Mama Salma Kikwete na Dr Lilian Mbowe; Mlinganisho wa maswali na majibu waliyoulizwa

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,386
2,000
MAMA SALMA ; source first Lady Salma Kikwete | darhotwire

Swali: Ni ipi historia fupi ya maisha yako?
Jibu: Mimi naitwa Salma Rashid. Nilizaliwa katika wilaya ya Lindi Mjini, Novemba 30, 1963. Baba yangu anaitwa Rashid Yussuf Mkwachu na mama yangu ni Mwanapaza binti Shariff.

Kwa asili, baba yangu anatoka Sarai, Rufiji mkoani Pwani na mama yangu anatoka Lindi.
Katika familia yetu, upande wa mama, tulizaliwa watoto saba, wasichana watatu na wavulana wanne. Mimi ni wa sita, ila kwa baba ni wa pili, nina kaka yangu na mdogo wangu. Nina wadogo zangu wengine watatu ambao tunachangia baba, kati yao wavulana ni wawili na msichana mmoja.
Baba yangu alikuwa mfanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 na kituo chake cha kazi kilikuwa Mtwara, wakati baba anafanya kazi, mama alibaki Lindi, hali ambayo ilinifanya nipate elimu yangu ya msingi kuanzia mwaka 1973 katika shule nne tofauti; Nnaida ya Mikindani, Mtwara, Rahaleo ya Lindi, Ligula (Mtwara) na Stadium, Lindi ambapo nilimalizia elimu yangu ya msingi.
Ingawa wakati ule nafasi za kujiunga na sekondari zilikuwa chache, namshukuru Mwenyezi Mungu nilikuwa miongoni mwa waliochaguliwa.
Swali: Wewe unatoka Lindi na Mheshimiwa Rais anatoka Pwani, mlikutana wapi na mlifunga ndoa lini? Jibu: Kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu. Nilikutana na mume wangu mwaka 1985 nikiwa katika Chuo cha Ualimu Nachingwea, yeye akiwa ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Nachingwea.

Tulipokutana kwa mara ya kwanza kitu ambacho aliniambia ni kwamba nakupenda na nataka nikuoe kusema kweli hakusema anataka awe rafiki yangu au vipi, sijui kama huo ndio utaratibu wa kina baba wote, lakini nasema kutoka moyoni, hicho ndicho alichoniambia na mimi kwa sababu nilimpenda, nilimkubalia, ingawa uamuzi wangu sikuutoa papo hapo.
Tulifunga ndoa Machi 30, 1989 wakati huo yeye akiwa Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini. Swali: Baada ya kufunga ndoa ikawaje? Jibu: Baada ya kufunga ndoa nilifanya taratibu za uhamisho kwa mujibu wa taratibu za kikazi.
Kwa hiyo nilihamia Dar es Salaam ambapo niliungana na mume wangu na tukawa tunakaa Mikocheni mtaa wa Ursino.
Swali: Katika miaka yenu hii 20 ya ndoa mmejaaliwa kupata watoto wangapi na wako wapi?
Jibu: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumejaaliwa watoto watano kati yao wanne ni wa kiume na mmoja wa kike. Wote wanasoma, wa kwanza yuko kidato cha sita, wa pili cha nne, wa tatu cha pili, wa nne yuko darasa la tano na wa mwisho yuko darasa la tatu.

Lakini kwa ujumla tuna watoto wanane, ikiwa ni pamoja na watatu ambao mume wangu alipata na mke wake wa kwanza.

Hawa wakubwa mmoja ni mwanasheria, mwingine ni daktari na mwingine ni mtaalamu wa Teknohama (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

Ila siku zote napenda kusema tuna watoto wanane kwa sababu hata hawa wakubwa nimewalea mimi tangu wakiwa na umri mdogo sana. Kwa hiyo hawa ni watoto wangu sawa sawa na hawa niliowazaa mimi.

Swali: Una mipango gani ya baadaye?

Jibu: Kwa jumla mipango yetu katika taasisi ya WAMA ni mikubwa sana. Sasa ndio tumeanza, tuna shule moja tu, lakini tunatarajia kuongeza shule nyingi zaidi katika maeneo tuliyoyakusudia kwa sababu watoto wanaohitaji msaada wako wengi sana.DR LILIAN MBOWEsource-https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/329499-dr-lilian-mbowe-interview-alofanya-na-kipindi-cha-wanawake-live-eatumanne.html

Aliulizwa yeye ni mke wa mtu mwenye nafasi kubwa katika jamii (kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ndugu Aikael Mbowe), wana mali na maisha mazuri inakuwaje anachapa kazi kwa bidii?


Mimi ni mwanamke msomi wa degree na masters ya udaktari, nimelelewa katika mantiki ya kujijenga mimi kama mimi na nisitegemee mtu mwingine. Mimi kuolewa na mwanaume mwenye fursa ktk jamii siyo tija na kuna kitu ktk roho yangu kinachoniambia lazima nifanye kazi.Siamini katika mantiki ya kula kulala, hata kama pesa ipo lazima mtu ufanye kazi fulani kusudi uweze kuijenga ile pesa, kuingiza kipato na kujua kinachotokea.Kama ningekuwa amelala nyumbani sifanyi kitu chochote,tatizo laweza tokea, kuna leo na kesho.Leo niko na mume wangu kesho na kesho kutwa siko naye .Sasa baada ya hapo nitakwenda wapi? Au baada ya hapo nitafanya nini?

Je wanawake tegemezi wapo?

Kadri siku zinavyo kwenda kina mama nao wanaanza kujipatia kipato. Kuna kupewa lakini kupewa huko kuna mwisho wake.Kadri siku zinavyo kwenda zana ya mama wa nyumbani inatoweka, /inapungua kwa kina mama wengi.Lakini bado wako wengine wanapenda maisha ya kufurahia mali na position /kazi za waume zao na kutake advantage.

Unawaambia nini wanawake wategemezi?
Wawe waangalifu,kazi za watu zinapanda na kushuka, biashara nazo zinacollapse zinaisha,kuna kuchukuliwa na mwenyezi Mungu ghafla tu,sasa mama kama hujasimama na miguu yako miwili unaweza kupata shida sana.

Ushauri kwa wanaume wanaodekeza wake zao;
Sidhani kama ni vizuri kudekeza mwanamke,kuna dini na mila zisemazo kwamba mwanaume ndo anatunza mwanamke lakini kwa karne hii ya 21 sidhani kama twaweza kuendelea kushikilia mila za zamani za kusema mwanamke tu atunzwe.Kwajinsi maisha yanavyokwenda na baadhi ya mambo kubadilika, wanaume wengi wanaona nikiondoka leo, au nikimpa talaka huyu mwanamke anaweza akapata shida, hivyo kama unampenda mwenzio, nashauri kinababa wajaribu kusukuma kina mama wajaribu kufanya kitu chochote cha kujiendeleza, badala ya kuwadekeza sana na wao kubakia wanashughulikia kila kitu.

Anasema ana bahati mumewe siyo wa aina ile ya wanaume kudekeza wanawake na kuwaacha wakae tu idle, while wao wakiprovide kila kitu.Ana mume ambaye naye ndiye anayemsukuma na anamwambia kwamba lazima uwe na maisha yako lazima uwe na vitu vyako, lazima ujijenge. Anasema Kama siku hizi huwa wanagombana maana anamwambia lazima aende akasomee MBA, ukizingatia she is a doctor by profession, lakini sasa anashughulika na family business so mumewe anamsukuma asome zaidi hataki abaki hapo alipo anamshawishi achukue MBA ili aweze kufanya biashara vizuri.
 

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
527
500
Naona kama wameulizwa maswali tofauti hivyo inakuwa ngumu kuwacompare japo kielimu mmoja yuko juu ya mwingine. Aafu mbona mjukuu wa meghji na yule alokuwa mkuu wa mkoa wa mbeya kasahaulika?(just thinking loudly)
 

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,942
2,000
No comment bali mmoja maswali yamejibiwa kulingana na elimu ya mtu na silka ya watu anaokutana nao mara kwa mara
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,228
2,000
This is a joke mlinganisho wa mtu mwenye Masters tena ya udaktari na mwalimu wa UPE! Huoni huyo wa UPE kaambiwa ajieleze tu historia yake! sasa unafikiri angeulizwa nini zaidi! Ritz si uonevu huu!
 
Last edited by a moderator:

Dangire

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
221
225
kwani lengo lako lilikuwa ni nini? mbona maswali uliyowasilisha ni tofauti? jipange upya.
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
2,000
Pamoja na kuwa ni maswali tofauti, lakini mtu unaweza kujua uwezo wa kufikiri na upeo wa mtu kutokana na jinsi alivyojibu swali
 

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,476
2,000
Mlinganisho wako ungekuwa mzuri kama wote wangeulizwa maswali yanayofanana, sasa hapa kila mtu ameulizwa swali tofauti na mwingine. Kwa maoni yangu kila mtu amejibu vizuri maswali aliyoulizwa.

hata mimi nimeliona hilo,you cant make comparison whilst they have been asked different questions
 

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
2,000
Mlinganisho wako ungekuwa mzuri kama wote wangeulizwa maswali yanayofanana, sasa hapa kila mtu ameulizwa swali tofauti na mwingine. Kwa maoni yangu kila mtu amejibu vizuri maswali aliyoulizwa.

Maswali ya kisomi wanaulizwa wasomi, wewe ulitaka semi-illiterate aulizwe maswali sawa na masters holder?
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Sioni mantiki ya huu ulinganisho hapa? Hakuna msingi wowote wa kuweza kutoa judgement ya kwamba nani kasema vizuri au vibaya. Kila mmoja kajibu kulingana na maswali yake. Sema tu huyo Liliani Mbowe anaonekana ni mtu wa majisifa. Maana hakuulizwa elimu yake, yeye akaanza kujibu swali ambalo hajaulizwa (alitaka kujionyesha kwamba yupo juu).
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,302
2,000
Haya mtoa mada jazia nyama basi, maana ni upande mmoja tu umeuliza, je? huku kwingine kaolewa lini na watoto wangapi si vibaya ukawajuza wanaJF kuliko kumwaga upande mmmoja
 

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,476
2,000
Pamoja na kuwa ni maswali tofauti, lakini mtu unaweza kujua uwezo wa kufikiri na upeo wa mtu kutokana na jinsi alivyojibu swali

katika hali ya kawaida huwezi kuwa watu mitihani miwili tofauti then ukwa judge sawasawa kwa alama walizopata,hapo utakuwa hujatenda haki
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
2,000
katika hali ya kawaida huwezi kuwa watu mitihani miwili tofauti then ukwa judge sawasawa kwa alama walizopata,hapo utakuwa hujatenda haki
Elewa kuwa my judgment does not base kwenye euelwa wa maswali, bali uelewa (wa jumla) na upeo wa mjibuji maswali
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
7,376
2,000
Huku ni kumwonea Mama Salma, kwani Mrs Mbowe angeulizwa maswali ya kifamilia angejibu nini cha tofauti? Hakuna usomi kwenye maisha binafsi labda ingekuwa maswala ya upembuzi wa uchumi na sera.
 

Heavy equipment

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,358
2,000
Baba yake salma kikwete alikuwa anafanya kazi east africa mwaka 1977 je? baba yake salma kikwete alishawai kuandamana kudai zile pesa ambazo wazee wetu wengine ziliwasabishia kupigwa mabomu?
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,088
2,000
hakuna mlinganisho hapa ni usaniii tu

Unaipima chunvi kwa kilogram na kupima dhahabu kwa pound halafu unaangalia tarakimu kulinganisha ipi kubwa??? kweli??? bila common ground of references ....!!!!!!!

Lazima wote wawe kwenye maswali yaleyale na kwa mazingira fananishi ndipo uwapime kuupata ukweli.
 

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,843
2,000
mbona wale watoto mkulu alizaa na VIKIII KAMATA hawajumuishwa katika hao wanane msifanye watu mazuzu, after all, hata huyo Dk. Mtei ambae ni mtoto wa aliyekuwa Gavana wa BoT na Mwenyekiti & Muanzilishi wa CHADEMa, sasa ni mke wa Mbowe bado si mtu wa kutolea mfano Kuwa na BILICANAS ndo kufanya kazi kwa bidii tolea mfano mtu alitoka/aliyefanikiwa kwa bidii zake mwenyewe toka chini na si jitihada za Baba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom