Mama mzazi wa waziri Masha kufikishwa Mahakamani

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
428
LAURA Masha, ambaye ni mama mzazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na mgombea ubunge katika jimbo la Nyamagana kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Lawrence Kego Masha huwenda akaburuzwa kortini akikabiliwa na tuhuma ya kuwasilisha ushahidi wa uongo mahakamani.

Uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na umebaini kwamba Laura aliwalisha ushahidi wa uongo katika mahakama kuu ya Mwanza, dhidi ya kesi iliyofunguliwa na mtoto wa Mzungu aliyekuwa
mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa kampuni ya Kamanga Ferry Limited.

Laura alitoa ushahidi huo wakati wa kesi ya mirathi iliyofunguliwa mwaka 2008 na Mark Alexanda Gaetje ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kamanga Ferry Limited, yenye makao makuu yake mkoani Mwanza.

Uchunguzi huu umebaini kuwa mahakama kuu ya rufaa nchini imetupilia mbali utetezi pamoja na
ushahidi uliowasilishwa na Laura.

Kwa mujibu wa uchunguzi, Mark na wenzake wanakusudia kufungua kesi mahakamani ili mahakama ichukue hatua za kisheria dhidi ya mwananke huyo ambaye pamoja na mambo mengine alikuwa na nia ya kutaka wapoteze haki zao.

Imebainika kuwa kesi hiyo ilifunguliwa katika mahakama mbili tofauti baada ya Gaetje kufariki dunia mwaka 2004 akiwa Uganga kikazi.

Habari zinadai kuwa baada ya kifo chake (Klaus) alijitokeza mwanamke wa Kizungu, Brigitte Defloor
akidai kuwa yeye ndiye alikuwa mrithi halali kwa sababu alikuwa mke wa ndoa.

Uchunguzi umebaini kuwa Laura ambaye alidai kuwa alishuhudia tendo la kufungwa kwa ndoa hiyo Agosti 24 mwaka 2005; ndoa ambayo inadaiwa kuwa ilifungwa wilayani Magu na aliyekuwa Katibu Tawala wa wilaya hiyo.

Imebainika pia kwamba mama huyo (Laura) alitumia kampuni ya uwakili iitwayo Ishengoma, Masha, Mujulizi $ Magai (IMMA Advocates ) kwa ajili ya kukamilisha udanganyifu huo .

Uchunguzi umebaini kuwa katika kesi hizo, mlalamikaji alidai kuwa hamtambui Brigitte kuwa ndiye mrithi wala hakuwa mke halali wa ndoa wa marehemu baba yake.

Uchunguzi umebaini kuwa kesi ya awali ilifunguliwa katika mahakama kuu ya Mwanza ambapo kesi nyingine ilifunguliwa katika mahakama kuu ya rufani, baada ya mlalamikaji kukata rufaa.

Kwa mujibu wa uchunguzi, madai ya Mark yalitupiliwa mbali na mahakama kuu ya Mwanza na hivyo akakata rufaa kwenda mahakama ya kuu ya Tanzania.

Kesi ya kwanza ilihukumiwa na Jaji Sumari ambapo kesi iliyofikishwa katika mahakama kuu ya rufaa
ilitolewa hukumu na jopo la Majaji 3 ambao walikuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mbwana.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mlalamikaji katika kesi hiyo (Mark), alikuwa akiwawakilisha shangazi yake (Helda Gaetje) pamoja na mama yake mzazi , Wieby Gaetje ambaye alikuwa mke wa ndoa wa marehemu Klaus.

Hata hivyo, Uchunguzi huu umebaini pia kwamba Wieby alikuwa ametalikiana na mmewe Klaus Gaetje.

Kwa mujibu wa habari, mwanamke huyo aliwasilisha hati zilizoonesha kuwa yeye alikuwa shuhuda halali wakati wa ndoa ya kiserikali iliyofungwa mkoani Mwanza mwaka 2002 baina ya Wazungu wawili, yaani Brigitte Defloor na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamanga Ferry Limited, Klaus Gaetje.
 
haya ndo mambo ya asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Kama mama mwenyewe ndo hivi sasa huyo mtoto ana hali gani?
 
yule mama ni mhuni sana

anashirikiana na mama wa kambpo wa huyo kijana amabaye ni mtoto halali wa marehemu genji ili waweze kula mari ya marehemu genji
 
na hapa wakisema asiyefunzwa na mamaye, unakamatwa, unatiwa ndani

dunia hadaa, ulimwengu shujaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom