Mama Ndalichako, kichwa cha nyoka hiki hapa piga!!

nikusalimu mama, kwanza kabla ya yote mama niseme mimi nakukubali sana utendaji wako tangu ukiwa necta na hata kuchaguliwa kwako nilifurahi sana maana nakukujua na binafsi nimeshafanya kazi Mara mbili na wewe hivyo nakujua kidogo..

kadri siku zinavyosogea umaarufu wako unazidi kuporomoka kutokana na matamko yako na si utendaji wako!! wadadavuzi Wa mambo wanadai kinachokuponza ni kutamka tu...kila unapopita!! nimejaribu kufuatilia matamko yako nikaona una nia njema ya kuua nyoka lakini unapiga kwenye mkia bila kutafuta kichwa!!
nakuhakikishia ukipiga kichwani ni fimbo moja tu nzito kuliko kupiga fimbo mia mkiani...

mama ubora Wa Elimu nchi hii ni WALIMU !! hiki ndio kichwa cha nyoka! Mara majoho, sijui nini, ohh sijui hivi!! huko kote mama unapiga mkiani!!

kaa vizuri na walimu wako changamoto zao unazijua vyema!! poteza muda wako mwingi kukaa nao na kuwaambia kipi unataka wakifanye katika Elimu Yetu, tatua kero zao, boresha maslahi yao...rudisha ile morali yao ya kazi hiki ndicho kichwa mamaangu!!

najua siasa inaanza kukutawala kidogo na wapo watakaokunong'oneza kuwa nyoka ukimkata mkia atakufa pole pole!! achana nao .
Kama anapokea Ushauri,, hujampoteza apite humohumo,, hii nchiiii yetu wote,,
 
Na hzo kauli mbona hazna misimamo. Walianza name GPA juu wao wenyewe wakashusha tena.juzi tena ya diploma kutokwenda university jana tena wamekanusha eti ni uzushi mtandaoni ivi kweli sisi ndo wazushi au wao.
 
Unadhani mambo ni rahisi kiasi hicho mkuu ..!!??
kwanini isiwe rahisi kama watu unawatengenezea mazingira bora ya kufanya biashara zao,anyway kunavitu kama bahati nasibu yataifa nikati ya mahala pengine unaweza kuchangisha na kuzalisha pesa nyingi kwa serikali
 
hiki kidindi elimu yetu inapitia pagumu sana.Hawaangalii unafanya nini wanaangalia umepata alama ngapi kwenye cheti chao.Hata uwe na uwezo wa kuwafanyia kazi zao hawatambui hilo.Wanataka kuona una alama ngapi kwenye cheti!
 
Nilipita katika center moja kubwa ya open university. Si unajua 80% ya wanafunzi wa OPEN ni walimu na wengi wameanzia foundation course. Ukweli wapo full kuchanganyikiwa, kupoteza pesa, muda na nk. Eti kusoma kwingi kunaondoa maarifa? kwa kweli huyu mama nafikiri anaangaika kutafuta jibu la kati kuku na yao nani alianza. Muoneeni Huruma asaidiwe.
 
Mada inamuhusu ndalichako MTU analeta habari za lowasa. Mbona amekua wazili Mkuu akaishia kupiga PESA na kukimbia. Kama mama kakosea tumkosoe ila sio kumfananisha na wahuni kama lowasa
 
Mm huyu mama ndio sijuelewagi kabisa sijui huwa anawazaga nini
 
Mada inamuhusu ndalichako MTU analeta habari za lowasa. Mbona amekua wazili Mkuu akaishia kupiga PESA na kukimbia. Kama mama kakosea tumkosoe ila sio kumfananisha na wahuni kama lowasa
Una umri gani pia wakike au wakiume maana hujielewi
 
Ni kweli angeanza na walimu ila Walimu wengi ni failures. Huwezi kuinua elimu kwa kutegemea walimu failures. Serikali itengeneze mazingira ili kusaidia wanafunzi vipanga kusomea ualimu.
 
Lowassa aliwaambia yeye kitu chakwanza kabisa angefanya nikuboresha maslahi ya waalimu maswala ya madawati kwake isingekuwa issue..!!nikapiga akili kwaharakaharaka nikaona angeweza kwenda kwa Mengi akamwambia na hitaji kiasi kadhaa,Mo nakupa tax free kwenye eneo fulani nipe bilioni hapo ya madawati,TRA kwenye kodi ya mwezi huu toeni milioni miatatu ya dawati n.k
Aisee......una akili fupi mno.
 
Kweli......... Walimu wengi ufaulu wetu hafifu.

Unadhani ulivyofeli wewe basi walimu wote wamefeli hivyo....????

Ulivyo kilaza wewe usifikiri na wengine ni vilaza type yako.......

Heshimu taaluma ya watu
 
Hamjui Tu Kosa La Ndalichako Ni Kuwa Ccm Na Kujiunga Kwenye Fitna Tena Akujipambanua Kama Kada
 
Ni kweli angeanza na walimu ila Walimu wengi ni failures. Huwezi kuinua elimu kwa kutegemea walimu failures. Serikali itengeneze mazingira ili kusaidia wanafunzi vipanga kusomea ualimu.

unaposema walimu failures......unakuwa na maana gani labda.....embu fafanua.......

Ni hawa waliokufanya uwe mtu kati ya watu kwenye jamii.....waliokufanya ujitambue.....au unazungumzia walimu wapi hasa.....!!!!!
 
Unadhani ulivyofeli wewe basi walimu wote wamefeli hivyo....????

Ulivyo kilaza wewe usifikiri na wengine ni vilaza type yako.......

Heshimu taaluma ya watu
Povu la nini kiongozi. kwani ktk kusoma kwako hujawahi muita ticha flani yuko shallow. una poovuuu
 
unaposema walimu failures......unakuwa na maana gani labda.....embu fafanua.......

Ni hawa waliokufanya uwe mtu kati ya watu kwenye jamii.....waliokufanya ujitambue.....au unazungumzia walimu wapi hasa.....!!!!!
Acha kujitoa uelewa Mkuu. Accept the fact , seek for solution. kubwabwaja wala hakuta tatua tatizo.
 
naona walimu ndo wamejaa hapa kwenye uzi wao, si madoctor ngoja tupite pembeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom