Mama ni dhahabu ukimkosa utapata shida; ahimidiwe mfariji wetu Mungu wa mbinguni

Huu uzi umenikumbusha usiku wa tarehe 7.11.2006 ,nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza udsm.
Nilirudi nyumbani kwa maoumziko ya weekend mnamo tar 4 ambapo nilimkuta mam Yangu mpendwa amepika chapati na njegere alinisihi nile ila by thn sikuwa na hamu ya kula kbs ila ilinibidi nile kidogo kumridhisha nae alifurahi sana,masikini bila kujua kumbe ule ndio ulikuwa mwisho wa mm kuona tabasamu lake zuri.

Usiku wa kuamkia tar 6 dada yangu ambaye naye alikuwa mwanafunzi udsm alinipigia simu kuwa mama anaumwa sana wanampeleka tmj hosp basi nilishtuka sana na sikuweza kulala tena ,alfajir nilielekea tmj hosp ambapo nilimkuta mama ypo kwenye hali mbaya wamemuwekea oxygen basi niliumia sana nilishinda hapo hosp,basi mida ya jioni mama alipata nafuu akaweza kuongea akaniambia mm nirudi chuo nisome ila kesho yake asbh niwahi ili nikae nae dada yangu nae aende chuo
Haikuwa siku nzuri kwangu hata baada ua kuondoka pale hosp maana kila kitu hakikushikika.sikujisikia kusoma,sikujisikia kula yani mambo yalikuwa vululu vululu.

Usiku mida ya saa 7 simu yangu iliita ,kuangalia mpigaji alikiwa ni dada yangu ambaye nilimuacha na mama hosp,hata sikuwa na mashaka maana mama nilimuacha amepata nafuu kidogo ,lkn sikuamini masikio yangu baada ya kupokea simu ile,aliniambia Mdogo angu mama amefariki .
Nililia kilio kilicho amsha watu wengi kutoka kwenye flats mbalimbali pale kijitonyama hostel

Baada ya siku mbili tulimpumzisha mama kwenye nyumba yake ya milele.
Basi huo ndio ukawa mwanzo wa mahangaiko yangu hadi leo ,mabinadamu manafiki ndio wanaonizunguka.

Tuonane asubuhi ile mama yangu kipenzi.
Bado nakupenda vile vile ingawa hauko nami.
 
Mama yangu ilikuwa ndio nguzo yangu nilioitegemea kwani ndio nilikuwa nikiishi nae. Mimi niliona kawaida sana kwani aliniacha mdogo nikiwa na miaka Mitano tu. Mimi ndio nilikuwa nawaambia watu habari za Msiba watu walikuwa wakinishangaa sana lakini walijua ni akili ya utoto tu. Ilikuwa ni mwaka 1993 kadri siku zilivyoenda na manyanyaso ya ndugu ndio nikaanza kuona pengo la mama ni kubwa na halizibiki. R. I. P Mama ila umenipa funzo mpaka leo sijapata mtoto yaani naogopa kuzaa kabla ya ndoa Mwanangu asije akapitia niliko pitia mimi.
 
Tabia ya kukumbuka mambo yaliyopita ni udhaifu kwa mtazamo wangu.
Ungejua unaloliongea....! There some memory that can not be forgotten in life no matter how hard we try..!
Wote uliowackia waki share their memories with us, is such an experience that gives them right and position....!Don't ask for that,bad memory and experience.no one ever ask for them.
 
Mama yangu alifariki 2011..siku hiyo nilikuwa shule(boarding ipo mkoa wa pwani) nikajisikia hali fulani hivi kitu kinaniambia nirudi nyumbani na hamu ya kukaa shule ikaniisha kabisa so ikabidi nikaombe ruhusa(nilijisingizia ugonjwa),wakaniruhusu.

Nikaenda kituoni nikapanda basi kurudi nyumbani dar es salaam.basi nikafika home mida ya saa 9 hivi nikakuta milango ipo wazi,sebule haieleweki yani chakula kimeachwa mezani na hakuna watu.Basi nikakaa kidogo then nikatoka nje majirani wakawa wananiangalia kwa mshangao hivi mimi nikajua ni hali ya kawaida tu.

Baadae uncle mdogo akaja huku macho yakiwa mekundu akashangaa kuniona nipo nyumban alaf niko sawa tu akajikaza then akaniuliza mbona umerudi ghafla? Nikamwambia basi tu niameamua kuondoka shule;
Akaniuliza taarifa nani amekupa(na sikuwa na simu)!?
Nikaamuuliza taarifa gani!? Akasema kwani hujui!? No I am u up I as kuna nini kwani!?
Hakunijibu, alichukua simu akapiga nyumbani kwenye msiba(ni mkoani sio dar) alaf akanipa niongee nao.

Bibi yangu mzaa mama ndo alipokea aliposikia sauti yangu namsalimia akaanza kulia akashindwa hata kuongea,basi ikabidi kaka ake mama achukue simu ya bibi iliaongee na mimi(hapo ndo nikaanza kuhisi kuna kitu kibaya). Uncle alipochukua simu akaniambia "..hey huku hali ya mama yako si nzuri jikaze ww ni mtoto wa kiume(alikuwa ameshafariki ila uncle hakutaka kuniambia).." alaf nikasikia watu wanalia zaidi kwa mbali alaf akakata simu.

Yan hapo nilihisi kama nachanganyikiwa hivi pia sikuamini kabisa nikaanza kucheka nikihisi ni utani tu kumbe ndo ilikuwa imeshatokea
Basi huyu uncle mdogo niliyekuwa naye hapa ndo akaanza kunihadithia jinsi ilivyokuwa mpk mama akafariki na walipopata taarifa walikiwa wanakula wote wakachanginyikiwa wakatawanyika kwenda kukata ticket na kuomba ruhusa kazini bila hata kufunga mlango yan ndo maana nilikuta vitu havieleweki mule ndani.

Nilipata wakati mgumu sana lkn nikawa najifariji kwamba my mom can't die wkt sijamnunulia hata kitenge..nikawa najiaminisha kwamba nikifika huko nyumbani kwenye msiba(mkoani) nitamkuta kama nilivyomuacha..haikuwa hivyo wakuu..nilifika home nikakuta watu wengi wapo kwny majonzi mazito yan dah..sikuamini nilipomwona kwny jeneza na picha yake imewekwa pale juu wkt nilimuacha akiwa mzima na alinipa mkono wa heri na kunisisitizia nisome sana dah..mama nakupenda sana popote ulipo...nakupenda sana mama yangu dah..sikuwahi amini kabisa jmn km kuna siku kama ile ingekuja kunitokea..nakupenda mama. Poleni watu wote mliopoteza watu wenu wa karibu..ni uchungu mkubwa mno..inauma sana..
Pole Sana Mkuu
 
Pole sana kwa msiba wa mama,mimi mama alifariki january mwaka 2013 bugando mwanza baada ya kuumuguza miezi 3,alipata stroke ya upande mzima wa kulia,baba naye alifariki mwaka huo huo 2013 mwezi wa nane,Baba na Mama pumzikeni kwa amani huko mliko
OFF TOPIC mwaka 2016 ulikua form 2,kwa hiyo sasa uko form 3,napendekeza uongozi uone namna kutugroup kwa umri,maana ukiona kuna mtu wa umri wa watoto wetu tuchague maneno ya kuzungumza,maana tunatupia tu maneno ya kiutu uzima kumbe kuna watoto wetu wanatuangalia,kimaadili haijakaa vizuri
Pole Sana Mkuu,

Hapo kwenye 2016 ilikua ni 2006 nilikosea kutype, na nmeshindwa Ku edit .mpaka sasa ni miaka 11 imepita na sasa nipo natengeneza familia yangu
 
Nilipewa taarifa wakat naangalia mechi ya UEFA champion league kwenye bar mzee ananipigia simu kuwa mama angu amefariki usiku wa tareh 18 April 2017. .hakika niliangua kilio mule ndani kiasi kwamba ikabidi TV izimwe kwanza. .aisee we acha tu. .. nakupenda mama angu may your soul rest in eternal life amen
Pole sana mkuu
 
binafsi nilipewa taarifa ya kifo chake wakati nipo shuleni,ilikua asubui ya jumatatu wakati najiandaa kwenda darasani ili kumalizia maandalizi ya mitihnai ya kidato cha pili maana ilikua inaanza wiki inayofuata,

siku hiyo alikuja mwalimu akaniambia niende nyumbani nahitajika ,nikapanda gari huku nawaza sana,imekuaje leo naitwa nyumbani wakati sio kawaida na wanajua kabisa tuna mitihani wiki ijayo.nikawa sina namna ikabidi nipande gari kuelekea nyumbani japo ndani ya gari sikuwa na raha hata kidogo wakati siku za kawaida ukiambiwa urudi home ni shangwe kubwa sana.

ndani ya gari nikawa nawaza tu japo tokea usiku wa kuamkia jumatatu sikuwa na raha kabisa .basi niliposhuka kwenye gari tu nikakutana na bro wa mtaani kwetu,nikamwita bro vipi ,aliponiona akashtuka sana ila akaja na kunisalimia huku akiwa na mashaka ,nikashangaa akanipokea begi na akawa mkarimu sana kwangu ,nikamuuliza vip kwema huku akaniambia kwema,basi tukaongozana na yule bro hadi mitaa karibu na nyumbani ,kadri tulivyokua tunakaribia nikawa najihisi mabadiriko mwilini pia hali ya hewa nikawa siielewi kabisa.

ile kumaliza kona za mtaa tu na kuanza kupaona nyumbani ,nikaona watu wengi sana home na ndugu wengi wengi ,ile nasogea tu nikamuona mama mdogo ambae ni pacha ake mama na ndie nmekuwa nikiishi nae muda wote tangu nikiwa mdogo maana mama yangu alikua ni nurse jeshini hivyo hakuwahi kuishi sehemu moja,akaja akanikumbatia huku akilia sana ,akaniambia mama mkubwa wako amekubali yaishe tu(mama yangu nilizoea kumuita mama mkubwa).kamua kutuacha tujitawale sasa .baada ya kutoa kauli hiyo alilia sana akaniachia akataka kuanguka wakaja watu kumshika

Muda wote huo binafsi sikujua hata cha kufanya ,nilipigwa na butwaa na yule bro akanishika akanipeleka hadi ndani ilipokua maiti ,nilifika nikapiga magoti nikamkumbati huku nampapasa tu nisijue cha kufanya,wakaja wakanitoa nje na nisijue cha kufanya ,nilikaa muda mrefu sana allmost dakika 20 hivi ndipo nilipoanza kulia.

Aisee maumivu niliyoyapata siku ile hayavumiliki hata kidogo,yani mpaka sasa nikisikia mtu kafiwa na mama yake ,naogopa hata kwenda kumsalimia maana sipati picha kiasi cha maumivu aliyonayo maana kwa muda huo kwake huwa hakuna kitu cha thamani tena maishani.......
R.I.P MOM
Mkuu pole sana Mwenyezi Mungu ampumzishe mama kwa amani nimesisimuka sana
 
Yaani upo kidato cha 3 na unashida humu?
Twende kwenye mada pole kwa kufiwa na mama.
Mama yangu Leo yupo mahututi ana kansa ya kizazi.
Mungu ni Mkuu Sana, hakuna neno lolote lililo gumu kwake, naamini Mama atapona
 
Mliobahatika kuwaona mama zenu hongereni, mimi nimenyonya maziwa ya bibi na nimegundua kuwa sio mama mwaka 1958 mwezi wa pili nilipopewa story na mzee mmoja hivi baada ya bibi kufariki
Na uzee huu natamani ningemuona mama mzazi
Aisee pole Sana mzee wangu ,inaumiza sana
 
Ukweli kila ninapomkumbuka marehemu mama yangu machozi hunitoka ...nayakumbuka maneno yake, "mwanangu walimwengu sio wema usiwaone kucheka..."
 
Nilimpoteza mama yng nikiwa namiaka 10 tuu, yeye akiwa na umri wa miaka 30 tuu, she was too young to die, nilimpenda sn zaid hata nijipendavyo mm, kwa udogo ule nilijiuliza maswali bila kujua kwamba nakufuru Mungu, niliuliza hivi Mungu kwann umemchukua mama yng, kwann umekubali niish bila mama ktk umri huu, hata km kunajambo amekukosea cdhan km kweli alistahili adhabu hii,


Safar y maziko ilituchukua siku mbili huko Mahenge morogoro, hata baada y maziko nilikuwa natoroka asubuh naenda kabulin kwa mama yng nikiamn nitaisikia japo saut yake , nliish nikiamn kuwa mama hajafa ila amelala tuu cz ain't a woman alive dt could take my mam's place.
my dad aliply part kubwa sn km mama na baba kwetu, cz hakutafuta mke mwingine km mlez we2, aliamin ange handle situation ile n tunashukuru kwa hilo cz alijitahid sn kuwa karibu n ss,


Mwenyez Mungu mwing wa rekhma akampumzisha my dady pia , ni miaka 4 tu baada ya kifo cha mama yangu, yan nilipoteza wazaz wng wote nkiwa n miaka 14 tu, ila nashkuru kwa zawad y maisha, sweet memorials we shared, and all my childhood memories are full of all sweet things they did for me.
R.I.P Dady & Mom...
 
Mama yangu alifariki 28 Nov 2016 saa 10.45 jioni mbele yangu na mdogo wangu wa mwisho pamoja na mama mdogo yaani mdogo wake , vile vile alikuwepo mke wangu . asubuhi ya siku hiyo aliomba kuongozwa sala ya toba . alikuwa ameugua kwa muda wa miaka saba hivi akisumbuliwa na kansa ya ubongo. ilikuwa ni siku ya majonzi na huzuni kubwa
 
asante mkuu nishapoa ,ila Mungu ni mkubwa sana aliniachia mama mwingine ambaye kiukweli amejitahidi kunionyesha upendo wa dhati na rafiki zangu tuliokutana ukubwani wengi wanajua yule ndiye mama yangu.MUNGU NI MKUBWA SAN
mwenyez mungu azidi kutupa moyo wa ujasiri
LIFE GOES ON
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom