Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

JF ni tatizo kubwa.... hahaha watajiju, waziri amesema haijasajiliwa TZ hivyo hawawezi kuwafuatilia... waziri anawashauri wabunge wajiandae vya kutosha wanapoleta madai kuhusu taarifa za mitandao, kwani siku hizi unweza kupata taarifa popote na wakati wowote, aamue ni ipi ataisoma... safi sana WAZIRI
 
Ngoye swali lake la nyongeza:

1. Anadai baadhi ya ujumbe eti ni matusi tena ya nguoni. Je govt iko tayari kuleta sheria ya kuwabana wanaotukana na kueta uchochezi ktk mtandao huu?
2. Je govt iko tayari kuelekeza umri wa watu kutumia mitandao ktk internet cafe?

Naibu spika anadai jamiiforums in matatizo makubwa.

Majibu ya Waziri: Sheria ya habari inakuja na wabunge wajiandae kuchangia ktk sheria hiyo. Kuhusu internet cafe.......anatoa onyo kwamba tuwajibike tunawaelekeza watoto kuangalia vitu vinavyojenga maadili ya nchi yetu. Kwani source ziko nyingi...kama vile simu nk.
 
Mtandao wa jamii forums wajadiliwa bungeni. Mbunge adai mambo yanayojadiliwa humu ni maudhi. Mbunge ahoji kama serikali ipo tayari kuwabana wanaoandika maneno ya maudhi au uchochezi kwenye mitandao kama hii

Wamekosa la kufanya huko bungeni. ??
Kama wanafanya ujinga wataadikwa tu hata kwenye FB.
 
ha ha ha ha JF inawafanya wasilale.. mi sijui tatizo liko wapi? kama unatumikia wananchi kwa moyo thabiti JF itakupa sifa zako.. ukiboronga lazima tunkunange tu, sasa hawa wabunge wanaoishambulia JF sijui wana matatizo gani
 
Mchungaji LWAKATARE kaumbuka baada ya kujibiwa kuwa mitandao ya kijamii inaweza sajiliwa nje ya nchi na jamii forum pia haijasajiliwa nchini hivyo hawana meno ya kuizuia,inshort imekula kwake huwezi zuia nguvu ya wananchi
 
Jamii Forums yatinga rasmi bungeni! Kupitia Swali la Dr. Rwakatare!.
Hilda Ngoye apiga nyundo za kufa mtu dhidi ya jf!
Hebu elezea mkuu.......nyundo gani hizo, ili tuzijue kama ni nyundo au upupu!!
 
Wanajamvi kikao cha bunge kinachoendelea nimemsikia Mh. Ngoe akiuliza kwa niaba ya Mch. Getrude Lwakatale kuwa ni nani mmiliki wa JamiiForum?

Naibu Waziri kamjibu kuwa Jamii Forum haijaanzishwa Tanzania na mmiliki wake huenda ni mtanzania!

Tena akaongeza kusema kuwa Jf tunatoa mambo ya ajabu tena wakati mwingine ni matusi
 
kweli jf ni kiboko kwa serikali kwani inaonekana kuwanyima usingizi tena hata furaha.
Viva jf
 
Naibu waziri amejibu kuwa kunasheria ya kusimamia mawasiliano iko kwenye michakato ya mwanzo na muda si mrefu utaletwa bungeni, hivyo mbunge ajiandae kuchangia.
 
big promo!!!! wametambua bunge la jf linafanya vizuri na jamii kama jina forum lilivyo, inaridhika na upashanaji wa habari.
 
Mode change headline ili isomeke

"Jamii Forums Yabalaswa Bungeni, Serikali Yaitetea!. Jf yatambulika rasmi kama chombo cha habari cha kijamii!
man, you are not saying anything........what are these 'posho' people saying?
 
hawana jipya hao! Kuna mambo mengi muhimu sana yenye maslahi kitaifa wenyewe wanajadili jf? Wajadili mgomo wa madactari kwanza:.....
 
Hata Job anahisi JF ni hatari maana Amaris msisitizo kuwa Jaf iangaliwe kwa mapana.
 
Back
Top Bottom