MwenyeziMungu awape faraja

Unafiwa, unawekwa ndani, unasimangwa hujui kulea, unaambiwa ukachukue mwili wa Mtoto wako ukazike huku ukiwa Mahabusu na unaambiwa ukichelewa mwili unakabidhiwa kwa Halmashauri wakaufukie
 
Dar es Salaam.

Wakati mama na dada wa marehemu Hamza Mohammed wakiachiliwa baada ya mahojiano, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema bado wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi, jirani na ulipo Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi liliwakamata ndugu kadhaa wa Hamza waliokuwa jijini na Dar es Salaam na wengine Chunya mkoani Mbeya.

Hata hivyo, alipoulizwa na Mwananchi kuhusu watu waliokamatwa kutokana na tukio hilo jana, Kamanda Muliro alisema; “Jamani nyie hamtaki tupeleleze? Ni sahihi tuseme hadi wapo mahabusu namba ngapi? Ametoka au hajatoka? Ndugu yangu Mwananchi!”

Wakati Muliro akisema hayo, Msemaji wa familia ya Hamza, Abdul-rahman Hassan aliliambia Mwananchi kuwa watu takribani saba wakiwamo mama na dada wa Hamza wameachiwa na wengine watano wanaendelea kushikiliwa na polisi.
 
Wakamatane wao kwa wao, wawaachie hao watu wasio na hatia.

Waliodhulumu madini tuwajue, Sirro akane hilo kukaa kimya maanake kuna mshindo.

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Nyamaza wewe! hujui upelelezi unavyofanya kazi. popote duniani hao ndugu zake lazima wangebebwa tu.
Sasa ili upelelezi ukamilike si wangekamata na Polisi pia,Siro awekwe ndani ili upelelezi uende vizuri. Yeye km bosi wa polisi ili asaidie upelelezi, Nasema uongo ndugu yangu?
 
Siasa zinawafanya muwe vichaa, mnajifanya kuponda polisi cha ajabu mkikumbwa na mabalaa mnakimbilia polisi.

Sioni cha ajabu ndugu wa karibu kohojiwa.
 
Mama na dada wa yule gaidi katili Hamza Mohamed wameachiwa na polisi huku watu wengine watano wakiendelea kushikiliwa.

Hamza Mohamed alifanya mauaji ya kutisha kabla ya kuuawa kwake pale salenda darajani.

Source: Mwananchi
Hamza the great,kada wa ccm toka ilala
 
Yaani walikuwa bado behind Bars...., Kweli when it rains it pours....
 
Back
Top Bottom