Mama Salma Kikwete asalimiwa kwa ishara ya Chadema na Wanafunzi wa Shule

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,416
12,604
Nimesikia taarifa ya habari Clouds FM asubuhi ya kwamba Mama Salma Kikwete alisalimiwa na wanafunzi kwa ishara ya vidole viwili na wanafunzi wa primary.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tukio lilifanyika wakati wa ufunguzi wa madarasa mawili na ugawaji wa madawati katika shule hiyo (Wilayani Bunda kama sijakosei).

Baada ya salamu hiyo 1st Lady alimgeukia mkuu wa wilaya na kumwabia hivi ndivyo mnavyowafundisha watoto hawa.

Hii imekaaje wadau, ina maana watoto nao ni Chadema damu au wamefundishwa na waalimu wao kufanya hivyo.
 
hahahhahah!! kimewakaaaaaa!
kwa hiyo anajifanya hajui sababu?
na bado-kingwendu
 
Nilikuwa barabarani wakati inatangazwa, sikupata details zote. Naomba mtu mwenye taarifa kamili atupe news make nimeipenda sana hii.

Naomba imtokee na mwenye kaya siku moja. Aghaaaaaaa.
 
v.jpg Hii alama ina maana nyingi. Inamaanisha vilevile 'amani'. Huyo Headmaster asije akakurupuka kuwaadhibu hao vijana!
 
View attachment 30390Hii alama ina maana nyingi. Inamaanisha vilevile 'amani'. Huyo Headmaster asije akakurupuka kuwaadhibu hao vijana!

Pia inamanisha ushindi.Kwani huyo SK anahamaki nini kwani hata kama wangemaanisha CDM ni dhambi? Mbona yeye mwanawe ni kiongozi wa chipukizi wa magamba? Mwambieni aache ushamba wa kimachinga hapa.
 
kama pia anamaanisha amani basi ccm pia waitumie , kwa kifupi na furaha mi binafsi naipenda sana si kwa ajili ya amani no bali kwa kuwa inatumika na chama langu la ukweli peoplezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
View attachment 30390Hii alama ina maana nyingi. Inamaanisha vilevile 'amani'. Huyo Headmaster asije akakurupuka kuwaadhibu hao vijana!
 
Kwanza huyo mama inaonekana naye ni kilaza tu, kwani hajui mazingira nisehemu ya darasa maishani kwanini amuulize mkuu wa wilaya? Yeye kama mwalimu mzoefu hakupaswa kuuliza hilo bali alitakiwa akifika ikulu ambane mzee wa kaya ili awe siriazi zaidi na maswala ya kitaifa badala ya kimataifa.
 
atajipanga!! mbeya walishamfanyiaga huu mchezo, tena ni akina mama wa rika lake!!hapo wa kuulizwa ni wazazi pia.
 

Attachments

  • cdm simbol.jpg
    cdm simbol.jpg
    5.4 KB · Views: 37
  • cdm simbol.morgan tvangirai.jpg
    cdm simbol.morgan tvangirai.jpg
    5.8 KB · Views: 36
  • xhuma s.africa.jpg
    xhuma s.africa.jpg
    5.6 KB · Views: 39
Lazima binadamu wote wawe na uhuru wa kuabudu na kupenda chama chochote............
 
Hawa wanafunzi damu ya harakati imeanza kuwaingia,mambo ndiyo yameanza kwa kuikomboa TANZANIA kwa mara ya PILI.
 
Safi sana hao ndio watakaoendeleza mapambano na kuongoza nchi siku za baadaye
 
Na hili ni kama onyo la awali, Tunamsubiri mkuu wa kaya ajaribu kutembea mikoani aone moto wake.
 
Napenda kuwapa taarifa zilizonifikia hivi punde,TANZANIA HALI NI TETE SANA KWANI WATOTO WENGI SANA WA MASIKINI WANAHOJI NINI SISI WAKUBWA TUMESHINDWA KUPAMBANA NA MAFISADI?JAMANI SIYO SIRI YAWEZEKANA SANA MKOMBOZI WA SISI WANYONGE AKAWA MTOTO MDOGO.
 
Back
Top Bottom