Mama Salma amvaa Waziri Mkuu bungeni kuhusu ufisadi wa bilioni 30

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Aliuliza kuhusu Bodi ya Korosho inadaiwa kufanya korosho ufisadi wa bilioni 30 ila serikali haijatoa tamko, serikali inasemaje kuhusu ubadhirifu huo hasa kwa mikoa ya Mtwara na Lindi

Waziri mkuu amasema serikali itavifanyia ukaguzi wa kina kwa vyama vyote nchi nzima kutoaka na vyama hivyo kuwa na hali mbaya na hasara iliyptokea ni bilioni 6 na sio 30 baada ya kamati kuchunguza, na hasara hiyo haikusababishwa na bodi ila imesababishwa na vyama vya ushirika

Mechi za ugenini!

Napenda mkondo wa siasa unapobadilika.Inaleta raha kidogo.Watu wa chama kimoja kulumbana kwa hoja ndiyo msingi wa Maendeleo thabiti na kuondokana na dhana ya kiafrika ya "Wakwetu" hakosei na hata akikosea tutarekebishana baadaye chumbani.

Hiki ndicho kiichokuwa kikifanyika Athens na Great Thinkers,Elite philosophers na Critical thinkers.Huku Afrika unaitwa "Msaliti".Hii ni aibu sana.

Hongera sana Mama Salma kwa Kui-reason Chama Chenu.
 
Hajaongea lolote kuhusu escrow wakati mumewe wanachota kodi za watanzania kwenye mifuko ya sandarusi? Maajabu hayataisha nchi hii
Mama Salma ni zao la Jamii yetu ilivyo!

Hakutoka peponi na wala si Malaika.Hatufunzwi kuusema ukweli na hatutokaa tuuseme ukweli.Kuanzia ndani kwenu,Jamii yako na hata katika ngazi ya Kitaifa.Ni kuufumbia macho ukweli Mwazo mwisho.

Hatuna Mama mwenye uwezo wa kuusema wizi wa Baba hadharani.
 
Anatafuta kiki ya kwenda kugombea ubunge ufisadi ulikuwepo tangu alipokuwa madarakani Mzee.
 
Hii mbinu inayotumiwa ni hatari sana. Watu wa maeneo husika fungueni macho muone, mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo anawanyemelea taratibu. Kwa kuanzia tumuulize ule mfuko aliokuwa akiusimamia enzi za ufirst lady wake ulikusanya jumla ya Tsh. Ngapi na zilitumikaje?
 
Aliuliza kuhusu Bodi ya Korosho inadaiwa kufanya korosho ufisadi wa bilioni 30 ila serikali haijatoa tamko, serikali inasemaje kuhusu ubadhirifu huo hasa kwa mikoa ya Mtwara na Lindi

Waziri mkuu amasema serikali itavifanyia ukaguzi wa kina kwa vyama vyote nchi nzima kutoaka na vyama hivyo kuwa na hali mbaya na hasara iliyptokea ni bilioni 6 na sio 30 baada ya kamati kuchunguza, na hasara hiyo haikusababishwa na bodi ila imesababishwa na vyama vya ushirika

Vp hajagusia ule wa lugumi?
 
Back
Top Bottom