Mama Salma Kikwete: Uchaguzi mkuu 2020 kura zote kwa Dk Magufuli na hatutaacha kata wala jimbo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,852
141,786
First Lady mstaafu, Mama Salma Kikwete, amemhakikishia Rais Magufuli kuwa kura zote za uchaguzi kuanzia serikali za mitaa hadi ule mkuu kutoka Nachingwea zitaenda CCM.

Mama Salma amesema hayo wakati akiwasalimia wananchi wa Nachingwea baada ya kupewa fursa ya kusalimia na Rais Magufuli.

Rais Magufuli yuko ziarani mkoani Lindi akisikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuwashukuru kwa kura nyingi walizompa 2015.

Chanzo: TBC
 
Mkuu ulitegemea mama Salma aseme tofauti na alichosema? Tatizo sio kura zote kwenda kwa Magufuli, bali wapiga kura watakuwa tayari kushiriki uchaguzi ambao Magufuli anatumia madaraka yake kutangazwa mshindi yeye na wagombea wenzake wa ccm?
 
Huyo dada yuko vizuri kwenye kampeni.
Nakumbuka mwaka 2010, CCM walipotezea kumnadi JK, aliingia ulingoni yeye na Rizimoja. Ndio mwishoni akaja mzee Mkapa amefura, eti kwanini wanamsema kuwa CCM wameiachia familia kampeni
 
Ubunge ni mtamu jamani. Kuna watu wanazaliwa na bahati sana, kutoka kushika chaki paap u First Lady baadae u heshimiwa.
 
Back
Top Bottom