Mama lishe jijini Mwanza waacha kuuza chai kwa kuwa bei ya sukari imepanda mara dufu

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mama lishe jijini Mwanza wameacha kuuza chai kwa kuwa chai yao imekosa wateja kwa kuwa bei juu,
wanasema wananunua kilo moja ya sukari kati ya shilingi elfu tano hadi shilingi elfu sita, hivyo hulazimika kuiuza chai kwa shilingi mia tano, ambayo wateja wanaiona ni bei ya juu mno na kushindwa kununua
tazama video hii kwa taarifa zaidi
 
Ujasiliamali wa kukalili, aangalie soko linahitaji nini kwa sasa na alifuate.
Kama kuwajali maskini ni hivi, acha tu wabangaize wenyewe.

Awamu hii hasa kwenye miaka hii ya mwanzo ya kuweka system sawa Darwin Theory inaapply. Be strong uta survive, ukiwa weak lazima uanguke
 
Sijui juice na soda nazo zitapanda? Maana bidhaa hizi nazo zinahitaji sukari ili kuzalishwa .Ngoja niwahi nikanunue juice zangu za kutosha kabla bei haijapanda.
 
Jiji la Arusha ilitoka sukari siku ya juma nne na ilikuwa kwa ajili ya kina mama ntilie tu, kila mwenyekiti wa mtaa alipata sukari ya kwenda kuuzia mama ntilie wa mtaa wake, na hapo ndio na wengine tulipata angalau kilo moja moja maana mama ntilie walikuwa wanapewa kilo 5, na wengine tukapata huruma kutoka kwa kina mama hawa. Hakika mwanamke ni jeshi kubwa.
 
jiji la arusha! mkuu ebu eleza zaidi.. hiyo ndio ile iliyokamatwa?au

kwaiyo na wenyeviti wakawa wachuuzi?
Hiyo haija kamatwa ilitolewa na mfanya biashara ikauzwa kwenye kata na wenyeviti ndio wakawa wasimamizi tu maana iliuzwa kwenye ofisi ya mtendaji wa kata.
 
Mpumbavu ni wewe uliyekalia kulia lia na kulalamikia sukari kila kukicha kana kwamba maisha yanaishia kwa kunywa chai.


kama kikombe cha chai kimefika Tsh 1000... Hii ni hatari sn.

Ni heri kutumia ile sukari ya Tsh 800 kutoka brazil.
 
Back
Top Bottom