Mama Salma ananitia kichefuchefu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Salma ananitia kichefuchefu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Sep 15, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,441
  Likes Received: 1,749
  Trophy Points: 280
  Kutoa maagizo kwa mkuu wa mkoa wa Mara, Mafuru, awaambie wana usalama wampeleke yule mjane ikulu ndogo ili amweleze shida zake ni sahihi kweli? Kwa nini asitoe maagizo kwa mwenyekiti wa UWT? Hivi nae akiwa peke yake anafikia Ikulu ndogo?

  "Rushwa ilipingwa na nchi yetu zama za TANU hata vyama vya upinzani havikuwepo, ambapo katika ahadi za wana TANU zilisema kuwa rushwa ni adui wa haki sitatoa wala kupokea rushwa sasa kama kwa wapinzani kama hawana sera wanyamaze kuliko kusema kitu wasichokijua" alisema Mama Salma (Mtanzania, 15/09/2010, uk. 3).

  Moja, huyu mama hajui historia ya nchi yetu, kwani wakati wa miaka ya mwanzo baada ya uhuru kulikuwa na vyama vya upinzani. Pili, vita vya rushwa si vya maneno ni vya vitendo; je, Andy Chenge na Idrissa kuhusu rushwa ya rada CCM na chombo chake TAKUKURU wamewafanya nini mpaka sasa? Tatu, hivi Dr. Slaa na Prof. Lipumba hawaijui hii nchi kama anavyoijua huyu mama? Nne, naomba huyu mama alete data zenye inference kutoa ushahidi dhidi ya vita ya rushwa na ushindi wa serikali kwenye vita hivyo. tano, atuambie kwa nini ripoti ya Warioba sehemu ya pili imefichwa kabisa na serikali? Sita, hivi kati ya mumewe na Dr. Slaa nani ameiga kutumia helikopta kwenye kampeni? Saba, hivi WAMA ni sister organisation ya UWT?
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 145
  hasira hizo mkuu... taratibu

  FYI, wengi wanamu-ignore tu huyu mama... hana impact yoyote kwa taifa aisee, labda kwenye fashion za nguo na vilemba
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,251
  Likes Received: 15,059
  Trophy Points: 280
  Bwana ehhh.........
  Nasikia yuko mbioni kufunguliwa mashtaka.
  Sijui kama hiyo kesi itafanikiwa,
  maana hao ndio walio shika mpini.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huyu mama naye! Akitoka mumewe naona yeye atagombea kama mama clinton kajikita kwenye siasa mno
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ni kulewa madaraka tu, otherwise hana uelewa wowote wa nafasi yake kama firstLady!...Kipofu kaona mwezi!
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,140
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  huwa ananikera sana huyu mama hana maana kabisa

  bora afuatane na mumewe
   
 7. Davis

  Davis Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hana jambo la msingi ndio maana anaongelea simulizii na si historia. Hivi anayo madalaka ya kutoa maagizo kwa mkuu wa mkoa? Nafikiri yeye anaweza kufanya hayo huko WAMA na kwingineko. Ashakum si matusi!
   
 8. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,452
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Hawawezi kufuatana,wataumizana roho tuu..kila sehemu anayokuwepo mjamaa kuna totoz!
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 10,644
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  We acha tu hii ndo tz ya kikwete...........
   
 10. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sababu nyingine ya kuiangusha CCM ya Kikwete ni kwamba ameshindwa kuheshimu sheria na katiba ya nchi aliyoahidi kuilinda. Mkewe amejikweza na kujipa uwaziri na utendaji katika serikali ambao haupo kwenye katiba ya nchi hii.
  Na anaiingiza nchi kwenye gharama zisizo za lazima kwa safari zisizo na manufaa kwa Watanzania
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,271
  Likes Received: 3,947
  Trophy Points: 280
  Tafadhali uisimwite Mama....hili ni neno tukufu...watu wanaoleta kichefuchefu hawawezi kuwa mama....mwite Salima inatosha au Mrs.Kikwete
   
 12. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #12
  Sep 15, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu mama ni mke wa ndoa wa JK au ni nyumba ndogo?
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 145
  heshima kidogo mkuu.... mbona unaleta za kuleta?
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,271
  Likes Received: 3,947
  Trophy Points: 280
  Mjibu basi kaka....pengine hajui...tueleze walifunga ndoa lini na wapi an mapicha kama ya yule ya Josephine kama yapo
   
 15. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndo maana Museveni wa Uganda kwa kuyaona haya alimpa mkewe uwaziri...........:confused2:
   
 16. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hee ndugu! uko serious au unatania!! kama hujui basi huyu ndo mwenye sauti NYUMBA NYEUPE Palee magogoni, Mzee Chekacheka kazi yake ni kutangaza tu alichotaka Bi Mkubwa.
   
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 21,568
  Likes Received: 15,943
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani wafuatane, mama yuko kwenye kampeni ya SHUKA KWA SHUKA
   
Loading...