Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,178
- 876
Salma atesa na ndege ya Kikwete
Ni ile ambayo rais anaogopa kuitumia kikazi Ulaya
Aipanda kwenda na kurejea katika ziara binafsi
Aitumia kuendea sherehe za mila za Mswati III
na Mwandishi Wetu
BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kuogopa kutumia ndege yake iliyonunuliwa kwa mabilioni ya shilingi bila idhini ya Watanzania, sasa ndege hiyo inatumiwa na mkewe, Salma katika ziara binafsi.
Mara ya mwisho, Salma alitumia ndege hiyo kwenda kwenye sherehe za kimila nchini Swaziland, kushuhudia Mfalme Mswati III akichagua mke wa 13.
Uchunguzi wa Tanzania Daima umethibitisha kuwa Salma aliondoka Dar es Salaam Agosti 29, mwaka huu saa tisa jioni, akiwa amepanda ndege hiyo aina ya Gulfstreame Jet Engine kwenda Manzini, Swaziland.
Ndege hiyo ya rais namba 05H-ONE, iliondoka Dar es Salaam kuelekea Swaziland, alikokuwa anakwenda kuhudhuria sherehe za kimila, ambazo baadaye zimeshutumiwa na wanaharakati kwamba zinawadhalilisha wanawake.
Septemba 5, mwaka huu, ndege hiyo ilimfuata na kumrejesha Dar es Salaam.
Kwa hakika haya ni matumizi mabaya ya ndege ya rais, kwa kuwa mke wa rais, si rais, na hapaswi kuitumia kama anasafiri peke yake kwa safari binafsi.
Fursa pekee aliyonayo mke wa rais kutumia ndege hiyo, isiyoweza kunungunikiwa hata kidogo, ni pale anaposafiri na mumewe katika safari za kikazi.
Matumizi haya ni kashfa nzito kwa serikali ya awamu ya nne, inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, aliyesema tangu awali kwamba urais wake usingekuwa wa ubia na mtu yeyote.
Miezi miwili iliyopita, gazeti hili liliandika habari kuwa Rais Kikwete anahofu kupanda ndege hiyo katika safari zake za kikazi Ulaya, kwa madai kuwa ni gharama kubwa mno kwa nchi maskini kama Tanzania.
Badala yake, ameazimia kuitumia katika safari za Afrika, hali inayotafsiriwa pia kuwa anaona aibu kupanda ndege ya kifahari kwenda Ulaya kuomba misaada kwa serikali zinazoongozwa na viongozi wanaotumia ndege za kawaida katika safari zao za kikazi.