Mama Mkapa abanwa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,155
29,607
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Mama Mkapa abanwa
Gloria Tesha, Dodoma
Daily News; Wednesday,July 17, 2008 @19:01

Serikali imeombwa kufuatilia madai kwamba mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Anna, anawakata riba kubwa walimu kupitia kampuni ya ukopeshaji. Kwa mujibu Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) wakati akichangia makadirio ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi bungeni juzi jioni, kampuni hiyo hutoza riba inayofikia asilimia 67 na wakati mwingine hadi asilimia 200.

"Walimu wanasikitika na suala hili na wamenituma niulize bungeni kama huu si wizi ni nini, kwa sababu wamekuwa wakitozwa riba kubwa kuliko kampuni nyingine na kutokana na shida walizonazo imewabidi wachukue mikopo hiyo," alisema. "Mara nyingi shughuli za vigogo wakubwa hazisemwi hadharani, lakini hii naomba niseme.

Inamilikiwa na Anna Mkapa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (Ibrahim) Kaduma," alisema Zambi na kuitaja kampuni hiyo kuwa ni Bayport Financial Services aliyosema ina wamiliki wengine ingawa hakuwataja majina.

Kwa mujibu wa maelezo ya Zambi, wamiliki wa Bayport wakishirikiana na wadau wengine wamekuwa wakiwakopesha watumishi wa umma hasa walimu, kwa mfano Sh milioni moja na kutakiwa kulipa Sh milioni tatu katika kipindi cha miaka mitatu.

“Walimu wa Mbozi wamenituma na pengine wapo wa majimbo mengine wanakumbwa na tatizo hili. Ni upi uhalali wa kampuni kuwatoza walimu riba kubwa hivyo katika mikopo kama kweli tunalenga kuinua elimu?” alihoji Zambi.

“Wataalamu wa kampuni hii walipokuwa wanatangaza kampuni yao hawakusema riba ni kiasi gani. Kulikuwa na udanganyifu na waathirika wakubwa ni watumishi wa umma,” alisema Zambi na kuongeza; “mikopo yote hutolewa kati ya mwezi mmoja hadi miezi 36.

Hata hivyo, Mbunge huyo hakuweza kueleza kiasi cha hisa kinachomilikiwa na kila mwanahisa katika kampuni hiyo.Akijibu hoja hiyo Waziri Maghembe alisema suala la mikopo linategemea muda wa urejeshaji, lakini akasema hoja ya Zambi imezingatiwa na itafuatiliwa kwa umakini.

Hata hivyo, aliwatahadharisha walimu kuwa makini wanapochukua mikopo. Malalamiko ya bungeni jana ni mlolongo wa tuhuma kadhaa za ukiukwaji wa misingi ya biashara ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi ya familia ya Rais mstaafu Mkapa katika siku za karibuni.
 
Hii inatisha sana, at the same time imekiuka Code of Conduct kwani Mama Mkapa ni kioo cha jamii. Amemchafua Mh. Mkapa, cha kufanya ni yeye kuwarudishia kiasi chote alicho wazulumu walimu hao.
 
Back
Top Bottom