The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,250
- 42,864
Hapa huenda ilikuwa too late hata kuvaa barakoa. Kama ni mwanae basi kuna possibility kubwa alikuwa anamuuguza (kama walikuwa wanaishi wote) hivyo pengine alikwisha ambukizwa. Anyways sipingi wazo lako la kuvaa barakoa ila nimechangia kuonyesha huu ugonjwa unavyokuwa deadly kama hauna muongozo mzuri kutoka serikalini.
Tukiendelea kusubiria muongozo kutoka serikalini tutakwama sana.
CDM wanapiga kelele kila siku kuhusu uwepo wa huu ugonjwa na kuilaumu serikali kwa kutochukua hatua, nilitegemea wawe mfano wa kuigwa inapotokea tukio linawahusu kwa kuzingatia na kufuata taratibu zote za kuzuia maambukizi ya huu ugonjwa.
ACT nao walitangaza kiongozi wao kupata haya maambukizi awali kabisa ( Mungu Amrehem) lakini cha ajabu msisitizo wa namna ya kuendesha shughuli za mazishi na uhusishwaji wa waombolezaji haukutiliwa mkazo na chama kuzingatia maambukizi zaidi wakati wa zoezi zima, hasa maambukizi kati ya waombolezaji.
Hii inaonyesha namna gani hata wanaopiga kelele wanaleta siasa kwenye hili janga.
Pole kwa wafiwa wote na walioguswa na huu msiba.