Mama Salma Kikwete alalamikia kuonyeshwa alama ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Salma Kikwete alalamikia kuonyeshwa alama ya Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 21, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAWA WANAWAKE WA MBEYA WAMEVUNJA REKODI KWA KUWA MNO WAWAZI. HUKO MOSHI HUWA WANAMSHANGILIA LAKINI AKISHAONDOKA WANAMSENGENYA NA KUMCHARURA KISHA WANAAAPA KUTOKIPIGIA KURA CHAMA CHAKE.
  HAPA WANAMUONYESHA WAZI KUWA WAO NI CHADEMA? NAOMBA WANAWAKE MSIENDELEE KUMTESA MAMA YETU. ACHENI APITE KWA AMANI KUOMBA KURA.
  JAPO MNALALAMIKA ANAOMBA ZA FAMILIA. SITAKI MUMTESE MKE WA RAIS HATA KAMA ANAMALIZA MUDA WAKE MPUNGIENI TAFADHALI.  NA THOBIAS MWANAKATWE
  21st October 2010
  B-pepe
  Chapa
  Maoni

  Mke wa Rais , Salma Kikwete
  Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
  Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
  “Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana,” alisema.
  Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
  Mama Kikwete alisema wanawake waonyeshe msimamo kwa kukipigania Chama cha Mapinduzi (CCM).
  “Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,”alisema Mama Salma Kikwete.
  Alisema wanawake ambao kura hazikutosha wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM hawana sababu ya kuendelea kukaa na kinyongo na badala yake wawape ushirikiano walioshinda kuhakikisha CCM inapata ushindi.
  Aliongeza kuwa wanawake wana kila sababu ya kujivunia na kutembea kifua mbele kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na wanawake wenyewe kuinuliwa katika ngazi za maamuzi.
  Alisema wanawake wana kila sababu ya kujivunia maendeleo ya wanawake kama ilivyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro ambaye ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa Tanzania.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ahaaaaaaaaaaa sasa si angeuchuna tu duh watu wengine noma wamempa za uso
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Huyu maza bwana ananifurahishaga kweli. Yaani serikali ya mumewe inapiga vita matamko ya Tamwa kwamba yanashabikia siasa, yeye na WAMA yake wanafanyaga siasa mchana kweupeee na usiku wa manane..

  Mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 4. J

  Jemedari Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kazi kwake............
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  huyu mama legelege sana, ingekua na uwezo ningemwambia JK aache kumtanguliza mbele za watu anaaibisha sana, uwezo wake ni mdogo.
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli habari hii ni njema kwa mageuzi ya nchi na mwamko wa siasa za nchi kwa ujumla wake. Ila kwa yeye mama angekaa kimya busara yake ingeng'aa zaidi ya alichofanya. Kwa kuwa kusema alichosema ni kufagilia CHADEMA na naamini hili halikuwa lengo lake.
   
 7. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu mama mzee anampeti saa ngapi? make anabidii kuliko Rais mwenyewe! Au mzee anakiwee na kule kusini hakusisimuki tena Dr wa ukweli amesha maliza kila kitu!
   
Loading...