasifu wa mama maria nyerere ukianikwa hovyo au mama siti mwinyi na ana mkapa? Ulitaka kuona wasifu wa mwandani wa Rais??.. Hebu weka wasifu wa mamaako kwanza tuone makorokocho yake kwanza kabla hujatamani kuona wasifu wa first lady ukianikwa hadharani..haya tuanze na wasifu wa mamaako sasa...
 
Ulitaka kuona wasifu wa mke wa rais ili iweje? Ulishawahi kuona wasifu wa mama maria nyerere ukianikwa hovyo au mama siti mwinyi na ana mkapa? Ulitaka kuona wasifu wa mwandani wa Rais??.. Hebu weka wasifu wa mamaako kwanza tuone makorokocho yake kwanza kabla hujatamani kuona wasifu wa first lady ukianikwa hadharani..haya tuanze na wasifu wa mamaako sasa...
Wasifu wa Michelle Obama, Cherie Blair, Sally Mugabe, Nana Rowlings na wake wa marais wengi mbona uko wazi
 
Siku zingine nyie akina Mama mnapoalikwa katika ' matamasha ' kama haya ya Wanawake / Watoto wa Kike muwe mnajitahidi kuwa makini na kauli zenu / matamko yenu ili msije mkajikuta mnatudhalilisha / mnatutukana Sisi Wanaume
viongozi wote wa awamu hii kwenye kuongea kama hawajaandikiwa script tegemea uchafuzi wa hali ya hewa. Sijui akili huwa yanaweka wapi pale wanaporuhusuwa kupiga free style bila kuandikiwa.
 
Back
Top Bottom