Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Biashara ya chakula inauzika na ina uhakika kwasababu kila siku watu wanahitaji kula. Wateja wengi wanavutiwa na ladha ya chakula pamoja na mandhari ya eneo.
Katika maisha ya kila siku huku mtaani, wapo ambao hawana muda wa kupika nyumbani, wanatumia muda mrefu katika shughuli zao za kila siku na hurudi nyumbani usiku wanahitaji kupumzika ili kesho wawahi kwenye shughuli zao.
Wengine ni ma bachelor, shughuli ya kupika na kuosha vyombo kila siku ni ngumu kwao, hasa siku za mvua eti mkaka atoke akanunue dagaa na nyanya aje apike mboga na ugali!
Wengine wana wagonjwa hospitali na hawana muda wa kupika na kupeleka chakula hospital. Unaweza kupata order za lunch maofisini.
Mama lishe wakijiongeza tena kuwa na app, mteja analipia kabisa kwenye simu, unampigia simu mlangoni kwake atoke achukue chakula chake.