Mama kukosa maziwa ya kutosha, atumie chakula gani ili yatoshe kwa ajili ya mtoto?

Umkilo

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
470
419
Mke wangu alijifungua tar 6/01/2018 mtoto wa kiume shida amekuwa na changamoto ya kukoswa maziwa ya kutosha kunyonyesha mtoto afanyeje ili kupata maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto?
 
Mke wangu alijifungua tar 6/01/2018 mtoto wa kiume shida amekuwa na changamoto ya kukoswa maziwa ya kutosha kunyonyesha mtoto.

Afanyeje ili kupata maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto?
Pole sana. Anakula chakula gani? Kuna baadhi ya vyakula vinavyosaidia kwa mama anayenyonyesha. Jaribu kumpatia uji wa ulezi, supu ya nyama ya ng'ombe, mbuzi, au kuku, na hata uji wa mahindi kama ulezi unakuwa shida kupata.
Hata hivyo, kuna baadhi ya kina mama wanakuwa na maziwa kidogo (hayatoshelezi kwa mtoto). Hivyo msione vibaya kumwanzisha mtoto maziwa ya chupa. Ulizeni ushauri wa wataalamu wa afya juu ya hilo.
 
Azingatie lishe bora ahakikishe anashiba vizuri. Anywe maji na juisi kwa wingi haswa juisi ya carrot. Anywe uji, kama ni wa mahindi anaweza kuweka pilipili manga iliyosagwa.

Aepukane na msongo wa mawazo, msongo wa mawazo pia huchangia maziwa kua machache. Apate muda wa kupumzika na amnyonyeshe mtoto mara kwa mara hii husaidia uzalishwaji wa maziwa kuongezeka.
 
Supu ya mbuzi anakunya kila asubuhi, chakula kingine ni kawaida tu ugali nyama /samaki/maharage/mbogamboga na matunda. Usiku wali akiadilisha ndizi
 
Azingatie lishe bora ahakikishe anashiba vizuri. Anywe maji na juisi kwa wingi haswa juisi ya carrot. Anywe uji, kama ni wa mahindi anaweza kuweka pilipili manga iliyosagwa.

Aepukane na msongo wa mawazo, msongo wa mawazo pia huchangia maziwa kua machache. Apate muda wa kupumzika na amnyonyeshe mtoto mara kwa mara hii husaidia uzalishwaji wa maziwa kuongezeka.
Asante sana.
 
Pole sana. Anakula chakula gani? Kuna baadhi ya vyakula vinavyosaidia kwa mama anayenyonyesha. Jaribu kumpatia uji wa ulezi, supu ya nyama ya ng'ombe, mbuzi, au kuku, na hata uji wa mahindi kama ulezi unakuwa shida kupata.
Hata hivyo, kuna baadhi ya kina mama wanakuwa na maziwa kidogo (hayatoshelezi kwa mtoto). Hivyo msione vibaya kumwanzisha mtoto maziwa ya chupa. Ulizeni ushauri wa wataalamu wa afya juu ya hilo.
Pamoja na hayo hapo juu pia mtafutie tende awe anakula mara kwa mara.
 
uji unasaidia zaidi si chini ya lita mbili kwa siku hata asipokula hayo mamitori hiyo inakaa sawa anaweza kuwa anabadilisha aina ya uji pia sio lazima anywe uji wa aina moja
 
Uji na mchemsho wenye mchanganyiko wa ndizi na samaki. Naona wengi wanafanya ivyo.
 
Uji wa mchele wenye nazi (nazi inasaidia sana kuongeza maziwa),Uji wenye mbegu za maboga asagie humo kwenye unga iwe rahisi kupika ,Unywaji wa maziwa nao unaongeza maziwa na mwisho ajitahidi kunywa maji ya vugu vugu sana hata litre tatu akiweza kwa siku hata angaika kamwe.
 
active_mamaz follow hiyo account instagram, utapata unga bora wa mbegu za maboga!!ilimsaidia sana mke wangu kipindi amejifungua.
 
01). Apendelee kunywa uji (ulezi/ mchele/mahindi) uliotiwa pilipili manga,

02.Apendelee kunywa supu yenye mchanganyiko wa ndizi + bilinganya na nyanya chungu (Ngogwe)
Vile vile kama ana msongo wa mawazo ajitahidi sana kuuepuka.
Itamsaidia sana.
 
Mtafutie supu ya pweza nzito na nyingi anywe.atatilikisha maziwa kama bomba.
 
Mke wangu alijifungua tar 6/01/2018 mtoto wa kiume shida amekuwa na changamoto ya kukoswa maziwa ya kutosha kunyonyesha mtoto afanyeje ili kupata maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto?
ale kwa wingi mbegu za maboga
 
Mke wangu alijifungua tar 6/01/2018 mtoto wa kiume shida amekuwa na changamoto ya kukoswa maziwa ya kutosha kunyonyesha mtoto afanyeje ili kupata maziwa ya kutosha kumnyonyesha mtoto?
Chukua uwatu 100gm chemsha kwa maji lita moja na nusu kisha anywe nusu kikombe kutwa mara 3 siku 14, pia atie pili pili manga katika uji wake
 
Back
Top Bottom