Mama Rada Bi Clare Short kupewa tuzo

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,892
31,098
Waziri wa zamani wa Uingereza wa ushirikiano wa maendeleo Bi Clare Short aka mama rada anatarajiwa kupewa tuzo mahsusi na kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu Tanzania [LHRC] kwa msimamo wake wa kupinga ununuzi wa rada.

Bi Clare Short alianzisha mzozo wa kupinga ununuzi wa rada katika bunge la Uingereza,nchi ambayo ni mfadhili mkubwa wa maendeleo ya Tanzania,na hasa bajeti ya taifa ambayo zaidi ya 30% hutegemea wafadhili.Hoja zilizokuwa zikitumiwa na Bi Clare katika kupinga ununuzi wa rada ni pamoja na rada hiyo kuuzwa kwa bei ghali tofauti na thamani halisi lakini pia ubora wake ulikuwa wakutiliwa shaka.

Source:Raiamwema
 
Ni kwani nini asipewe Andrew Chenge? Maana yeye ndiye MSHINDI katika sakata zima to the extent kwamba serikali ya Uingereza imeamua kurejesha "kick-back"!
 
Ni kwani nini asipewe Andrew Chenge? Maana yeye ndiye MSHINDI katika sakata zima to the extent kwamba serikali ya Uingereza imeamua kurejesha "kick-back"!

Heshima kwako Baba_Enock,

Chenge anastahili kupelekwa segerea lakini muungwana anajua akimgusa lazima Chemkapa na system nzima itawajibika.

Kwa kuanzia LHRC wamefanya jambo zuri sana kukumbuka mchanga wa mama rada raia wa Uingereza aliyekuwa na uchungu na fedha za Tanzania kuliko chenge mtanzania aliekuwa anawaza vijisenti
.
 
Ni wazo zuri kumtuza mama huyu. Ni watu wachache wenye moyo kama wake!
 
Na Tony blair na Mkapa Je? Wapewe zawadi ya sampuli ipi....?

damn them!!!!!
 
Mama Rada alijitahidi kututetea sana, kiburi cha Mkapa na misemo yake ya wavivu wa kufikiri viliishia kuitia nchi hasara ambayo mpaka leo bado tunailipia.

Natamani siku ifike tumpandishe Mkapa Kizimbani kwa kuitia nchi hasara
 
Che Nkapa amekwenda Iringa vijijini wiki moja iliyopita akaringa kwamba hajazomewa. Kumbe anapenda kuzomewa. Sasa mama Rada (Clare Short) anakuja ili tumpe tuzo kwa kuwajali na kuwasemea walalahoi wa Tanganyika walio fisadiwa fedha zao kwa kiburi cha Che Nkapa cha kusema watanganyika ni wavivu wa kufikiri kwa kutofagilia rushwa ya ununuzi wa rada.
 
Back
Top Bottom