Mama Maua Daftari

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,517
4,987
Jamani huyu mama ni mara chache anaongelewa, sina hakika ila niko tayari kukosolewa. Nadhani huyu mama si wakuwekwa kwenye kundi la mafisadi. Amekuwa naibu waziri kwa muda mrefu na pengine kuliko wote tulo nao. Sasa wanajamvi mnamwonaje. Narudia tena nadhani sio fisadi na kama nimekosea niko tayari kukosolewa!
 

Attachments

  • DSC03230.JPG
    DSC03230.JPG
    44.2 KB · Views: 137
Mmh alikuwa na kesi mahakamani ya kumtapeli mkazi wa Kibaha mamilioni sijui hiyo kesi imeishia vipi,kwa kifupi si msaafi kwa sana kwani kwa kiongozi kuwa na kesi ya utapeli si sifa nzuri,ngoja ninukuu usemi maarufu wa hapo kale ni kuwa mke wa kaisari aliwahi kutuhumiwa,naam mfalme akamtimua akisema mke wa mfalme hatakiwi kutuhumiwa
 
jamani huyu mama ni mara chache anaongelewa, sina hakika ila niko tayari kukosolewa. Nadhani huyu mama si wakuwekwa kwenye kundi la mafisadi. Amekuwa naibu waziri kwa muda mrefu na pengine kuliko wote tulo nao. Sasa wanajamvi mnamwonaje. Narudia tena nadhani sio fisadi na kama nimekosea niko tayari kukosolewa!



Unajaribu kumwosha kabla ya uchagzi mkuu?. kutoongelewa si kwamba yeye ni msafi kihivyo bana, wapo Mawaziri wengi kweli orodha ya kabineti ya JK hawajawahi kabisa kuongelewa/kutajwa vibaya lakini hilo halimaanishi wapo mswano kwa vitendo vyao.

Daftari alishauguswa mara kibao hata hapa ndani bana kwa mfano hii hapa chini yamhusu yeye huyo Daftari:

kampuni mpya ya ndege...mama maua daftari umo?
pakajimmy
user_offline.gif
22nd january 2010, 01:19 pm


kuna kampuni mpya ya ndege inaitwa air zara international!

jumapili 17/1/2010 walizindua rasmi safari za arusha, wakiwa wameandamana na waandishi wa habari kibao toka dar.

na watu kama mimi tukazipata habari hizo, tukaenda kufuatilia.

katika msafara huo wa uzinduzi, mkuu wa msafara wa uzinduzi alikuwa naibu waziri wa miundombinu, maua daftari.

mama huyu hakujivunga pale, akatuomba tuliokuwepo pale tusaidiane kutafuta wateja ili kuiungisha kampuni hiyo mpya.

jumatatu, waziri huyo alikuja tena arusha, akaongelea ndege hiyohiyo, kuwa itakuja tena alhamisi na kumchukua yeye na abiria wengine.

alhamisi, wanafamilia wa huyu mama walisafiri na ndege hii jioni.

kuna tetesi kwamba mama huyu ana hisa katika kampuni hii kutokana na ukaribu wake na uongozi wa ndege hii, na kufikia hatua ya kuipigia debe bila woga!

hongera mama kama ni kweli. Kilimo kwanza bana, kwani nini!
 
Hapana best simsafishi sikujua kuwa naye yumo kweli nimeamini kimya kingi....
sasa hii sirikali ya ccm kuna mzima kweli?

Zipo sura nyingi tu hazijawaji kutajwa hapa kwa uovu lakini zinakula nchi kimya kimya hapa . Waweza kuzitambua
attachment.php
 
Back
Top Bottom