Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Kati ya matatizo lukuki yaliyojazana katika jamii huyu mama anaongelea nani mmliki wa JF?

Huku ni kupoteza muda na rasilimali kwa kuwa na wabunge wa namna hii..mpaka leo sijaelewa kigezo cha kumpa huyu mama huo Ubunge..
 
Hivi wanashindwa kuongelea mgomo wa madaktari huyu ni mchungaji wa mbuzi u kondoo?

Anajipanga kuuliza swali lisilo na tija kwake,eehh akishajua mmliki wake what next?mbona facebook hawaulizi? Au kwa vile na yy ni member kule?

Ni bora hata angeweka maombi maalum kuliombea bunge ili wabunge wenzake magamba wakatae hizo laki 3 wanazopewa kwa kuulia mmiliki wa JF ni nani.
 
Mkuu hii siyo mara ya kwanza hata kwenye kikao cha nec ya magamba pamoja na ripoti ya kina mkama walisema kuwa jamii forum ni mwiba kwao.

My take:
huu ni ufinyu wa mawazo hivi kweli mbunge unayepokea 330,000 kodi za wavuja jasho kwa kupasha moto kiti unasimama unasema upupu kama huu hunakuwa huitendei haki kodi ya mwananchi.yaan kipindi chote ambacho alikuwa nje ya bunge ndo wananchi wamemtuma kuja kuuliza mmiliki wa jf?then what?
 
Tatizo letu ni Ubishi JF haitakiwi na Magambaz

kwa nini haitakiwi na Magambaz? Tutumie busara kutafakari ili tupate jibu inawezekana na sisi wana JF tuna matatizo. Lakini kweli sometimes baadhi yetu wanakwenda nje ya maudhui ya JF.

Sasa kama utaanza kusema fulani mjinga, Kilaza, kubeza kitu kitu na mambo kama hayo hayo, kweli tunakuwa hatuko tena kwenye lengo la kukosoa, kuboresha, kushirikisha ili mwisho wa siku maendeleo kwa watanzania.
 
natamani waifunge ili niiingie hukohuko kwenye mtandao wao wa ccm, labda jk atanisikiliza huko. NDO MAANA NASEMA WABUNGE WA CCM NI VILAZA SANA TUU!
 
hili swala la umiliki mbona ilisha wekwa hadharani siku mingi na inajulikana nani hasa mmiliki wake au ndi wanataka tu wapoteze mda kujadili mambo mengine na kuacha mambo muhimu yanayo gusa taifa kwa ujumla.

Ndo maana tunasema wabunge wanatumia makalio kufikiri wameacha kujadili mgomo wa madaktari nchini wapiga kura wao wanakufa mawodini kwa kukosa huduma na madawa katika kipindi hiki kigumu wao wanataka JF ifungwe kwa vile tu baadhi ya member wa CDM wanawazidi hoja member wa CCM huu ni ujinga hauvumiliki
 
Hata mimi nimeshangaa kumbe huyu mchungaji naye anaijua JF! siajabu ana fake ID na kuchangia labda anachangia humu

Yawezekana JF imempunguzia kondoo kanisani kwake sasa sadaka zimepungua anashindwa kupiga vito vya thamani.
 
Msameheni bure. Hana hoja, swali wala mchango wowote tangu aingie bungeni. Angalau mwacheni leo ajitutumue kupitia mgongo wa JF na yeye aonekanage we!!!
 
Yaani hata cjui huwa wanaogopa nini, siku zote mtandao au kitu kielimishacho jamii watawala hukipiga vita maana hiyo ndo sehemu itakayo wavurugia kula yao, Viva JF na Aluta Continua
 
Kama kuna siku magamba watakua wamekosea step ni kufunga JF maana kitakochokuja kitakuwa moto zaidi ya JF.

serikali ya ccm ni wapumbavu walidhani wakichukua jina la jambo kuwatakuwameimaliza sasa wanataka kuja na lingine wana-jf hebu tuwekeeni cv ya huyu mama
 
Here at JF, is where we can freely utilize our freedom of speech...if they want to take that right away from us....they might as well make this country a communist nation!!!!
 
Kwani michango ya mawazo yanayotolewa humu ni ya wamiliki wa JF?

JF ina members zaidi ya sitini elfu sasa. Wote hawa hili ndilo jukwaa lao kama yeye alivyo Bungeni na kanisani kwake.

Tumewashika pabaya wanasiasa wetu.
 
Huyo kisha choka kuwaibia waumini wake anatafuta wapi pa kwenda
 
Sijawahi kumsikia huyu Mchungaji akikemea ufisadi, leo hii anataka kunyamazisha watu kwa faida ya nini? Anamwakilisha nani huyu mama? Mchungaji gani anayanyamiza watu wasikemee maovu?
 
Back
Top Bottom