cleokippo
JF-Expert Member
- Dec 21, 2014
- 2,072
- 1,697
waache wale mkuu mpaka wajiharishie , wala hatupaswi kumlaumu kwa hoja yake kwani ujinga tumeofanya sisi wenyewe japo uyo bi mkubwa ubunge wake wa kupewaKwa kweli nilishtushwa Sana niliposikia mama Salma Kikwete, akilitumia Bunge la Jamhuri ya Tanzania, badala ya kuongelea Shida za watu wa Jimbo lake la Mchinga, anaongelea mambo yake binafsi.
Eti anataka yeye kama mke wa Rais mstaafu, naye alipwe pension!
Hivi hawa viongozi wa CCM wanatuonaje watanzania?
Hivi Katika kipindi kama hiki, ambacho Taifa linapitia Katika kipindi kigumu mno cha uchumi, kwa kupanda bei kwa kila kitu, kutokana na kupanda Sana kwa bei za mafuta, wakati kipato cha mtanzania hakijaongezeka, hivi ni wakati sahihi wa kutumbukiza maoni binafsi ya kuomba kulipwa pension kwa ajili tu ya kuwa ni mke wa Rais mstaafu?
Hata hivyo nimuulize mama Salma, hivi hatosheki na kipato anachopata cha maslahi ya ubunge wa "kupewa" wa kipato cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ukiacha maslahi mengine ya Mheshimiwa mbunge, kama vile "seating allowance" ya kila kikao cha Bunge kinavyoendelea?
Hebu nimuulize tena mama Salma, hivi haridhiki na pension anayolipwa mumewe, Jakaya Kikwete, ya kuwa Rais mstaafu, ambayo ni 80% ya mshahara aliokuwa akiupata alipokuwa Rais wa nchi hii?
Hebu pia nimuulize mama Salma, hivi haridhiki na "upendeleo" aliopewa mwanaye Ridhiwani Kikwete, ya ubunge, ambapo pia "amezawadiwa" u-Naibu Waziri, ambapo anapata maslahi kibao?
Hivi mama Salma, hayaoni matatizo ya mamilioni ya watanzania, wanaohangaika kila kukicha, kutafuta riziki zao za kila siku, ambao hata wakifika umri wa uzeeni hawalipwi pension yoyote?
Hivi mama Salma, hayo uliyoyaongelea Bungeni, ndiyo mawazo ya wapiga kura wako wa Jimbo la Mchinga, waliyokutuma uwasemee?
Hakika baada ya kusikia kauli za mama Salma, alizozitoa Bungeni, nmeamini kabisa, kuwa hatuna wawakilishi wa wananchi huko Bungeni, bali tuna viwavi wa CCM wanaotaka kula kwa kuvimbiwa na watuache watanzania tukiwa hatuna kitu kabisa!
Nimeamini kuwa nchi hii kuendelea kuwachagua wawakilishi toka chama tawala cha CCM ni kuendeleza laana, ambayo itaendelea kututafuna kwa vizazi vingi vijavyo!
inatakiwa tujifunze sasa ili tusifanye makosa 2025
mtu mumewe alikuwa Rais ana pensheni za kutosha, mtoto ni naibu wazir, Mama ni mbunge lakini cha kusikitisha bado anaendekeza njaa tu
kweli kuna viongozi wengine ni viwavi jeshi jaman