Mama, "mwanangu utafute ufalme wa pesa mengine utazidishiwa"

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
1,314
Mwanangu mimi ndie niliekutafuta nikakuweka tumboni kwangu miezi 9. Siku ya siku ilipofika nilitimiza wajibu wangu wa kukuleta duniani. Kulea ujauzito, kuzaa na kulea mtoto si mambo ya lelemama.

Ndio maana mimi kwa kwako ni "Malkia wa nguvu". Kwa maana hiyo maamini utauzingatia ushauri wangu.Siku zote umekuwa ukilalamika juu ya masuala yako ya mahusiano.

Mara nyingi kama sio zote umetamani kuwa na mtu mmoja umpendae ili aje kuwa mkeo na mimi mama yako nipate fahari kupitia wewe mwanangu. Hiyo limeshindikana kwani kila upatapo mtu mambo hayaendi kama utakavyo. Hili limekuwa likikusononesha si haba.

Kwa kuwa mimi ni mama yapo nilieanza kuliona jua na kukuleta katika hii dunia naomba uzingatie hili mwanangu. "Tafuta kwanza ufalme wa pesa mengine utazidishiwa ikiwa ni pamoja na ulimwengu wa mapenzi".

Tangu enzi za Bibi yake na Bibi yake mama yangu mwanamke ni mtu mwenye kupenda pesa zamani zile kama mwanaume hana ujasiri wa kuiba ng'ombe, kucheza ngoma au si mganga wala "Jumbe /mangi/mtemi" alikuwa akipata mwanamke ili mradi.

Hayo niliyoyataja hapo juu kwa tafsiri ya leo ni nguvu ya pesa au uchumi. Mwanamke anataka akiona wigi la milioni 3 walau uwe na milioni 2 za kumpa ili 1 aongeze. Anataka ikifika "birthday" yake au ya wanae afanye sherehe yenye kusisimua kama sio kuacha simulizi. Tafsiri ya haya yote ni pesa.

Mwanangu tafuta pesa, tafuta sabuni ya roho, tafuta money, tafuta "pakee". Badala ya kutongoza mwanamke atajiweka barabara mwenyewe ili gari limgonge. Wao wenyewe wataenda "kupikwa nyungu" kama sio kupewa "makombe" ya kutumia ili nyota zao zing'ae wakupate.

Yangu yalikuwa hayo mwanangu, baraka zangu zikufikie huko uliko ili jina lako liwe miongoni mwa watakaoingie kwenye ufalme huu mpya. La mwisho mwanangu ule msemo "Mjini msingi kiuno" naomba uupuze. Waachie wengine na si wewe.
 
kweli, mimi mwenyewe huwa nawaambia wanangu pesa ndio msingi wa furaha katika maisha
 
Pesa sio msingi wa furaha,unaweza kuwa na pesa telee...majumba ya kifahari lakini unashida zimekujaa na fedha haiwezi kutatua shida hizo kwa mfano magonjwa km kisukari,ugumba,ukimwi nk
 
Pesa sio msingi wa furaha,unaweza kuwa na pesa telee...majumba ya kifahari lakini unashida zimekujaa na fedha haiwezi kutatua shida hizo kwa mfano magonjwa km kisukari,ugumba,ukimwi nk
Kama pesa haileti furaha, nini kinaleta furaha?
 
Pesa sio msingi wa furaha,unaweza kuwa na pesa telee...majumba ya kifahari lakini unashida zimekujaa na fedha haiwezi kutatua shida hizo kwa mfano magonjwa km kisukari,ugumba,ukimwi nk
hehehe hapo tofauti ya mpunga na mchele sasa
 
Pesa sio furaha maan kuna watu wana pesa ila awana furaha hata kdg wanataman maisha ya furaha na wanapesa zao lkn awaipati iyo furaha
 
Back
Top Bottom