The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 376
Habarini ndugu zangu.
Baada ya miaka mitatu ya mahusiano, mwezi wa nne mwenzangu alinimwaga bila sababu. Nilimuheshimu, nilimjali, nilimsupport kwa mambo yake nk. Aliniambia kanichoka na upendo tena haupo hivyo nimwache akatafute upendo mahala pengine.
Ilikuwa ngumu kukubali ukuzingatia home kwao kote nilijulikana ingawa haikuwa rasmi na kitendo hicho kilimfanya mama mkwe awe karibu sana na mimi.
Mimi sina wazazi. Mama mkwe amekuwa karibu yangu kiasi cha kuogopa nitamlipa nini. Nikiumwa yupo muda wote, nikipata shida yeye ni wa kwanza kunisaidia. Amekuwa rafiki sana kwangu kiasi cha kujua ninapopata shida hata kama sijaongea.
Of course anajua juu ya relationship yetu na hata tulipogombana anajua. Sasa kinachonipa mawazo, Jana nilikua napiga nae story. Sielewi mada za ndoa zilikujaje ndipo nikaropoka kuwa mimi natafuta Pesa na wala sitaki ndoa.
Mama mkwe hakukubaliana na Mimi na maneno aliyokuwa akiongea ni kama vile anataka kunirudisha kwa mtoto wake tuliyetoka kugombana naye toka mwezi wa NNE.
Binafsi nafikiria kumkimbia huyu mama mkwe, nikijaribu kuzima simu anakuja hadi home.
Sijui nifanyeje kumkimbia huyu mama bandugu maaana naona ataturudisha kule tulipotoka.
Msaada tafadhali.