Mama Mghwira kwa hili hapana! Umetoa majibu mepesi kwa jambo zito sana

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Vifo vya watu 20 kwenye mkutano wa mtumishi Boniphace Mwamposa


Kwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro Mama Mghwira .

Kauli yako kuwa kulikuwepo na utaratibu mzuri tu kwa watu kukanyaga mafuta ila vibaka waliharibu utaratibu kusababisha maafa yaliyopelekea vifo vya watu 20 haijakaa vema.

Sifahamu chanzo hasa cha vifo hivyo lakini kwa mtazamo wangu majibu yako ni mepesi mno kulinganisha na uzito wa tukio lenyewe.

Mama Mghwira huu ni msiba wa kitaifa na watu wana huzuni kubwa kwa kuwapoteza wapendwa wao.

Ungelitoa nafasi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina na kisha kutoa taarifa.

Taarifa ya uchunguzi huo kwa maoni yangu ingalitolewa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi!

Pole sana mama mgwira ila kwa jambo hili natofautiana na wewe.

Mungu azipumzishe mahala pema roho za marehemu

images (1).jpeg
 
Vyombo vya ulinzi na usalama vipi tena? Hujui kuwa mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa? lile tamlo Kalitoa kwa niaba ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa baada ya uchunguzi
 
Boniphace Kichonge,
Nimemsikiliza hata mimi nikagundua hajui nini la kuongea halafu kajivua lawama wakati yeye mwenyewe ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa.

Viongozi wa Tanzania hawajui kitu kinaitwa uwajibakaji. Kaenda mbali zaidi na kuanza kunang'a imani za watu kuwa ni wafanyabiashara. Inawezekana ndiyo ni kweli ila sasa unawapimaje kamani wafanyabiashara na hawa si wafanyabiashara?
 
Back
Top Bottom