Kama inawezekana hii tuiache kwa muda, kwanza ni Ijumaa kwahiyo inaweza kuwa burudisho. Huyu mama asije akawa anamtwanga mzee wetu makofi!
Mama Malecela awatetea wanawake wanaopiga waume zao
JIBU LA SWALI LA MBUNGE SAME MASHARIKI
na Rahel Chizoza na Salehe Mohamed, Dodoma
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), amewatetea wanawake wanaowapiga waume zao na kusema kuwa huwa hawafanyi hivyo kwa makusudi, bali ni kutokana na wao kuwa katika kipindi cha menopause.
Akiuliza swali bungeni jana, mbunge huyo alisema kuwa kipindi hicho cha menopause huwakumba wanawake walioacha kuzaa au kupata hedhi, hivyo inawezekana makosa yanayofanywa na wanawake katika kipindi hicho si makusudio yao.
Mama Malecela alibainisha kuwa uchunguzi uliofanywa umebaini kuwepo kwa asilimia 35 ya wanaume wanaopigwa na wake zao, lakini wamekuwa hawasemi kwa kuona aibu, hali ambayo imekuwa ikisababisha kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Mbunge huyo pia aliitaka serikali kutafuta dawa za kuwatibu wanawake hao katika kipindi hicho cha mpito, ili kunusuru ndoa zao kwani dawa hiyo ipo na baadhi ya nchi wamekuwa wakiitumia.
Akijibu swali na ushauri huo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Aisha Kigoda, alikiri kuwepo kwa hali hiyo ya menopause, ambayo alisema kuwa si ugonjwa bali ni hali ambayo huwapata wanawake wenye umri wa kati ya miaka 45 hadi 52.
Alisema mabadiliko hayo humtokea mwanamke baada ya kufunga hedhi na kukoma kuzaa, ambapo hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine, ambapo wengine huwa na hasira, huwa wakali, husinzia bila mpangilio, kuwa na joto kali na wengine kupata hamu ya tendo la ndoa.
Alisema kutokana na hali hiyo kutokuwa ugonjwa, hakuna dawa ya kutibu hali hiyo, ambapo ushauri umekuwa ukitolewa kwa wanawake na wanafamilia kufahamu kuwa kipindi ni cha mpito na hudumu kwa muda usiozidi mwaka mmoja na badaye mwanamke hurudia hali yake ya kawaida.
Alibainisha kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itaandaa vipeperushi vya kuelimisha jamii kuhusu hali hiyo, ili kunusuru ndoa nyingi zinazovunyika katika kipindi hicho kutokana na ombi la mbunge huyo.