Mama Mkwe amenishangaza! Anamwambia mke wangu (Mwanaye) ataachana na mimi kama yeye alivyoachana na Baba Mkwe

Kaka, tulia kabisa urelax, hakuna laana palipo na haki, kama mkeo hajamtukana mama yake. Be conscious kwa kuwa mnalifaham hilo. Mama hakujisikia vizuri mlipoanzia kwa mme wake wa zaman, ali feel undermined na kupuuzwa. Relax na mtengeneze stronghold na mkeo. Mama mkwe wako ana shida kichwani
 
Kusema ukweli binafsi nimeoa familia ambayo mama na baba walitengana, ila mtu akija kuniomba ushauri kijana anaetaka kuoa mtanisamehe sana ila siwezi kumshauri akaoe kwenye nyumba ambayo baba na mama walitengana, kama kifo ndio kiliwatenganisha hapo sawa ila eti baba anaishi na mama anaishi huku wametengana mimi atakaenishauri ntamwambia asioe kwenye familia hiyo. Kwa kesi ya binti kuolewa kwenye familia ambayo wazazi walitengana sina experience nayo ila kwa mwanaume kuoa binti ambae baba na mama waliaachana mazima kila mtu anaishi kwake tafadhari fikiria mara mbili there is a consequences. Kwa ntakaemkwaza anisamehe ila ukweli ndio huo
Endelea kufunguka... inakuaje ukioa ktk familia wazazi waliachana.. nini hutokea baadae.

Binafsi nimeona vinana wengi wameachana, lkn wazazi wao wakiwa bado pamoja ktk ndoa.

Na nimeona ndoa nyingi ziko imara, ili hali wazazi walishatengana kitambo
 
Fanya yako. Tengeneza ndoa yako na maisha yako, ishi vizuri na mkeo.
Hata mimi niliambiwa kama wewe ulivyoambiwa, mwaka wa 10 huu ndoa bado ina amani tele. Waliokua wanasubiri tugombane, bado wanahesabu miaka.
Changamoto kwenye ndoa hazikosekani; Lakini waamuzi wa kwamba ndoa yao iwe na amani kwa muda gani ni wanandoa wenyewe, si mtu mwingine yoyote wa nje Clinker belite
 
Awali ya kwanza, usimchukie mkwe upande wa baba wala Mama hata chembe. Chuki huzuia Baraka kutoka kwa Mungu. Pili kama wewe ni mtu mcha Mungu, usiwe na wasiwasi. Kumbuka katika familia kuna mgonjwa ambayo huridhiwa( generational inheritance like sickle cell, cancer, HBP, mental disorder, uchawi) magojwa na kuridhi. Kwa kithungu huitwa “family curses, generational curse” ambayo ni Mtumishi wa Mungu wa kweli ndiye anaweza kuyavunja yaani healing and deliverance. Kama mke wako hatakuwa delivered itafiki kipindi yatatokea kwako! She has to be delivered by a True Man of God na siyo siyo kwa Ma Pastor wa hivihivi. Yaani siyo kuambiwa kupanda mbegu ndo aombewe, not at all. Mchungaji wa kweli hadai hata senti moja kabla au baada ya deliverance, ni free of charge. Kama unataka msaada mtafute Mama Brandina Nyoni ambaye wakati fulani alikuwa Katibu Mkuu wa wizara, moja utapata maelekezo. Hii ni kwa faida yako ya familia yako else hiyo curse itawafika.
To be delivered from what? Sijaelewa aisee. Mke amanahitaji deliverance???
 
Guest au kwenu kama ni karibu kama hamna guest ni bora kulala hata kwa jiran, wachaga wanaelewa hili vizur
Mfano, tunaishi dar. Home kwetu mimi ni mbeya. Na ukweni ni ifakara..

Nalalaje guest? Nasemeje yaan nnavoaga
 
Fanya yako. Tengeneza ndoa yako na maisha yako, ishi vizuri na mkeo.
Hata mimi niliambiwa kama wewe ulivyoambiwa, mwaka wa 10 huu ndoa bado ina amani tele. Waliokua wanasubiri tugombane, bado wanahesabu miaka.
Changamoto kwenye ndoa hazikosekani; Lakini waamuzi wa kwamba ndoa yao iwe na amani kwa muda gani ni wanandoa wenyewe, si mtu mwingine yoyote wa nje Clinker belite
Shukran bro.
 
Pole sana mkuu ,watu wa ifakara wanaongea sana,jamii za wandamba na wapogoro ni kama wazaramo tu,wana maneno mengi sana na ukichangia pia huyo mama ametengana na mumewe yawezekana bado anatamani maisha ya ndoa.

Muhimu wewe endelea kuishi na Mke wako kwa upendo kwani maisha ya ndoa hayana kanuni maalum,kila ndoa huwa na furaha yake na changamoto zake,ndoa ya mama mkwe sio yako na mkeo
 
Kusema ukweli binafsi nimeoa familia ambayo mama na baba walitengana, ila mtu akija kuniomba ushauri kijana anaetaka kuoa mtanisamehe sana ila siwezi kumshauri akaoe kwenye nyumba ambayo baba na mama walitengana, kama kifo ndio kiliwatenganisha hapo sawa ila eti baba anaishi na mama anaishi huku wametengana mimi atakaenishauri ntamwambia asioe kwenye familia hiyo. Kwa kesi ya binti kuolewa kwenye familia ambayo wazazi walitengana sina experience nayo ila kwa mwanaume kuoa binti ambae baba na mama waliaachana mazima kila mtu anaishi kwake tafadhari fikiria mara mbili there is a consequences. Kwa ntakaemkwaza anisamehe ila ukweli ndio huo
Nimekuelewa sanaaa mkuu....kupitia maelezo yako kuna kitu nimejifunza,upo sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom