Mama Maria Nyerere anawakumbuka wanawake wavaa mabaibui waliopigania Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
Miaka 60 ya uhuru:Kinamama wengine hawakujua kusoma -Mama Maria Nyerere 6 Disemba 2021 'Katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, ambayo sasa ni Tanzania, BBC imefanya mahojiano na watu mbalimbali, na miongoni mwao ni Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa baba wa Taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau amemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam, kwanza amemuulizia anajisikiaje kuona nchi inaadhimisha miaka 60 ya Uhuru?

MAMA MARIA ANAKUMBUKA HARAKATI ZA AKINA MAMA WAVAA MABAIBUI KATIKA TANU

“Wakinamama mchango tulioufanya ni kwanza kukubali…ambalo halikuwa katika uwezo wetu walioharakisha uhuru ukapatikana katika muda mfupi ile miaka ya kwanza ya pili ni hapa Dar es salaam ni akina mama wa MABUIBUI ambao wengine hawajuwi kusoma wala kuandika, ni kina mama washamba hata wakipita stesheni hawaelewi maana yake nini...wakina mama wale hawajuwi kusoma wala kuandika lakini akifika kwenye jukwaaa…hee Profesa wa wa wapi?”

(Mama Maria Nyerere katika mahojiano yake na muandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Aboubakar Famau tarehe 06.12.21).

Kaka Mohamed Said hebu chambua kidogo hawa wanawake wa MABUIBUI wa Dar es salaam aliowatambua Mama Maria Nyerere katika mchango wao wa kupigania Uhuru ni kina nani?

Miaka 60 ya uhuru: Kina mama wengine hawakujua kusoma wakati wa mapambano ya uhuru-Mama Maria Nyerere

 
Back
Top Bottom