Mama Maria Nyerere avunja Ukimya, aungana na Vijana wazalendo kulaani kutukanwa Mwalimu

mkuu lisu alisema walivyozoe kusema uongo hawawezi kujifunza kusema ukweli akatoa sababu mbalimabali mfano je Mwalimu mamlaka ya kikatiba aliyapata wapi ya kubadili mambo ya tanganyika kuwa ya muungano na watumishi wake? lakin ccm badala ya kujenga hoja kuwa mamlaka aliyapata katika sheria number-------- lakin watu wanakimbilia kusema ametuka sasa kawa mantiki hii unaweza kusema ametukana?[/QU
Usipotoshe kauli ya Lisu ilikuwa thabiti kwamba
Nyerere alizoea vya kunyonga
Nyerere aliishi kwa uongo
Kama sio matusi kwa mtu anayeheshimika ni nini?
 
Nyerere hakuwa Mungu , wala hakuwa malaika , Nyerere si Mtakatifu, Nyerere ni Binadamu kama wengine.:

huu ndio Ujumbe tutakaowapelekea WaTz...
Hayo yote uliyoorodhesha Mwalimu Nyerere mwenyewe kwa mdomo wake,mbele ya halaiki ya watu na bila kumung'unya maneno alitamka kwamba yeye sio malaika,Hivyo kama binadamu wengine ALIFANYA MAKOSA.
 
Lissu ni msiba mkubwa kwa taifa...huwezi kutukana waasisi namna hii...laana haitamuacha
 
Kuna wakati huwa sitaki kabisa kushiriki katika argument na watu wajinga ila kwa sababu upuuzi wao umekuwa unapitiliza wanatia hasira mpaka mtu unajikuta unajibu matapishi na uozo wao. Anyway acha nikushughulikue tu..

Kuna wakati kama haujui sheria basi uliza uelimishwe ili yasikukute yanayowakuta wenzako unaowatetea. Leo Ben bila hata aibu unaandika hapa Viongozi wa UAMSHO waachiwe..kwa sababu na justification za kitoto kitoto., hivi ninyi watu mnaitakia heri hii nchi au mnapenda kuona kila siku damu zinamwagika..?

Mmelisha watu sumu, mmewalipua kwa mabomu, mmwlemwagia watu tindikali na bado mnatamani kuona damu zaidi inamwagika kwa kutaka wachochezi wlna wavunja amani watolewe ili muendelee kushirikiana kuliangamiza Taifa.

Mama Maria anajua Taifa hili limetoka wapi, anajua nini hasa harakati na ugumu wa kujenga amani ya nchi kamwe hawezi kuungana na wapumbavu ambao mchana kweupe wanamtukana Mumewe katika kuruhusu upumbavu wao wakuona nchi hii inavurugwa.

BY the way; bado unaendelea shughuli yako ya kuosha nguo kwa mchumba wa babu..?

Asante kwa kumshughulikia,maana watu wengine wanatia hasira sana kiukweli,kama mtu hana hoja bora asichangie

It does not make any sense kusema eti ponda aachiliwe,huo ni upuuzi mtupu
 
Ni ukosefu wa nidhamu kwa kiasi kikubwa, ni kukosa adabu kwa vijana wa leo kumdharau.kumkejeli na kumtukana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Vijana wa leo kwa kutotambua na kukosa malezi mazuri wamejikuta wanakuwa mambumbumbu juu ya historia ya Taifa lao.hawajui wala kutambua mchango mkubwa wa waasisi wa Taifa hili katika ujenzi wa Taifa huru la Tanzania.

Laiti kama ungefahamu hata robo tu ya mchango wa Mwalimu katika uhuru wa nchi hii na maendeleo ya watu wake basi katu usingeliuliza swali la kipuuzi kwa nia ya kejeli kwa Baba wa Taifa.

Waonekana umekariri wewe, hivi waeza nijibu huyo babako wa taifa ni wa taifa lepi???Tanganyika, Zanzibar ama Tanzania????

Watanganyika na Wazanzibar wanaojitambua na kufaham hitoria ya kweli wanamlaani kwa nguvu zote huyo babiyo wa taifa.

Wajua pana tabia ya kupamba wasifu wa marehem, Sasa ngoja nikupe wasifu wa babiyo wa taifa lenu sijui lepi maana sie Watanganyika hatuna baba ya taifa, Marehem alikuwa ni kibaraka wa kanisa Catholic, alikuwa ni dhwaalim,muuaji, mrongo na mdanganyifu, alikuwa hapendi watu wenye elim na wanayopinga misimamo yake yakidini kwa hoja za wazi, mbaguzi wa kidini.....

Sijamtusi babiyo ila nimekupa wasifu wake akiwa hai.
Mungu amuongezee adhabu ya kaburi barabbara.
 
Hao ni wanafiki wakubwa, wamekwenda kujipendekeza tu kwa mama Maria Nyerere.
 
Nashangaa sana mnaosema nyerere katukanwa
tuwekeeni hayo matusi bas tuyaone nyie lumumba
 
Mama Maria Nyerere amezungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Msasani, na kuwataka vijana waliokwenda kumtembelea kuzunguka nchi mzima kuwaambia ukweli watanzania juu ya Maisha halisi ya mwalimu na mchango wake katika ujenzi wa Taifa huru la tanzania.

Vijana wazalendo na wapenda Amani ambao wamemtembea Mama Maria wakiongozwa na Kiongozi wao anayejulikana kwa Jina la Mohamed Nyundo, wamesema wako pamoja na familia hiyo na kwamba wamesikitishwa na kampeni inayoendelea ya kumchafua Baba wa Taifa, kumkebehi na kumtuhumu kwa Uzushi na uzandiki.

View attachment 158628View attachment 158630

Ujumbe wa Vijana wazalendo kulaani na kupinga kebehi, tuhuma na matusi kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

========

UJUMBE WA VIJANA KULAANI VITENDO VIOVU VYA KUMVUNJIA HESHIMA BABA WA TAIFA.


Kumekuwepo na kampeni yenye nia ovu iliyoasisiwa hivi karibuni ya kuharibu taswira na heshima ya Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere katika jamii ya kitanzania na kimataifa. Kampeni hiyo inayoendeshwa na vibaraka wa nchi za magharibi na Ulaya, wazandiki na maadui wa Amani ya Tanzania imeendelea kusambazwa kwa kasi na kwa gharama kubwa.

Kutokana na kuwepo kwa Kampeni hiyo, jumuiko la Vijana Wazalendo na wapenda Amani tumeamua kutoa tamko hili la kulaani na kupinga vitendo viovu vya baadhi ya watu kumtuhumu, kumkebehi na kumtukana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa kutambua Mchango wa Baba wa Taifa kama muasisi wa Taifa hili, mpigania Uhuru shupavu, Shujaa aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwa watu wake na kwa kutambua umahiri na jitihada za kujenga Taifa lenye Muungano, Umoja, Amani na Utulivu, jumuiko la Vijana wazalendo limeamua kuukumbusha Umma wa watanzania juu ya mchango wa utumishi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere katika ustawi wa Taifa letu, lakini pia kuhamasisha watanzania hasa Vijana kuenzi kwa Vitendo moyo wa kujituma,weledi na busara za kiuongozi, pamoja na ushujaa na ushupavu wa Mwalimu Nyerere.

Sisi Jumuiko la Vijana wazalendo, tumeona ni vyema kuja kumfariji Mama yetu, Mama Maria Nyerere pamoja na familia nzima ya Mwalimu Nyerere na Kwamba sisi kama wananchi na Vijana makini tutaendelea kuwa pamoja na familia katika kupinga na kulaani vitendo hivyo viovu vya kejeli, matusi, tuhuma na kebehi zinazoelekezwa kwa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwa masikitiko makubwa, tumeshitushwa na kufadhaika kuona chombo kikubwa na taasisi muhimu ambayo ni muhimili mkubwa wa Serikali kama Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania linakuwa ndio uwanja wa matusi ya kumtukana muasisi wa Taifa hili, imetusikitisha na kutufedhehesha. Imefika wakati sasa, kwa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kudhibiti na kuondoa kinga yake kwa wale wote ambao kwa ujinga na kutumika wameamua kuanzisha na kuendesha kampeni kabambe ya kutia doa taswira na heshima ya Baba wa Taifa.


Imetolewa na:


Mohamedi Nyundo.
Kiongozi wa Jumuiko la Vijana Wazalendo na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani.

Hivi na wewe ni mzalendo?.
 
Acha unafiki ulishiriki kwa 100% kuuingiza utawala huu madarakani tena kwa hila....


Hutapata Amani ktk maisha yako kama hutapata msamaha kwa uliyemtendea hila.


Acha unafiki, umasikini umekuwapo tangu ulimwengu unaumbwa. Vitabu vitakatifu vimeusema sana. Kinachosikitisha ni hali tu ya maisha ilivyo. Nitajie nchi ambayo haina masikini.
 
Wewe ndio ndio hujui maana ya Amani, kama kweli unajua amani usingeandika hivyo pole sana... Ukawa kwakuikomboa nchi
 
Alaaah, I'm lost! mi nilidhani tunajadiri maada, kumbe tunamjadiri mtu!? Anyway mama, nimepitia hata magazeti mengine nimeona yameandika kitu kinacho fanana na alichokisema Yeriko Nyerere (sasa hili jina, awe anatoka kwenye huo ukoo au hatoki binafsi sioni point hapo, nimeishi Mwanza kwa muda kidogo, kuna akina Nyerere wengi tu, mgodi wa GGM ndio kuna mfanya kazi wao 1 anaitwa Julius Nyerere kabisa, kabila lake huyo jamaa ni Mjaluo while JK Nyerere alikua Mzanaki)

Ushauri wa bure kwako mama na shoga yako Riz1, pitieni hata na tumagazeti twa leo muone uongo wa Yeriko, au kama vipi, hao vijana wa Lumumba watuwekee clip hata ya Audio humu tuchuje wenyewe, ubishi wa nini sasa!

Kiswahili ni lugha yako ya Taifa. Kienzi. Rekebisha.

Unajuwa kusoma? yeye alisema ni mtoto wa Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Msasani na Mwitongo, hao wenye majina ya Nyerere unaowasema hatujawaona wala kuwasikia wakijinasibisha na Julius Kambarage Nyerere. Huyu Yericko kadanganya kuwa ni wa Nyerere wa ukweli. Sijui umeelewa au bado?

Na hilo la kuandikwa kwenye magazeti ndilo alikoyapata huko akaja hapa akajidai alikuwepo Msasani. Nisome vizuri.
 
Jamani hivi bado mnafikiri tupo kwenye ile miaka ya zidumu fikra sahihi za mwenyekiti? No tushatoka huko tuko kwenye ukweli na uwazi sasa . Kila baya litasemwa Nyerere ndo chanzo cha matatizo ya nchi hii kuanzia viongozi aliyowaweka na sera zake. Kama kweli angekuwa kiongozi mzuri watu wasingejaribu kumpindua. Rip Pius Lugakingira

Kama watu wanapindua pipa, seuze binadamu? Lakini kwa jina la Mungu aliye hai walishindwa hadi Mungu alipomtwaa kwa mujibu wa ahadi ya kila binadamu kuonja mauti!
 
Hujajibu hoja

Hoja gani? Umasikini haujaanza kwa Kikwete. Upo tangu kuumbwa kwa dunia. Ninyi ndiyo aina ya watu mnaodhani maisha yatawashukia tu bila kujibidisha. Wewe uzae watoto 15 utarajie nani awajengee shule? Nani awanunulie vitabu? Mliposhabikia ubepari haya ndiyo matokeo yake. Kila siku unamtukana Mwalimu Nyerere kuwa Ujamaa haufai. Sasa ngoja uone moto wa ubepari. "Ubepari ni Unyama"-Julius Nyerere.
 
Hiv mpka leo kuna pumbaf* flan znaamini nyerere alizd wa Tanzania wote akili?

Kwanza nakerwa na jina la baba wa Taifa, taifa hili lilikuwepo kabla ya nyerere, baba wa taifa langu Tanganyika badae Tanzania ni Mungu wa mbinguni.
 
Back
Top Bottom