Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mama Salma Kikwete amewaonya wanaume kuacha tabia ya kuwaambia wanafunzi wa kike wa shule za msingi na Sekondari kwamba wamependeza.
Alisema kauli ya kupendeza haina lengo jingine bali kuwarubuni na kuwashawishi kufanya nao mapenzi.
Kauli ya mama Salma ambaye ni mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ni ya pili katika kipindi kifupi baada ya ile ya kuwataka watoto wa kike kubana mapaja yao ili kuepuka mimba za utotoni.
Akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku mtoto wa kike Oktoba 11 mwaka huu, chini ya shirika la Room to Read mailimoja mkoani Pwani, mbunge huyo wa kuteuliwa alisema watoto wa kike lazima watambue thamani ya usichana wao kwa kufunga mapaja, kwani kufanya hivyo hakuna mdudu yeyote atakayeingia katikati yake.
"Nimelazimika kutumia lugha hii nyepesi ili watoto wote wanielewe ninachomaanisha, itaweza kusaidia kuliko kutumia lugha ngumu ambayo inaacha maswali", alisema.
Kauli ya sasa ameitoa katika mahafali ya Sekondari ya St Marcus ya mkoani Songwe Oktoba 23 mwaka huu, ambapo aliwaambia wahitimu wa kidato cha nne, wazazi wa wanafunzi kwamba tabia ya kuwasifia watoto wa kike kuwa wamependeza inazidi kushamiri lakini lengo kuu ni kuwashawishi kimapenzi.
"Niwaambie wanaume wote wanaowaambia wasichana wa shule kuwa wamependeza kwa lengo la kuwashawishi kufanya nao mapenzi wakome... Waache kuwarubuni kwa maneno hayo machafu ambayo hayafai kwa watoto wa shule", alisema mama Salma Kikwete.
Chanzo: Mtanzania