Mama Salma Kikwete ni Mheshimiwa?

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
9,205
8,236
Niko Musoma, muda mfupi ujao mama Salma Kikwete atawasili hapa, kufungua maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwa UWT, swali langu liko hapa gari la matangazo linapita mitaani kuhamasisha wananchi wajitokeze kumalaki Mheshimiwa mama Salima Kikwete, Je mama Salma Kikwete ni Mheshimiwa?
Naomba kuwasilisha!
 
Siyo Mheshimiwa ni mke wa Kikwete na hakuna sababu yoyote ya kumuita mheshimiwa labda kama upo punguani utamwita hivyo.
 
Niko Musoma, muda mfupi ujao mama Salma Kikwete atawasili hapa, kufungua maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwa UWT, swali langu liko hapa gari la matangazo linapita mitaani kuhamasisha wananchi wajitokeze kumalaki Mheshimiwa mama Salima Kikwete, Je mama Salma Kikwete ni Mheshimiwa?
Naomba kuwasilisha!

Nani anamuheshimu....?
 
Sherehe za UWT kwa gharama ya serikali.........halafu wanashindwa kulipia pango Mawizara yake
 
Ingekuwa Vizuri tungejua maana ya neno mheshimiwa kabla ya kupost hizi comments zetu.
 
Sherehe za UWT kwa gharama ya serikali.........halafu wanashindwa kulipia pango Mawizara yake

Nashanga! Ndo anawasili sasa MC anasherehesha vilivyo, ''mama yetu mpendwa mh. mama Salama'' Yaaani hata simuelewi, natamani nikamyanganye mic. Halafu wanajamvii kuna kitu kinanitatiza, hivi hizi sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa kila wizara na taasisis zake, hizi gharama zinatoka wapi, sikufuatilia vizuri bajeti za wizara wakati wa bunge la bajeti sababu ya mgao wa umeme, naomba mnijuze. Manake siku nchimbi anafungua haya maadhimisho huko Butiama, dar kwenye ofisi zake vyombo vilikuwa vinatolewa nje kwasababu wameshindwa kulipa kodi. Lol!
 
Mtu gani anastahili kuitwa mheshimiwa na nani hastahili kuitwa. Tuanzie hapo kwanza.
 
Mama ndo ametua sasa naona mchuma wa serikali ndo umemleta
 
sherehe za miaka 50 ya Uhuru ni ufujaji wa pesa tunasheherekea nini haswa kwa linchi lililopoteza mwelekeo...........hosp zetu dawa hakuna wagonjwa wanataabika bila msaada huku wengine wapo busy kusheherekea uhuru ni upu**** mtupu
 
  • Thanks
Reactions: ram
Niko Musoma, muda mfupi ujao mama Salma Kikwete atawasili hapa, kufungua maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kwa UWT, swali langu liko hapa gari la matangazo linapita mitaani kuhamasisha wananchi wajitokeze kumalaki Mheshimiwa mama Salima Kikwete, Je mama Salma Kikwete ni Mheshimiwa?
Naomba kuwasilisha!

Kwenye bold red
Kwani waziri wa jinsia yuko wapi? hili suala la uhuru si ni la kitaifa?
 
Acha upumbavu. Yule ni muheshimiwa penda usipende hata watoto wao ni waheshimiwa.

wakati mwingine jaribu kuuficha upumbavu wako, si lazima uchangie kila thread inayoletwa hapa. Eti hata watoto wao ni waheshimiwa... Wewe ndo wale wale ukimuona Miraji unaanza kutetemeka, utakuwa mtumwa hadi unakufa nyamb**u wewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom