Mama Ndalichako, kichwa cha nyoka hiki hapa piga!!

Nikusalimu mama, kwanza kabla ya yote mama niseme mimi nakukubali sana utendaji wako tangu ukiwa necta na hata kuchaguliwa kwako nilifurahi sana maana nakukujua na binafsi nimeshafanya kazi Mara mbili na wewe hivyo nakujua kidogo..

Kadri siku zinavyosogea umaarufu wako unazidi kuporomoka kutokana na matamko yako na si utendaji wako!! wadadavuzi Wa mambo wanadai kinachokuponza ni kutamka tu...kila unapopita!! nimejaribu kufuatilia matamko yako nikaona una nia njema ya kuua nyoka lakini unapiga kwenye mkia bila kutafuta kichwa!!

Nakuhakikishia ukipiga kichwani ni fimbo moja tu nzito kuliko kupiga fimbo mia mkiani...

Mama ubora Wa Elimu nchi hii ni WALIMU !! hiki ndio kichwa cha nyoka! Mara majoho, sijui nini, ohh sijui hivi!! huko kote mama unapiga mkiani!!

Kaa vizuri na walimu wako changamoto zao unazijua vyema!! poteza muda wako mwingi kukaa nao na kuwaambia kipi unataka wakifanye katika Elimu Yetu, tatua kero zao, boresha maslahi yao...rudisha ile morali yao ya kazi hiki ndicho kichwa mamaangu!!

Najua siasa inaanza kukutawala kidogo na wapo watakaokunong'oneza kuwa nyoka ukimkata mkia atakufa pole pole!! achana nao .
Umenena yaliyo mema kwa huyu bi mkubwa,yale mazuri yake yote ya necta ameamua kuyazika mwenyewe.
 
Yaani laiti wangejua waalimu wanavyoheshimika katika nchi hizo ambazo cullicilumu yetu tunaiga kwaoo, wasingefanya mambo kama hayaa, yani sie kazi kuiga mitaala tuu basii, vitu vingine hakuna, nchi hii waalimu hawaheshimiwi kabisaa yani wanaonekana kama wajenzi wa madaraja ya viroba ambapo hayo madaraja hayatodumuuu

* Lool.! afadhali ya Jana kuliko leoo*
 
Mada inamuhusu ndalichako MTU analeta habari za lowasa. Mbona amekua wazili Mkuu akaishia kupiga PESA na kukimbia. Kama mama kakosea tumkosoe ila sio kumfananisha na wahuni kama lowasa
Naona brother umeumia kusikia lowasa! Hehehe! Pole huo ndio ukweli!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom