Mama Rwakatare ni Mtakatifu au Mtakavitu?

Mijadala ya dini huwa haimalizi mduara (closing the loop). Ya Kaizari tumwachie Kaizari na ya Mungu tumuachie Mungu. Tangu mijadala hii ilipoanza enzi na enzi haijawahi kutokea muafaka, na ndio maana kuna madhehebu kedekede.
 
hivi kweli unaushahidi wowote kuwa mama Rwakatare amedanganywa na wale watoto au unaropoka tu?
 
Personally huwa nayakumbuka maneno ya biblia kuwa watakuja ibuka manabii wa uongo naona ndo hawa wahubiri wetu ambao Frankly speaking wanaganga njaa.

Wale watoto mpaka wazazi wao wameadmit udhalimu wa watoto wao kuwa hutumikaga kwenye wizi na vitendo viovu.Unajua logic yao ni kuwa hawa watoto waliangushwa na nyungo zao kwa nguvu ya maombi kumbe sivyo lengo apa ni kupata waumini wengi zaidi as that mama she is purerly an entrepreneur .Ili aonekane amezishinda nguvu za giza.

Kwa mtu ambae amesoma bible deep,i only spent six years on divinity & bible knowledge huyo mama anachohubiri kumuelewa ni shida na usipoangalia aweza kuerrode ufahamu wako juu ya mambo mbalimbali ya biblia.

Tabu ni kwamba dunia right now iko na problems nyingi as a result watu wanakuwa stranded if not confused na izo problem hasa wanawake(samahani mwafrika wa kike kwa ilo and she-creatures wengineo) ni rahisi mno kuvutwa na vijineno vya hawa wahubili wasiokuwa na mbele wala nyuma kwa visingizio vya ushuhuda ambao most of the time unakuwa umepikwa.

Inatupasa kuwa makini na wahubiri wa siku izi ambao wanadiriki ata kujitangaza kwa lengo la kupata waumini wengi.Thus spending millions of money kununua program via TV NA RADIO.Mind you kununua one hour iwe star au ITV is not less than 500,000 tshs.
Ebu fanya kwa mwezi then kwa mwaka and see how much is used on that.To me it would have been Ideal izo ela zingeenda kwa masikini.
 
Mwacheni jamani akale wapi?

Km ni hivyo wataachwa wengi; hata mafisadi!

Huyu mama si tu km anapo pa kula, bali pia ana uwezo wa kuwapa wengine mahali pa kula.

Hii ni hulka tu ya biandamu, walio wengi; hawaridhiki na daraja/madaraja ya mafanikio waliyoyafikia. Akipata utajiri, anatufuta umashuhuri (km hanao); akipata umashuhuri, anatafuta kuonekana kuwa karibu zaidi na Mungu kuliko watu wengine (km "nabii na mtume Josephat Mwingira" na "nabii G. Lwakatare"); akifanikiwa kuwaokota watu ktk hili (km alivyofanikiwa huyu mama na Mwingira), atataka sasa aabudiwe!
 
NIMETUMIA NENO ...MTU WA MUNGU....KWA MWONGOZO WA KIBIBLIA......!

HEBU TUREJEE KWENYE GOMBO LA CHUO TUONE MATUMIZI HASA YA NENO HILO.....!
SOMA 2KINGS 1:9(2WAFALME 1:9)......HAPO TUMEENDA MOJA KWA MOJA KWENYE MATUMIZI YA NENO ...MTU WA MUNGU....!

UKIANZA MWANZO WA KITABU CHA WAFALME WA PILI MPAKA PALE MFALME ANAONGEZEWA UMRI WA KUISHI INAELEZA KWA KINA KUHUSU SWALI LAKO....HAPO NDIPO UTAKAPOONA KUWA KUNA WATU WA MUNGU......!

Angalia sehemu ya mwisho ya yale niliyoyaandika. Nimegusia khs matatizo ya tafsiri.

Hilo "Gombo la Chuo" nalo pia ni tafsiri ya "Gombo" lingine, ambalo nalo linahitaji lingine na lingine kwa ajili ya rejea. Je, ndugu mahesabu, unalo hilo "Gombo" rejea la "magombo" yote ili tuangalie ukweli kuwa "watu wa Mungu" ni hao hao walioelezwa ktk "Gombo" ulilonalo, na hivyo huyu mama ni miongoni mwa hao?
 
Kinachonishangaza ni jinsi hawa "manabii" wa kujipachika wanavyopata wafuasi. Tena wafuasi wengine wana elimu kubwa tu! Tanzania kuna "self styled" ama "self appointed" prophets wengi sana sasa hivi, na haweshi vituko. "Mtume na Nabii" Josephat Mwingira na vituko vyake pale mwenge (na kesi mahakamani inayohusu eneo analofanyia shughuli), na pia ana kampuni au agents wa ulinzi, nabii huyu au biashara!

Soma http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/06/04/91872.html.

Yuko mwingine Vernon Fernandes hukohuko Dar, naye ni "mtume na nabii", naye kategesha nyavu zake hukohuko barabara aliko Mwingira, naye kipaumbele chake katika mahubiri yake siku zote ni "kutoa", namba ya akaunti ya kanisa lake inakuwa kwenye screen ya tv muda wote, yakikukolea tu ukatumbukize mahela humo! Hata siku moja sijawasikia wakisema hiyo akaunti ina hela ngapi sasa tangu watu waanze kutumbukiza "mafungu" humo ya "kupanda mbegu".

Njia hiyohiyo kuna Sylvester Gamanywa, angalao yeye hajajiita nabii na wala sijasikia kituko chochote dhidi yake, lakini nina mashaka. Kwa nini wanapenda tu huko Mbezi Beach? Wajanja hawa, wanajua kuna "ming'ombe minene" huko, zinatoka sadaka za maana! Sasa je, ulitaka waende Mkuranga au Rufiji wakafe njaa? Maskini wa Mbagala anagombania gari hadi anatolewa ngeu ili aende Mbezi Beach kupewa maneno ya matumaini kutoka kwa "nabii". Na "nabii" huyu si kama wale tuliosikia habari zao zamani, ambao walifunga wakisali, walivaa nguo duni, waliishi na masikini, walipeleka mafundisho ya ukombozi kwa masikini huku wakikemea wafalme na mafisadi bila woga. Hao ndio manabii niliofundishwa habari zao katika Biblia. Lakini hawa wa siku hizi wanabariki mafisadi! Wanakamua maskini!

Nikiambiwa leo nitoe mfano wa nabii katika karne iliyopita japo hakuwahi kujiita hivyo, nitamtaja bila kusita Rev Martin Luther King Jr. Ukisoma habari zake, na wale waliobahatika kuishi na kumsikiliza enzi zake, utaamini huyu kweli alikuwa wa pekee, lakini hakujiita nabii!

Mwisho, changamoto, hasa kwa walioko vyuoni wanaosoma sociology au anthropology. Hili ni eneo zuri sana la utafiti. Nini kinachomsukuma mtu kumfuata "nabii"? Hivi mwajua hata yule mwanamke "nabii" Alice Lakwena wa Uganda aliyeanzisha jeshi la kumtoa Museveni akidai alikuwa anaongozwa na "roho mtakatifu", alikuwa na wafuasi wasomi sana? Mmoja wapo alikuwa Prof Isaac Newton Ojok, ambaye aliwahi kufundisha Makerere University na pia aliwahi kuwa Waziri wa Elimu katika serikali zilizotangulia Uganda. Na alijiunga na Alice Lakwena kwa vigezo vya kiimani zaidi kuliko siasa au uchumi, maana kwa elimu na nafasi yake angeweza kujiunga na makundi makini zaidi kama shida ilikuwa tu kutofautiana na Museveni. Humo kwenye dini ya Lakwena akawa na title ya "Apostle" Prof! Na aliandika vitabu vya imani hiyo, kimojawapo ni "The Bloody Road to Life" bofya hapa: [ame]http://www.amazon.com/Bloody-Road-Life-Isaac-Newton/dp/1903970180/ref=sr_1_2?ie=UTF8&s=books&qid=1206925972&sr=1-2[/ame].

Ajabu nyingine, miongoni mwa wafuasi wa Kibwetere wa hukohuko Uganda, alikuwako Padre mwenye elimu ya Masters katika Theology! Watu hawa wanafuata nini kwa "vibwetere"?

Ni eneo zuri la kuchukulia PhD wanawane!
 
Mimi sioni ubaya wa Mama huyu ktk shughuli zake ambazo ni za kidunia (kutafuta posho) na za kiimani (mambo ya Mungu). Hi ni kwasababu ya "Kaisari anampa Kaisari" na ya "Mungu anampa Mungu". Haya ni maneno ya Yesu Kristo mwenyewe, "Ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu" In fact ana-balance vizuri ndio maana anafanikiwa kotekote. Anatimua mapepo na anapata ubunge. Big up Mama Rwakatare!
 
Ni eneo zuri la kuchukulia PhD wanawane!

Kithuku,

Kwanza thanks kwa kunipa idea ya kufanyia research hii issue coz am going to consider that. Lakini pia lazima tuelewe hizi ni nyakati za mwisho kwa wale wanaosoma biblia na kuilewa. Kuna mvutano mkubwa sana. Shetani anatafuta watu wengi zaidi wa kwenda nao lakini pia Mungu wetu anataka pia kuokoa watu wake.

Ndo maana hakuna wakati katika historia ya neno la Mungu ambapo matendo makuu, ishara na miujiza itajidhihirisha kama sasa kwa sababu Mungu anataka ajithibitishe kwa watu wake hata kwa wale wagumu wa kuamini ili wamtambue na kuokoka hata through miujiza kwanza kabla ya kuamini. Kwa hiyo ndo maana utaona mitume wengi, manabii wengi, wachungaji wengi, waimba gospel wengi etc. Hii haimaanishi wanatafuta pesa, kumbuka Neno la Mungu linasema wote lazima walijue kabla ya ule mwisho ili asiwepo mmoja wa kusema mimi sikuwahi kumsikia huyu Yesu.Ili hiyo itimie lazima watenda kazi waongezeke.

Mbona hamuulizi kila baada ya nyumba kumi kuna bar ila makanisa na wachungaji mnaquestion? Mbona hamuulizi kwa nini watenda maovu wanaongezeka ila mnauliza kwa nini mitume na manabii wanaongezeka? La muhimu ni kwamba wanamhubiri Yesu aliye hai, wewe chukua uujumbe unaofaa, na ayantendayo yeye mwachie ni yake. La mwisho who are we to judge?
 
Y Kaizari na apewe kaizari na ya Mungu apewe Mungu ,Lakini inakuwa vipi mchungaji anapokuwa tayari kuacha kuundi la kondoo wake na kufuata siasa ,Mbaya ?
 
Ya Kaizari apewe Kaizari na Ya MUNGU apewe MUNGU ! Inakuwaje Pale Mchunga Kondoo anapotaka kuwaacha Kondoo kufuata siasa ? MBAYA ?
 
hivi kweli unaushahidi wowote kuwa mama Rwakatare amedanganywa na wale watoto au unaropoka tu?
Jamaniee mi nachoka kabisa bora kuacha haya mambo maana hata serikali haiamini uchawi ingawa viongozi wanapishana huku kwa waganga.Naikumbukwe jamani kuna wabibi wanawatumia wajukuu zao kwa uchawi na wazazi wao hawajui kabisa ombeni agape wana kipindi cha ushuhuda kinaitwa this is my story mtaona mambo kule.na mwenye ushahidi hawa watoto ni matapeli aweke wazi
 
Mwenzake huyu hapa anaitwa Benny Hinn:

[media]http://www.youtube.com/watch?v=FUyPjeIFKug&feature=related[/media]
 
HAYA SASA WADAU NAONA MMEFIKISHWA,SASA KUDANGANYWA MTU NI KAWAIDA AU MAMA RWAKATARE ALIWAAMBIA YEYE NI MARAIKA???
SASA BASI KWATAARIFA YENU MUNGU NDIE ALIYE FANYA HAO WATOTO WAUMBUKE,

YAANI NAONA MMECHANGAMKIA,MAMA WAWATU ANABARIKIWA TU YESU ANA MBARIKI KAMPA UBUNGE WATANZANIA WOTE MNAMUESHIMU MNA MWITA MUHESHIMIWA.

KUDANGANYA LAZIMA UTAUMBUKA TU! MPAKA HAPO UJUE MAMBO YA KIROHO UKIDANGANYA UNAUMBUKA KAMA HAO MADOGO.
 
Inaonekana kila mtu anaongelea mapungufu ya Mheshimiwa Getrude Lwakatare! Bado sijaona kitu gani huyu mama amewakosea watanzania au kinachofanya kila mmoja wetu kuona anazo sababu za msingi kumnyooshea kidole kama ni mkosaji. Wakati mwingine ni busara kujihoji wenyewe maisha yetu kabla hatujamkosoa mtu mwingine. Ni jambo la kawaida kuona kila mtu mwenye dini kuamini kuwa dini yake ni bora kuliko nyingine au kile anachoamini ni sahihi kuliko vingine vyote. Kuna rafiki yangu haamini kabisa kama kuna kitu kinaitwa Mungu na katika maongezi ukitaja Mungu lazima akusimamishe na kukuambia wazi hapendi huo uongo kuhusu uwepo wa Mungu; kwa mtazamo wake sisi wenye dini na kuamini uwepo wa Mungu tumepotea.

Suala la imani ya dini ni la mtu binafsi, uchaguzi wa kuwa kwenye dini na kwenye siasa ni wa mtu binfsi pia na katiba ya nchi yetu haina tatizo na hilo ndio maana hajawahi kufunguliwa mashataka kwa kuwa mtu wa dini na mwanasiasa wakati huohuo. Isitoshe asilimia kubwa ya wanasiasa wana Imani fulani za dini, kama sio waislamu, basi ni Wakristo, Hindu, nakadhalika. Kwa nini tunamkomalia mama wa watu peke yake?

Kwa mtazamo wangu Mheshimiwa Lwakatatare kwa nafasi yake kama Muhubiri wa dini na Muombeaji hajawahi kujitangaza kama anatenda miujiza; nijuavyo mimi yeye huwa anahubiri juu ya Mungu na kuwa anamuomba Mungu ili awatendee miujiza wenye shida. Maswali kwa nini muujiza haukutokea au , in this case, kwa nini hawa watoto wamepeleka uongo kanisani bila kugundulika anatakiwa aulizwe Mungu. Wengi wetu tuna experience ya kudanganywa, kuumwa, kufiwa, kupata hasara kwenye biashara na vitu vingine tusivyovipenda. Still bado tunamuomba na kumuamini Mungu.

Argument kuwa huamini kuhusu muujiza inawezekana iwapo hujawahi kupata Muujiza. Kwa sisi tuliowahi kutendewa miujiza ni ngumu sana kuamini hizo arguments. Lakini all in all nafikiri Mungu halazimiki kumtendea Muujiza kila mtu au kumfanya kila mtu awe na hali sawa na mwingine.

Badala ya kuangalia upande mmoja ni vizuri kuangalia na mchango wake pia katika Taifa.Kama mwanasiasa na mbunge Mheshimiwa Lwakatare anayo nafasi kulitumikia Taifa; tumuombee atimize huo wajibu kwa ukamilifu. Katika kazi zake kama Muhubiri na mtumishi wa Mungu bado naona anatoa mchango mkubwa kwa jamii sababu mafundisho na mahubiri yanayotolewa makanisani na misikitini yanalenga kutujengea raia bora wenye maadili mema. Katika biashara zake kama mmiliki wa Shule za St Mary's na kituo cha watoto yatima Tabata Bima pia anatoa mchango mkubwa kwa Taifa. Wenye kumudu zile ada wanakwenda kusoma kwenye shule zake badala ya kupeleka watoto nchi nyingine mbali na wazazi wao. Wakati tunamnyooshea vidole huyu mama ni muhimu kujihoji sisi tumechangia nini katika hili Taifa.

Kama kuna kosa alilolikosea Taifa au kuvunja sheria ya nchi ni vizuri kulizungumzia hilo badala ya kuongelea ishu za kizushi na chuki binafsi. Au kama amemtukana na kumkashifu mtu katika mahubiri yake tujadili hilo. What is wrong mtu akitangaza kuwa anaamini Mungu anaponya, kinachotakiwa si kama unaamini uungane nae na kama huamini unashika hamsini zao?!!! Tuache "wivu wa kijinga", pesa na biashara ni zake mwenyewe, Imani ya dini na style ya kumtumikia Mungu ni yake mwenyewe. Upenzi wake katika Siasa ni uhuru wake wa kikatiba. Kuna shida gani kuhubiri dini katika TV kwa kulipia TShs 500,000 za kwake mwenyewe?!!
 
Yuko mwingine Vernon Fernandes hukohuko Dar, naye ni "mtume na nabii", naye kategesha nyavu zake hukohuko barabara aliko Mwingira, naye kipaumbele chake katika mahubiri yake siku zote ni "kutoa", namba ya akaunti ya kanisa lake inakuwa kwenye screen ya tv muda wote, yakikukolea tu ukatumbukize mahela humo! Hata siku moja sijawasikia wakisema hiyo akaunti ina hela ngapi sasa tangu watu waanze kutumbukiza "mafungu" humo ya "kupanda mbegu". Njia hiyohiyo kuna Sylvester Gamanywa, angalao yeye hajajiita nabii na wala sijasikia kituko chochote dhidi yake, lakini nina mashaka. Kwa nini wanapenda tu huko Mbezi Beach? Wajanja hawa, wanajua kuna "ming'ombe minene" huko, zinatoka sadaka za maana! Sasa je, ulitaka waende Mkuranga au Rufiji wakafe njaa?

Wasalaam Kithuku!!

Nimecheka sana na observation yako ya kutegesha nyavu kwenye samaki wakubwa!!

Lakini nafikiri hii haina shida sababu hata wakazi wa Mbezi beach wanahaki ya kupata mahubiri na huduma za kiroho. Kama ujuavyo huko ndio kuna watu wenye nguvu kubwa kiuchumi, na logically hayo makutano na makanisa ya huko yana nguvu kubwa kiuchumi na hivyo kumudu kutoa matangazo redioni, kwenye TV, magazeti nakadhalika. Usisahu hata huku kwetu mtoni kwa aziz ally tunayo makanisa, kule vingunguti, buguruni, mbagala, kigilagila kote huko kuna makanisa. Hao jamaa wamekuwa maarufu kutokana na maeneo wanayofanyia kazi kuwa ni maarufu pia. Hawa wa huku mtoni na kigilagila huwajui sababu hawaruki kwenye TV.

Suala la kutoa sadaka kwa hiari lipo kwenye dini zote. Hata babu zetu wanatoa sadaka kwenye matambiko. Kithuku acha hizo kwani wewe hutoagi sadaka? Au umeshtuka sababu akaunti ipo kwenye TV? Sasa kama muhubiri anahubiri kwenye TV sadaka itatolewa wapi.? Hiyo ndio electronic Gospel mkubwa!
 
navyoamini mimi, wachungaji ni watu maalum katika jamii ambao wamejaliwa kuwa viongozi wetu wa kiimani....nimesoma kwa mshtuko from some newspapers that mchungaji mama Getrude Rwakatare (MB), amedanganywa na vijana, tena wadogo mno kiumri (7-10 yrs), waliojifanya ni wachawi waliodondoka toka safari zao...eti cha kushangaza zaidi, ilibidi ipigwe ibada ya nguvu kuwaombea!! utata naopata mimi, na ninaomba wadau wenzangu mnisaidie ni kwamba, je mama Rwakatare alishindwa kutumia nguvu za kiroho alizonazo kutambua kwamba those guys were conmen???? uko wapi mpako wa roho mtakatifu kwa mchungaji wetu? haya, kazi kwenu, tudanganyeni tu!!!??
Naomba hii mada niilete tena kwani kuna ushahidi zaidi umepatikana.

Yule mtoto aliyeanguka kutoka kwenye paa la kanisa sasa amekutwa na kichwa cha mtoto wa kama miaka mitatu.

Je, wadau mnasemaje juu ya uwezo na nguvu za huyu mchungaji Rwakatare? Na je, mtachukua muda kuomba radhi kwa yale mliyoyasema ya usanii na nini ili msije mkakutwa na yale yaliyowakuta waliomsema mabaya mtumishi wa Mungu Musa?

Hakuna sanaa ndani ya jina la Yesu bali kuna nguvu na uweza.

Usifiwe msalaba lisifiwe kaburi. Asifiwe Yesu Kristo kwa kutupa nguvu hii.

Kama watu wasingepuuza nguvu za Mungu katika Kristo Yesu mtoto huyo wa Tabata asingepoteza maisha. Ila kwa ajili ya mioyo ya watu kuwa mbali na Mungu na kutaka kutengeneza vichwa vya habari kwenye magazeti na JF ndo hayo yametokea.
 
Naomba hii mada niilete tena kwani kuna ushahidi zaidi umepatikana.

Yule mtoto aliyeanguka kutoka kwenye paa la kanisa sasa amekutwa na kichwa cha mtoto wa kama miaka mitatu.

Je, wadau mnasemaje juu ya uwezo na nguvu za huyu mchungaji Rwakatare? Na je, mtachukua muda kuomba radhi kwa yale mliyoyasema ya usanii na nini ili msije mkakutwa na yale yaliyowakuta waliomsema mabaya mtumishi wa Mungu Musa?

Hakuna sanaa ndani ya jina la Yesu bali kuna nguvu na uweza.

Usifiwe msalaba lisifiwe kaburi. Asifiwe Yesu Kristo kwa kutupa nguvu hii.

Kama watu wasingepuuza nguvu za Mungu katika Kristo Yesu mtoto huyo wa Tabata asingepoteza maisha. Ila kwa ajili ya mioyo ya watu kuwa mbali na Mungu na kutaka kutengeneza vichwa vya habari kwenye magazeti na JF ndo hayo yametokea.

Ngonalugali,

Heshima yako natanguliza mbele.

Kisha najaribu kukuelewa kuhusu hayo ulosema...Huyo
mtoto aliyekatwa kichwa kwani alimsema vibaya Mama Rwakatare?
Kisha naona unasifia nguvu za msalaba na kaburi...najua these
are some main tenets of the christian religion and the
Christians know it better.Kama wasemavyo there is power in those
two but what people are debating over here is the fact that
Mama Rwakatare anatumia dini kuendeleza mambo yake binafsi na
sio mambo ya Mungu.
 
Ngonalugali,

Heshima yako natanguliza mbele.

Kisha najaribu kukuelewa kuhusu hayo ulosema...Huyo
mtoto aliyekatwa kichwa kwani alimsema vibaya Mama Rwakatare?
Kisha naona unasifia nguvu za msalaba na kaburi...najua these
are some main tenets of the christian religion and the
Christians know it better.Kama wasemavyo there is power in those
two but what people are debating over here is the fact that
Mama Rwakatare anatumia dini kuendeleza mambo yake binafsi na
sio mambo ya Mungu.
Sijasema kuwa mtoto huyo alimsema vibaya mama Rwakatare isipokuwa ni yule kijana kudondoka kwenye paa la kanisa la mama Rwakatare na watu kusema ni usanii wa wachungaji wa kupandikiza watu kusemea nguvu za Mungu na huku ni maneno ya kupanga.

Kuna watu wawili hapo. Mtoto aliyekatwa kichwa na huyo mtoto aliyemkata kichwa ama aliyekamatwa na kichwa cha huyo mtoto wa kike kikiwa fresh. Ninayemzungumzia mimi ni huyo mtoto wa kiume.

Na zaidi na-support huduma za zinazotolewa na mama huyo, kwani kumtumikia Mungu si kuwa maskini na zaidi ya hayo ni kuwa wa kwanza katika kila kitu.

Mungu hakuwafanya watu wake kuw mikia bali wawe vichwa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom