Mama Maria Nyerere awalipua mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Maria Nyerere awalipua mafisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JoJiPoJi, Aug 10, 2009.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,471
  Likes Received: 1,426
  Trophy Points: 280
  MJANE wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, ameibuka na kusema kuwa ufisadi umeliangamiza taifa, ndiyo maana maisha ya Watanzania yameendelea kuwa duni hata baada ya kujikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni.
  Mama Maria alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Huduma za Nishati na Ujasiriamali Endelevu - Machame (Machame COSEESE), uliofanyika wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, ambapo Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, alikuwa mgeni rasmi.
  Machame COSEESE, imeanzishwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayoshughulika na uendelezaji wa teknolojia za nishati endelevu na kuhifadhi mazingira (TaTeDO), wakishirikiana na taasisi inayojishughulisha na uundaji wa vikundi vya kijasiriamali kwa ajili ya kupunguza umaskini (VICOBA).
  Huku akionekana mwenye afya njema, Mama Maria alisema siku zote huwa anajiuliza sababu ya umaskini wa Watanzania wakati nchi ina rasilimali za kutosha na hali ya hewa nzuri kwa kilimo na kubaini kuwa umaskini wa Watanzania umetokana na ufisadi.
  ‘Siku zote nimekuwa nikijiuliza, kwa nini Watanzania ni maskini wakati wenzetu hasa wale wanaopitiwa na mstari ule wa Ikweta, wanapata maendeleo haraka, hasa zile nchi zenye hali ya hewa nzuri? Tatizo letu ni ufisadi. Rushwa hii itaisha lini?” alihoji Mama Maria Nyerere na kushangiliwa na umati wa wananchi wa Machame.
  Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk. Norman Sigalla, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mama huyo wa taifa alienda mbali kwa kusema kuwa unyonyaji unaofanywa na mafisadi hao ambao hakuwataja majina, umefanya baadhi ya watu kuwataja kwa majina na kufanya hivyo si kuwahukumu bali kutokana na uchungu.
  Kwa mujibu wa Mama Maria, ufisadi umelifanya taifa la Tanzania kuendelea kuwa ombaomba wakati liko huru kutoka mikononi mwa wakoloni.
  “Wengine wanasema Tanzania ni maskini kutokana na kutawaliwa na wakoloni, mimi nafikiri si sahihi kusema umaskini wetu umetokana na kutawaliwa na wakoloni, hiyo isitumike kama sababu ya umaskini wetu,” alisema Mama Maria.
  Akizungumza kwa hisia kuhusu umaskini, Mama Maria alisema hivi sasa baadhi ya afya za Watanzania ni duni kutokana na kutokuwa na uhakika wa chakula.
  “Tunahitaji watoto wawe na afya, lishe nzuri kama watu na watoto wa hapa Machame ninavyowaona, nami mnisaidie niwe na afya nzuri. Kwa sasa afya yangu ni nzuri, umri wangu bado si mkubwa sana, natembea na mkongojo kwa sababu tu sina mazoezi, lakini ningekuwa na mazoezi nadhani afya yangu ingekuwa nzuri zaidi kwa sababu taifa linanitunza vizuri,” alisema Mama Maria.
  Mama huyo wa taifa alimmwagia sifa Mengi kwa kazi anazofanya na moyo wa kujitolea katika kutoa misaada mbalimbali kwa vikundi vya kijamii kwa ajili ya maendeleo yao.
  “Ukipata pesa, usikimbilie kwenda sehemu kama Zanzibar au sijui wapi kutafuta ukimwi, wape na hawa wengine ili wajikwamue na umaskini kama anavyofanya Mengi,” alisema Mama Maria.
  Kabla ya kuzungumza na wananchi wa Machame, Mama Maria aliweka shada la maua kwenye kaburi la Dk. Elbenezer Mwasha, ambaye alikuwa daktari wa Mwalimu Nyerere.
  Kwa upande wake, Mengi ambaye alitoa hundi ya sh milioni 210 kwa ajili ya taasisi hiyo na watoto yatima na wenye ulemavu wa ngozi (albino), alisema adui mkubwa wa taifa kwa sasa ni ufisadi.
  Alisema mafisadi Watanzania, wana roho ngumu, kwani wanatembea kifua mbele na wanapotajwa, wanakimbilia mahakamani.
  “Watu wakimkamata kibaka, wanampa kibano, lakini mafisadi ukipambana nao, wanakimbilia mahakamani, lakini tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete, kinara wa mapambano hayo, ametoa uhuru wa vyombo vya habari kuibua mambo ya ufisadi, kwa sababu yeye si fisadi na ufisadi mwingi ulioibuliwa sasa, ulitokea kabla hajaingia madarakani,” alisema Mengi.
  Kuhusu ujasiriamali, Mengi ambaye aliwapongeza wananchi wa Machame kwa hatua hiyo, alisema tatizo la watu wengi ni kutojiamini, hasa wanapotaka kuingia kwenye biashara.
  Mengi alitumia muda mwingi kueleza jinsi alivyoanza biashara katika mazingira magumu, alisema kilichomfanya afanikiwe hadi kufika mahala alipofika leo, ni kujiamini na kujiona kama anaweza, hata kama hakuwa na uwezo huo.
  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofana, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk. Sigalla kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega, alisema Mengi si mkabila kwani shughuli anazozifanya kusaidia vikundi vya kijamii, viko nchi nzima.
  “Kama humpendi Mengi, basi zipende jitihada zake, lakini inawezekana vipi upende jitihada zake halafu mwenyewe usimpende?” alihoji Dk. Sigalla.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa VICOBA nchini, Devota Likokola, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), alisema kazi anazozifanya Mengi leo, ndizo alizozipigania Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake, kupigana na umaskini na kutetea hali za wanyonge.
  Mbunge huyo ambaye alitamba kwamba VICOBA imepiga hatua katika kupambana na umaskini, alisema amedhamiria kupambana na umaskini na sasa taasisi hiyo imesambaa nchi nzima na kuwataka wananchi kujiunga, ili waweze kunufaika. Katika risala yao, wana vikundi vya Machame COSEESE, walisema lengo la kituo hicho cha kwanza na cha aina yake nchini, kina lenga kutoa huduma za sekta ambayo kwenye jamii haijapata msukumo wa kutosha. Kwa mujibu wa risala hiyo, wanachama wa vikundi hivyo wanajishughulisha na ujenzi wa majiko sanifu ya kuni majumbani na kwenye taasisi kama shule, uokaji kwa kutumia matanuri sanifu ya mkaa, ufungaji wa mitambo ya umeme wa jua, vitalu vya miti na shughuli nyingine mbalimbali za ujasiriamali.  Chanzo
  Tanzania Daima
   
 2. Companero

  Companero Platinum Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Naam nilimwona kwenye runinga. Kuna kamfano ka ufisadi alikatoa huku akiashiria kwa mikono, ni balaa. Ni kuhusu tabia ya kifisadi ya kunyoosha mkono. Yana mwisho haya!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Aug 10, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Ufisadi utapungua endapo tu CCM itawekwa benchi. Zaidi ya hapo sioni mwanga mwisho wa tanuru!
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Huyu naye katokea wapi tena.
  Zake si zimepita, enzi hizi za kina Salma Rashid Kikwete bana!!!
  Si anyamaze hajuwi kuwa mumewe katuchefuuuwa sana, kaitia nchi katika ufukara kwa sera zake za "kimasikini masikini" (azimio la Arusha), kama si ufisadi ule kitu gani?
  Na ajinyamazie huko!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Unajua huyu mama huwaga hana mazoea ya ku weigh in katika mambo mengi ya kitaifa. Lakini kama ilivyoripotiwa ni kweli, basi ujue huu ufisadi umefika level nyingine kabisa. Tatizo kubwa ni kwamba hatuna mtu mwenye moral authority na anaye command respect wa kuukemea huu ufisadi. Kila aliyeko ni mchafu tu si Mkapa, si Lowassa, si Msuya, si Mwinyi.

  Na vipi huyu Mengi anambusu busu Kikwete na kusema yeye si fisadi? I don't know anymore
   
 6. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ina maana Zanzibar ndipo ukimwi unapatikana! Na Zanzibar wasiende waliopata pesa, na watalii!

  Sentensi kama hizi kwa Tanzania ni poa kabisa, lakini kwenye standards za nchi nyingine hii ingekuwa controversial, inakuonyesha msemaji hakifirii anachosema, anaropoka tu. Ni kama hafuatilii kinachoendelea nchini with the high temperature state ya Muungano. Ngoja kina Shamhuna wasikie hii.

  Dongo kwa marehemu mumewe!

  Mumewe aliongoza nchi miaka 24 toka uhuru, kumbe ufisadi wa utawala wa mumewe ndiko matatizo yalikoanzia?

  Kwa maneno mengine, kama ambavyo tunapambana na vibaka kwa physical vibano, mafisadi nao wasikimbilie mahakamani, tunapambane nao jino kwa jino, sheria mkononi, kamata mwizi piga ua. Ndicho anacho endorse!

  Again, matamshi ya mtu asiyeandika spichi zake, anarusha kinachomjia kichwani. Na makofi anapigwa, ni kama vile wote hatufikiri. Hakuna wasaidizi wazuri wa kuwaandikia hawa wasemaji wetu hotuba?

  Kiongozi wa nchi fisadi unamsifia eti kwa vile anaruhusu magazeti yaandike kuhusu ufisadi, as if that's all he ought to do, are you alright?

  Unauma na kupuliza tu, huna lolote, huna balls za kuiacha juu juu ionekane unamkemea Kikwete, maana unasema mwenyewe wanakupa afya. Na labda bakshishi, usafiri, mapozeo, kifungua mdomo, na kifunga mdomo, utaacha ku watch what you say? Acha usanii Mama Maria bana.

  Hili ni dongo kwa Mkapa, factually correct kwamba Mkapa na utawala wake ndio ulinuka rushwa tunayoendelea kulizwa nayo mpaka leo, lakini hii ni direct attact to the legacy of Mwalimu Nyerere. Nyerere ndio alituletea huyu mtu. Kenneth Mkapa used was more popular than Benjamin Mkapa the day Mkapa turned his name in for candidacy of president, nobody new Mkapa's abilities kabla Nyerere kumsukumiza down our throats during uchaguzi wa 1995. ​

  Tukusaidie uwe na afya njema vipi wakati umesema mwenyewe unatembelea mikongojo kwa sababu hufanyi unachotakiwa kufanya, na kwamba tayari serikali inakutunza vizuri, Mungu akupe nini, gunia la chawa? Hapo pointi ni nini, unahimiza watu wakufanyie mazoezi au wao ndio wafanye mazoezi? We hufanyi!

  Sikuwahi kumsikia huyu Mama akiongea, alikuwa anabeba gravitas nzito kwa jamii, mpaka siku anafungua mdomo ndio unaona duu, bora angejinyamazia angebaki na heshima yake maana tunakuwa hatujui unafikiri nini.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Iam completely against you Junius!

  Nyerere was a good leader of his time, and, by then he was right on his decision, thats why people supported him however!
  Ni leo hii ambapo unaona kasoro zake baada ya kufutwa

  tongotongo za ukoloni!

  Mwache mama aseme bana!
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  " simjuwi nyerere" by w. Dourado
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ati nini?
   
 10. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Duuuh.....!

  Mods ingekuwa vema mngeweka na kitufe cha kulaani post i.e the opposite of thanks.........!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  NAAM!ingesaidia
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Safi sana huenda wakatokomezwa ili tupone ugonjwa wa ufukara.
   
 13. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #13
  Aug 10, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  una tegemea nini akisema Mkuu wa Kaya ni fisadi? unadhani pata kalika kweli? alisema RA nifisadi halima nusra wamtoa roho itakuwa kwa prezda?
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Dilunga,

  I knew one dimensional minds couldn't handle that.
   
 15. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  I am one of the so called one dimensional minds - and I see Dilunga and all who 'thank' him as misplaced robots/machines! How do you bring logics with your grandma! Are you trying to turn human beings into machines! Let the old lady speak her mind the natural way
   
 16. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Nilidhani amewalipua hao mafisadi kwa kutaja majina yao hadharani kitendo ambacho kitakuwa ndio mwanzo wa moto wenyewe.
   
 17. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi yetu maneno kama yale lazima ulaaniwe. Ningekuwa barabarani ningepigwa mawe!

  Sisi hatukupitia ma inquisition, na ma rannaisance, na ma crusade, na ma French Revolution na ma Civil War yanayotokana na clash of thought. Watu wanashtuka wakiona mawazo tofauti, unamkosoa Mama Nyerere?

  Kuna mtu hapo kasema "how do you bring logics to a grandma..." Yale yale!, Anasema "let her speak her mind the natural way," sisi wazima kweli? Amenilaani kwa sababu kwa jamii yetu isiyo na jadi ya kuangalia mambo kwa undani, ni kufuru kumkosoa mtu mzima kama yule akiongea pumba. Wanasema unaleta "logic." Kumbe ulete nini, nonsense? Yani mtu anaamini kwamba sio wakati wote inabidi ufikirie logically!

  Ukitamka neno "mafisadi " that's good enough, watakuita "mpambanaji," unachukia mafisadi. Hawataki kujua umesema nini kuhusu kukemea huo ufisadi. Hawana muda huo, wanachojua wao umekemea ufisadi, hata uwe msanii vipi. Mchukia ufisadi anasema nchi imejaa ufisadi, na tatizo letu kubwa ni ufisadi, na nchi inanuka ufisadi, lakini kiongozi wa nchi anafanya kazi nzuri!?! Yuko okay kweli huyu Mama? Kwa nini, eti kwa sababu Kikwete karuhusu magazeti yaandike kuhusu mafisadi! Na watu wanashangilia, eti mwache bibi aongee anavyotaka. Bibi kasimama jukwaani ku address national issues, ukubali aongee pumba kwa vile ni mtu mzima?

   
 18. Kibatari

  Kibatari Member

  #18
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Mama Maria twakutakia kila laheri Mama
  Mama Maria Nyerere pole Mama mpendwa kwaheri Eee
  Ukikaa kwa Amani Mama Butiama kijijini
   
 19. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hivi mtu kama mengi akisema mzee wa kaya ni fisadi nini kitamtokea???

  kwa nini wakina dr slaa na wanasiasa wengine wanawaita watu mafisadi lakini mengi akiwaita inakuwa soooooo
   
 20. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dilunga!

  I could argue with you endlessly ....but in most cases I find your posts to be of someone considering themselves 'a perfectionist' trying to force kids to speak grammatical language...but the irony being this 'kifimbocheza' never ever being able to teach the so called grammar he stands for! Wewe ni kukosoa tu! Ajabu leo umeamua kumamini reporter wa magezeti! I am out! CARRY ON ... at your convenience! Sometimes, you do good moderation.
   
Loading...