Mama Malecela awatetea wanawake wanaopiga waume zao

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Kama inawezekana hii tuiache kwa muda, kwanza ni Ijumaa kwahiyo inaweza kuwa burudisho. Huyu mama asije akawa anamtwanga mzee wetu makofi!

Mama Malecela awatetea wanawake wanaopiga waume zao
JIBU LA SWALI LA MBUNGE SAME MASHARIKI

na Rahel Chizoza na Salehe Mohamed, Dodoma

MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), amewatetea wanawake wanaowapiga waume zao na kusema kuwa huwa hawafanyi hivyo kwa makusudi, bali ni kutokana na wao kuwa katika kipindi cha ‘menopause’.

Akiuliza swali bungeni jana, mbunge huyo alisema kuwa kipindi hicho cha ‘menopause’ huwakumba wanawake walioacha kuzaa au kupata hedhi, hivyo inawezekana makosa yanayofanywa na wanawake katika kipindi hicho si makusudio yao.

Mama Malecela alibainisha kuwa uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa asilimia 35 ya wanaume wanaopigwa na wake zao, lakini wamekuwa hawasemi kwa kuona aibu, hali ambayo imekuwa ikisababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi.

Mbunge huyo pia aliitaka serikali kutafuta dawa za kuwatibu wanawake hao katika kipindi hicho cha mpito, ili kunusuru ndoa zao kwani dawa hiyo ipo na baadhi ya nchi wamekuwa wakiitumia.

Akijibu swali na ushauri huo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Aisha Kigoda, alikiri kuwepo kwa hali hiyo ya ‘menopause’, ambayo alisema kuwa si ugonjwa bali ni hali ambayo huwapata wanawake wenye umri wa kati ya miaka 45 hadi 52.

Alisema mabadiliko hayo humtokea mwanamke baada ya kufunga hedhi na kukoma kuzaa, ambapo hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine, ambapo wengine huwa na hasira, huwa wakali, husinzia bila mpangilio, kuwa na joto kali na wengine kupata hamu ya tendo la ndoa.

Alisema kutokana na hali hiyo kutokuwa ugonjwa, hakuna dawa ya kutibu hali hiyo, ambapo ushauri umekuwa ukitolewa kwa wanawake na wanafamilia kufahamu kuwa kipindi ni cha mpito na hudumu kwa muda usiozidi mwaka mmoja na badaye mwanamke hurudia hali yake ya kawaida.

Alibainisha kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itaandaa vipeperushi vya kuelimisha jamii kuhusu hali hiyo, ili kunusuru ndoa nyingi zinazovunyika katika kipindi hicho kutokana na ombi la mbunge huyo.
 
Lakini mi naomba niseme kuwa naona wanawake kupigwa na waume yao ni tatizo kubwa zaidi inayopaswa kuzungumzwa sana bungeni. Lakini kama kiburudisho cha wikendi ni sawa tu...
Sidhani kama menopause is the most pressing health problem in Tanzania today!
 
Mkuu,

Mimi nilikuwa hata sijawahi kuusikia huo ugonjwa. Labda kwasababu mama watoto hajafikia umri huo. Itabidi kujiandaa mapema.

Naamini hata mama Malecela aliamua kufurahisha genge.
 
Katika nchi za wenzetu maswala haya yanazungumzwa hadharani. lakini hii ya kupiga waume zao ni exaggeration, ni extreme cases. But it makes for good fun in parlament where mstakabhali wa nchi unajadiliwa!
 
Wewe Mtanzania vipi mkuu, mbona kuna watu hapa hupigwa makofi na wake zao na tunawajua, unataka tuanze kuwataja hapa uwanja hautatosha huu, ebo!
 
Wewe Mtanzania vipi mkuu, mbona kuna watu hapa hupigwa makofi na wake zao na tunawajua, unataka tuanze kuwataja hapa uwanja hautatosha huu, ebo!

Kwi kwi kwi!!!! ndio maana nilisema ni Ijumaa tunahitaji maandishi kama hayo hapo.

Ningelisema wataje, lakini mkuu sitaki ufunguliwe mashitaka bure. Siku hizi hata Watanzania wameshajua madai ya Wamarekani, na wenyewe wanaanza kudai mamilioni kwa kukashifiwa.

Basi hayo majina itabidi yewe kwenye PM!
 
Nilikuwa naitafuta hiyo "quote" ya huyo mama kutetea wanawake wanao abuse waume zao.

Mwanakijiji,

Hapa mbona mimi nimetoka kapa? Ulikuwa unatafuta nini eti?

According to mama Malecela, asilimia 35 ya wanaume wanadundwa na wake zao. Ina maana
ukiweka Mwanakijiji, Mtanzania na FMES, mmoja wetu anapigwa. Mimi sio mmoja wapo, kazi kwako Mwanakijiji na FMES, mmoja wenu anachukua mikono toka kwa mama kwi kwi kwi!!!
 
Nilikuwa nisome hicho alichokisema hasa.. gazeti limesema "amesema" lakini hawajaonesha hasa alisema nini isipokuwa wameripoti tu. Sasa kesho akiibuka na kusema hajasema alivyodaiwa kusema si tutarudi yale yale ya Mwakyembe?
 
Mwanakijiji,

Hapa mbona mimi nimetoka kapa? Ulikuwa unatafuta nini eti?

According to mama Malecela, asilimia 35 ya wanaume wanadundwa na wake zao. Ina maana
ukiweka Mwanakijiji, Mtanzania na FMES, mmoja wetu anapigwa. Mimi sio mmoja wapo, kazi kwako Mwanakijiji na FMES, mmoja wenu anachukua mikono toka kwa mama kwi kwi kwi!!!

Kwi kwi kwi,

Mtanzania, sasa kama wewe haumo na imebaki kati ya Mkjj na FMES, unataka jibu la swali lako liwe hadharani au kwenye PM?

Mimi naamini Mama malecela alikuwa anaongelea tatizo kubwa sana na ameweka context nzuri ambayo inahitaji kusoma au kusikia the whole speech kujua alichosema.

Otherwise, kwa vile imewekwa kwa ajili ya friday, naomba kwa niaba ya Mama Malecela (joke) nikushukuru kwa kuweka hili hapa JF ili sasa kazi ya kutafuta huyo mmoja kati ya watatu anayebondwa ianze .... lol

Uwe na weekend njema.

Good night kwa wote!
 
Mimi sio mmoja wapo, kazi kwako Mwanakijiji na FMES, mmoja wenu anachukua mikono toka kwa mama kwi kwi kwi!!!

Mkuu Mtanzania, kuwa na heshima kidogo na wazee wa hapa JF, sasa itakuwaje tena iwe Mkulu MMJ, basi ni mimi ndiye ninayekula makofi na wife, basi yaishe....! kwi! kwi kwi! kwi!
 
Mkuu Mtanzania, kuwa na heshima kidogo na wazee wa hapa JF, sasa itakuwaje tena iwe Mkulu MMJ, basi ni mimi ndiye ninayekula makofi na wife, basi yaishe....! kwi! kwi kwi! kwi!

Mafundi Mitambo,

Basi hii ihamishieni kule kwenye nyepesi nyepesi maana FMES ameona akubali
yeye anadundwa ili yaishe kwi kwi kwi!!!!

Hao wengine wenye wake wenye hako kaugonjwa basi tutajulishana kwenye PM maana siku hizi Watanzania wamejua kwenda mahakamani, inaweza kuleta balaa.

Wewe Imagine tu siku moja wife wa MMJ anaingia studio na kumdunda MMJ
wakati yuko kumhoji Lowassa, nafikiri Agenda21 hapo watakuwa wamepata kile wanachokitafuta kila siku.

Weekend njema!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom