Mama mkwe ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,179
Leo asubuhi, baada ya kumsalimia mama mkwe, ameniuliza mimi na mtoto wake tulikutana wapi? Nimeshindwa kumjibu kwasababu sijaelewa mantiki ya swali lake.

1. Akishajua itamsaidia nini?

2. Au hajaridhika kuwa mimi nina hadhi ya kuwa mkwe wake?
 
Kwanini asimuulize mwanae jamani! Na hata mwanae kimsingi hapaswi kumuuliza swali kama hilo. Wakwe wengine, mungu awasamehe tu
 
Kwanini asimuulize mwanae jamani! Na hata mwanae kimsingi hapaswi kumuuliza swali kama hilo. Wakwe wengine, mungu awasamehe tu

Niling'ata meno, kwasababu ningeruhusu maneno yatoke ninadhani hali ingekuwa mbaya sana.
 
Mawazo mabaya huleta matokeo mabovu ukianza na fikra za kipuuzi namna hiyo hata hiyo ndoa utaiona chungu na hakuna jema utaliona kwa mama mkwe wako BTW HUYO NI MAMA YAKO KAMA ALIVO MAMA YAKO WA KUKUZAA.

(anaweza kuwa ni mtu wa utani alitaka akuchekeshe kitu huo ni mtizamo wangu KILA LA HERI)
 
Mbona swali la kawaida hilo? kwani we ukikataa kumwambia itakusaidia nini?
 
Ni vyema mzazi ajue ulipokutana na mwanae isije ikawa mmekutana stendi usiku.
 
mjibu tu kilabuni,kwani si umeshamuoa,hatakunyang'anya mkeo,mimkwe mingine bwana
 
mmmh huyo mama analake jambo ili kumkata stim mwambie mlikutana bar usiku then mwanae akavutiwa na unywaji wako, mlipomaliza kunywa mkaingia disco kulimwaga sebene asubuhi mkajikuta mpo gest ndipo mwanzo mlipokutana kimwili.au ye anataka kujua sehemu tu? manake kukutana kuna maana zaidi ya moja.mama mkwe wengine bana looh
 
Amekuja kutujulia hali, yeye anaishi mkoani.

Ok, Inategemeana amekuuliza katika mazingira gani? kama maongezi ya kawaida si unarespond tu tokana na kile mlichokuwa mnaongelea!! Lakini alipaswa kuuliza wakati wa Harusi.
 
Mwambie mlikutana baa.

Tena Corner Bar kabisa

mother-in-law.gif
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom