Mama Mdogo Kuliko Wote duniani Kujifungua Mtoto wa Tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Mdogo Kuliko Wote duniani Kujifungua Mtoto wa Tatu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 13, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,627
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  Mama Mdogo Kuliko Wote duniani Kujifungua Mtoto wa Tatu


  Stacey Herald anatarajia mtoto wa tatu ingawa madaktari wamemuonya maisha yake yako hatarini Friday, November 13, 2009 6:46 AM
  Mama mwenye umbile dogo kuliko wote duniani anatarajia kujifungua mtoto wa tatu ingawa madaktari wamemuonya kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na tumbo lake kuwa kubwa sana kuliko mwili wake kiasi cha kumfanya ashindwe hata kutembea.
  Stacey Herald, ambaye ana urefu wa sentimeta 71 anatarajia kujifungua mtoto wa tatu ingawa madaktari wameendelea kumuonya kuwa maisha yake yako hatarini kutokana na mimba aliyonayo.

  Stacey alishayapuuza maoni ya madaktari mara mbili na kufanikiwa kujifungua watoto wawili ambao urefu wao wakati walipozaliwa ulikuwa ni zaidi ya nusu ya urefu wake.

  Stacey mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Dry Ridge, Kentucky nchini Marekani anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Osteogenesis Imperfecta, ambao husababisha mifupa kuwa dhaifu yenye kuvunjika kirahisi, mapafu dhoofu na ugonjwa huo umemsababishia asirefuke.

  Stacey anaishi na mumewe Will mwenye urefu wa mita 1.75 na wanatarajia kupata mtoto wa tatu ndani ya wiki nne zijazo.

  Kutokana na ukubwa wa tumbo lake la ujauzito, Stacey hawezi kufanya kazi yoyote ya nyumbani na humtegemea mumewe kufanya kazi hizo.

  Kwa jinsi alivyo mfupi, mtoto wake atakayemzaa atakapofikisha umri wa mwaka mmoja atakuwa tayari ameishamzidi kwa urefu.

  Pamoja na vikwazo vyote, wanandoa hao ambao walivalishana pingu za maisha mwaka 2004, wamesema wangependa kupata watoto zaidi.

  Lakini madaktari wamemuonya Stacey kuwa mtoto aliye tumboni mwake anaendelea kukua na umbile lake litakuwa kubwa zaidi kuliko mwili wake mdogo na hivyo kupelekea viungo vyake vya ndani kupasuka na kupelekea kifo chake.

  Hata hivyo Stacey amepania kuendelea na ujauzito wake kama mimba zake mbili zilizopita ambazo aliambiwa maneno kama hayo lakini aliyapuuza na kuzaa salama.

  Mtoto wake wa kwanza Kateri alizaliwa mwaka 2006 akiwa na urefu nusu ya urefu wa mama yake kwa bahati mbaya alirithi ugonjwa wa mama yake kwahiyo naye pia hatarefuka atakuwa kama mama yake.

  Stacey alipata mimba kwa mara nyingine mwaka uliofutia na alijifungua mtoto mwingine wa kike aliyepewa jina la Makaya.
   
Loading...