Mama mkwe kajichimbia naona shida kumtoa

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,130
2,000
Daah
Mkuu kwanza pole sana. Inawezekana wengi wanaoponda au kuwa na negative perspective hawajawahi kupitia unapopitia. Kama kuna mtu ashawahi kuwa na mpenzi wa "mama kasema" anaweza akaelewa kile unachopitia. Kimsingi, hakuna ndoa au maisha yanayoweza kusonga ndani kukiwa na wanawake wawili wanaogawana maamuzi yako. Yaani hapo kama vile nakuona: huyo bibie kila jambo anarefer kwa mama yake. Mama kasema, mama hapendi, mama kashauri, mama anataka, mama... mama ... mama ... as if wewe ulitoka kwenye mti, yaani hauna mama
Anyways, mtongoze mama mkwe wako: next morning akiwepo home kwako njoo nikuongezee mbinu. Sumu/Dawa ya mwanamke ni mwanamke mwenziye
 
42774277

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
4,060
2,000
Nikuambie kitu mkuu, huyo mama amekuja kusaidia uzazi, unatakiwa kwanza ushukuru kwa msaada aliofanya. Najua wakati mwingine hizi nyumba zetu inakuwa ngumu kuwa na idadi kubwa ya watu coz space yaweza kuwa ndogo na uhuru wako pia.

Lakini likija swala la wazazi (iwe wa upande wako au wa mkeo), jaribu sana kuishi nao kama wa kwako, ukiweka matabaka namna hiyo hata siku akija mama mzazi mkeo anaweza kusema siwezi kuishi na mama yako.

Hawa ni wazazi wetu, baadhi hawapendi kabisa kukaa kwa watoto mda mrefu(wanajua madhara yake), wale ambao hawaelewi basi twende nao hivyo tu.
Mzazi anahamiaje nyumbani kwa watoto. Katika hili mimi siwezi kukubali
 
masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,731
2,000
Ila ujue km kipato ni cha kawaida biashara sio ya kukurupukia sjui mtaji atatoa wapi gafla ili atatue ilo tatizo
Dada nimekupenda Bure maana unaakili sana...
Kuna watu wanafikili kufanya jambo au kuanzisha jambo ni kitu cha kuanza tu unapojisikia
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,405
2,000
Fanya mpango kila ukienda home usibebe chochote vile vizawi zawadi acha kabisa wee ukienda nenda kama ndo unaenda bar na kwenye hela ya matumizi wee acha hela kidogo tuu
 
ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
29,595
2,000
Mzazi anahamiaje nyumbani kwa watoto. Katika hili mimi siwezi kukubali
Sio kila mzazi(familia) inafanya mnavyofanya nyie, kumbuka ulivyooa umeingia kwenye familia yenye hulka tofauti na za kwenu. Lazima ukubaliane na hali utakayoikuta. Kwa wazazi waelewa ni rahisi mno, a week or two is enough kumtembelea mtoto, lakini kama sio wa ustaarabu huo ishi na furahia maisha na wazazi wako.
 
Sweet16

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
4,382
2,000
Nikuambie kitu mkuu, huyo mama amekuja kusaidia uzazi, unatakiwa kwanza ushukuru kwa msaada aliofanya. Najua wakati mwingine hizi nyumba zetu inakuwa ngumu kuwa na idadi kubwa ya watu coz space yaweza kuwa ndogo na uhuru wako pia.

Lakini likija swala la wazazi (iwe wa upande wako au wa mkeo), jaribu sana kuishi nao kama wa kwako, ukiweka matabaka namna hiyo hata siku akija mama mzazi mkeo anaweza kusema siwezi kuishi na mama yako.

Hawa ni wazazi wetu, baadhi hawapendi kabisa kukaa kwa watoto mda mrefu(wanajua madhara yake), wale ambao hawaelewi basi twende nao hivyo tu.
Ila inawezekanaje mama kuhamia kwa mkwe bana?? Ukute ndo wale wa kutoka na kanga kifuani kajifunga bila nguo nyingine, mara wapishane wagusane na mkwe koridoni khaaa iyo apana kwa kweli
 
ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
29,595
2,000
Ila inawezekanaje mama kuhamia kwa mkwe bana?? Ukute ndo wale wa kutoka na kanga kifuani kajifunga bila nguo nyingine, mara wapishane wagusane na mkwe koridoni khaaa iyo apana kwa kweli
Nasema tena, tumezaliwa katika familia tofauti, tunakutana na watu wenye hulka tofauti. Huenda labda hujaingia kwenye ndoa na hujapata experience ya upande wa pili. Ndoa ni "takatifu" lakini ina changamoto nyingi, na moja ya hizo ni kuweza kuishi na watu wa upande wa pili kama ndugu zako wa damu.
 
masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,731
2,000
Wengi wanashauri tu kwa maandishi ila kiuhalisia ata kwa upande wao hawawezi kufanya vile
Hakuna wakati ambapo huwa inakuwa makini kiushauri kama nikiwa namshauri mtu aliye block. Yaani hana ramani ya maisha..maana sio wa kumlaumu na lazima ujue uwezo wake kwanza na udhaifu wake na mazingira yake..tofauti na hapo utaishia kumlaumu tu kuwa jamaa Fulani ni mvivu na anachagua kazi...
 
City owl

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,004
2,000
Dalili zinaonesha mkeo ndiye anayetaka mama yake aendelee kuwepo ndiyo maana alikuambia hata mkipata maid, bado mama ataendelea kuwepo.
Hivyo, anza na mkeo. Mfanye aelewe umuhimu wa mama kuwaachia nafasi, arudi kwake akaendelee na shughuli zake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom