Mama Ndalichako, Elimu yetu siyo salama kabisa

wiser1

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
2,468
3,643
Heshima kwenu wana Jamvi, mie mpya mpya hapa jukwaa la Elimu japokuwa huwa nasoma na kuelewa mada mbalimbali, hongereni.

Ndugu nyote, Ndugu mama Ndalichako,

Elimu, Elimu ,Elimu ya Tanzania Mambo ninayo yaona kwenye Elimu ya Tanzania mpaka naogopa jaman, mwanafunzi level ya masterz anameza kila kitu..anakariri akiingia kwa mtihani anatapika km kilivyo halafu anapata 99, kwenye research anadisco! This is crazy! Mpaka naogopa jaman. Ndalichako sijui yuko wapi mama huyu makini na machachari.

Suala la kupima uelewa wa mwanafunzi level ya masterz kwa kufanya mitihani ambayo ana tapika kila alichomeza SIYO SAWA, ndo maana ufanisi huko maofisini na kazi binafsi HAUPO.

NIMESHUHUDIA MWENYEWE, MTU anaandika hadi nukta ilipokaa ya Vitini vya mwalimu, kiukweli Najua wengine ndo Elimu tuliyopitia na tunafurahi kuvuka ila...balaa lake huku mtaani ni shida kubwaa sana.

Msaada tafadhali,

Pendekezo, wanafunzi level ya masterz na kuendelea wasipimwe uwezo wa kumeza na kukariri, wapewe kazi za kufanya ,kutunga katuni, kuandaa bajeti, kuandaa mapendekezo na mipango maalumu ya kujenga uchumi wa nchi, kumeza na kukariri hakusaidii chochote, ni AIBU KWA SERIKALI NA DUNIA NZIMA.

Nawasilisha.
 
Kwakeli ume nena points muhimu sana sijui serikali aioni ilo au vipi,,,level ya masters and above kama ulivyo sema ni level ambayo ina itaji graduate awe mbobevu na si kukariri coz education system ni ubongo wa taifa ..natunapo uchukulia poa, ubunifu na uvumbuz utakua ndoto
 
Well said ,mkuu! Kwa kweli inasikitisha sana hili jambo
 
Kwa kweli hali ni mbaya sana, mama Ndalichako asikie hiki kilio chetu. Elimu hii ni umasikini
Huku Chini Mambo mabaya,mnasemea masters wenye akili zao? Mtoto anamaliza kidato Cha nne hata barua ya kuomba kazi kwa lugha ya kiingereza hajui kuandika
 
Hatari sanaaa

Mpaka leo vyuo kibao wasomi wengi lakini wakijaa mtaani kwetu hawatofautiani zaidi ya kujua kingereza cha kusoma tuu.

Hata kuongea ni taabu tupu tena Level ya Digree.

Mtu kasoma kwa gharama na muda mwingi lakini tofauti na asie soma ni kiduchu sanaa tena wengine hata tofauti hamnaa wanakula bangi tuu huku mtaani

Wengine dah hata nisiseme maana.
Ni aibu Elimu yetu mtu anashindwa hata kubadilisha bulb.

Ushauri wangu vyuo vingekuwa viwili tuu
UDS na UDOM

Wengine wote tuwe vibarua wa kazingumu sanaa nahisi tungetoboaa
 
kiingereza cha Mama Ndalichako nilikisikia ile siku anaongea na wale wachina daaaaah kilikua ni shiiiiiiiiiida.
Kujua kiingereza sio kipimo cha elimu, bali kiingereza ni lugha kama lugha nyingine tu. Unaweza kuta aliyevumbua ndege hata kiingereza hajui. Shida ni kuwa mfumo mzima wa elimu yetu una shida kubwa.
 
Mbona hivo vyote huwa vinafanyika inform of assignments maana mtihani Ni asilimia hamsini tu marks zote.
 
Huku Chini Mambo mabaya,mnasemea masters wenye akili zao? Mtoto anamaliza kidato Cha nne hata barua ya kuomba kazi kwa lugha ya kiingereza hajui kuandika
Unashangaa form four wakati graduates hawajui hata kuandika barua nzuri, na ninaamini sio kila kitu utafundishwa shule wanachuo wengi wako busy na mitandao ya kijamii baada ya kuongeza maarifa
 
Kujua kiingereza sio kipimo cha elimu, bali kiingereza ni lugha kama lugha nyingine tu. Unaweza kuta aliyevumbua ndege hata kiingereza hajui. Shida ni kuwa mfumo mzima wa elimu yetu una shida kubwa.
Lakini sisi tunatumia mtaala kwa kingereza tofauti na Russia and China so no excuse kwa lugha
 
Kujua kiingereza sio kipimo cha elimu, bali kiingereza ni lugha kama lugha nyingine tu. Unaweza kuta aliyevumbua ndege hata kiingereza hajui. Shida ni kuwa mfumo mzima wa elimu yetu una shida kubwa.

Umesoma O’level,A level,Degree ya 1,Masters,PH.d una miaka ya kutosha kazini na kote huko umetumia kiingereza cha kuongea na kuandika na bado huwezi kuitumia lugha hio mpk leo na unakuja kusema sio kipimo cha elimu?hahahahah inashangaza sana
 
Sio kipimo cha elimu! Wewe elimu yako haijakukomboa kabisa mkuu kama unashindwa kulielewa jambo dogo hili. Kuna shule nyingi sana ambazo hata mwalimu anaongea kiswahili tu darasani. Mimi form five na six 70 percent walimu na wanafunzi tulikuwa tunaongea kiswahili na darasani. Nje ya darasa kiswahili ni full time.

Ukija olevel zipo shule kibao walimu wenyewe hawapo comfortable kuongea kiingereza unadhani wanafunzi inakuwaje? Akirudi nyumbani kwa shule za day mtu unaongea kiswahili muda wote.

Mkuu usiwe mtumwa, elewa tu kuwa lugha haufundishwi darasani bali lugha ni practice. Hata mtu asiyejua kusoma a wala b anaweza kujifunza lugha yoyote bila kuingia darasani ili mradi awe mahali ambapo lugha hiyo inazungumzwa muda wote. Kwa mazingira yetu Tz kingereza chetu tulio wengi kitabaki kuwa cha ugoko labda nyie mliosoma English medium kuanzia chekechea, ambapo na nyie sio fluent speakers mpo kwenye level ya very good but not fluent. Natumai nimekufungua macho kidogo.
 
Lakini sisi tunatumia mtaala kwa kingereza tofauti na Russia and China so no excuse kwa lugha
Excuse ipo wazi kabisa. Huwezi ongea kingereza kama mwingereza vinginevyo uwe umeishi huko kwenye lugha mama kwa miaka mingi tena ukiwa wewe mwenyewe bila mswahili mwenzako wa kupiga naye soga. Kingereza ni lugha ngeni hapa TZ na itabaki kuwa ngeni. Tunao wahandisi wazuri sana na madaktari wazuri sana lkn kwenye lugha hawajafikia level ya "fluent speakers", wengi wao level zo ni "competent user" au "good".
 
Back
Top Bottom