Elections 2010 Mama Kilango Malecela aonya machafuko uchaguzi 2010

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,803
30,738
MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ametoa tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea umwagaji damu katika uchaguzi mkuu wa 2010 iwapo mbegu za chuki za ukabila na udini alizosema zinapandwa sasa, hazitadhibitiwa mapema.


Kilango, mmoja wa wabunge wenye hoja nzito wakati wa kujadili masuala mbalimbali bungeni, pia alisema viongozi hawana budi kuwa makini katika kutoa kauli zao wakati wa kujadili mambo muhimu kwa taifa, ingawa hakutaja ni kauli na masuala gani.


Mbunge huyo wa Same, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alisema umwagaji damu uliotokea Zanzibar wiki iliyopita ni cheche tu na kwamba kama hali hiyo haitadhibitiwa haraka cheche zinaweza kuzaa moto.


Vurugu hizo zilitokea wiki iliyopita kisiwani Zanzibar wakati wafuasi wa CCM na CUF waliposhambuliana kwa silaha za jadi, yakiwemo mapanga na visu wakati wa zoezi linaloendelea la kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni.


“Hali ya Zanzibar inabidi tuikemee wote na kwa nguvu zote. Hivi kama leo wakati wa kujiandikisha tu, tunakatana mapanga... ikifika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 itakuwaje,” alihoji Kilango wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.


Mbunge huyo alikemea ubaguzi kwa misingi ya kabila ambayo alisema inaanza kujitokeza sasa na kutaka iwe marufuku kwa mtu yeyote kumuita Mtanzania mwenzake kuwa ni wa kuja pale anapojitokeza kugombea nafasi ya uongozi eneo ambalo hakuzaliwa.


Kuhusu kauli za kushambuliana ambazo zinatolewa wakati wa kujadili masuala muhimu ya kitaifa, Kilango alisema matamshi mengine yanachochea kuvuruga amani iliyopo.


Bila kumtaja kiongozi yeyote, Kilango alisema anakubaliana na watu wenye misimamo thabiti kwenye mambo muhimu ya kujenga nchi, lakini akashauri watumie ndimi zao vizuri ili matamshi yao yalenge kuimarisha amani.


“Kukosoana ni lazima... tukosoane ili tujenge lakini swali linakuja tunakosoleana wapi,” alihoji Kilango.


Suala la azma ya serikali kununua mitambo ya Kampuni ya Dowans Tanzania Limited liliibua mjadala mkubwa baada ya kamati mbili za bunge kutofautiana, moja ikitaka jenereta hizo za kuzalisha umeme wa dharura isinunuliwe kwa sababu ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na huku kiongozi wa kamati nyingine akishauri inunuliwe ili kulinusuru taifa na uwezekano wa kuingia gizani.


Tofauti hizo zilisababisha wabunge kurushiana maneno makali, ikiwemo kauli ya kumuelezea mmoja wa wabunge kuwa anajifunza siasa bungeni na kwenye kamati za bunge, kuhusisha mpango huo na ufisadi, kuhusisha msimamo na Operesheni Sangara ya Chadema na madai kuwa wanaounga mkono suala hilo walilipwa "posho posho kubwa".


Kilango alitahadharisha kuwa amani iliyopo leo ikitoweka itachukua miaka mingi kuirejesha na kutoa mfano wa nchi ya Rwanda ambayo tangu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, bado hawajaweza kuijenga nchi hiyo.


Kilango alisema kuwa Tanzania imekuwa ikisifiwa ulimwenguni kutokana na kuwa na amani na kiongozi mzuri wa nchi, lakini zinazoanza kujitokeza sasa nchini hasa Zanzibar, Tanzania inataka kujiondoa kwenye nafasi hiyo.

Source:Mwananchi
 
Hakuwezi kuwa na machafuko kama ulitimiza majukumu yako uliyoahidi wananchi wako wakati unaomba kura za ubunge kwanza tutaanza na yeye je alichoahidi wananchi wake ametekeleza ? Angalau kwa asilimia 40 na wananchi wake wanajua hilo ?

Ameanzisha miradi mingapi jimboni mwake ya kusaidia wananchi wake ? Katika miradi hiyo kumetengeneza ajira ngapi ? Amejenga shule ngapi ? Toka amechaguliwa ni wanafunzi wangapi toka kwake wamefanikiwa kwenda form 1 kidato cha 6 na elimu ya chuo kikuu ??

Kwanza tuanze na yeye
 
Hakuwezi kuwa na machafuko kama ulitimiza majukumu yako uliyoahidi wananchi wako wakati unaomba kura za ubunge kwanza tutaanza na yeye je alichoahidi wananchi wake ametekeleza ? Angalau kwa asilimia 40 na wananchi wake wanajua hilo ?

Ameanzisha miradi mingapi jimboni mwake ya kusaidia wananchi wake ? Katika miradi hiyo kumetengeneza ajira ngapi ? Amejenga shule ngapi ? Toka amechaguliwa ni wanafunzi wangapi toka kwake wamefanikiwa kwenda form 1 kidato cha 6 na elimu ya chuo kikuu ??

Kwanza tuanze na yeye

Unataka Mkuu FM ES arudi kwa nguvu zote.
 
“Hali ya Zanzibar inabidi tuikemee wote na kwa nguvu zote. Hivi kama leo wakati wa kujiandikisha tu, tunakatana mapanga... ikifika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 itakuwaje,” alihoji Kilango wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.

Yote hii inasababishwa na Tume za uchaguzi zilizo nyuma ya CCM, wao ndio huanza uharibifu ili kuisaidia CCM, wananchi wakija juu wanalalama. Wekeni (CCM) mazingira huru tokakujiandikisha mpaka kupiga kuramambo ya vurugu yatapungua.
 
Mama kilango anataka kututishia amani wakati yeye jimboni mwake amefanya madudu matupu -- inaudhi sana hii kiwango cha elimu jimboni mwake kimeshuka , ajira hajaongeza , kuna njaa na madudu mengine mengi tu sasa anataka kusema amani haitochafuka jimboni mwake kwanza kama yeye hajatimiza ahadi zake ?
 
Mama kilango anataka kututishia amani wakati yeye jimboni mwake amefanya madudu matupu -- inaudhi sana hii kiwango cha elimu jimboni mwake kimeshuka , ajira hajaongeza , kuna njaa na madudu mengine mengi tu sasa anataka kusema amani haitochafuka jimboni mwake kwanza kama yeye hajatimiza ahadi zake ?

Mkuu Shy zile picha zake bado unazo?
 
Kufanya au kutofanya madudu jimboni mwake mimi sitaki kuingilia. Inawezekana hajafanya chochote kwa sababu hana mapesa ya kifisadi ya kumwaga jimboni mwake kama vile wafanyavyo wabunge wengine wa CCM -- akina Kapuya, Mkono, Chenge n.k. na wengine ambao bado hata bado hawajapata ubunge -- kama vile akina Makalla.

Na kutokana na kauli zake, Mama huyu anaonekana mpinzani wa mafisadi wa CCM, na hivyo tayari ameainishwa kama mmojawapo wa kupigwa vita asirudi Bungeni, pamoja na akina Mwakyembe, Sitta, Kimaro, Ole Sendeka, Sellelii na wengine. Kwa hilo nisingependa kumzonga sana. hali kadhalika tunaweza kusema kuwa kauli zake ni za Mzee Malecela, mme wake, ambaye amekuwa ni kama bubu anayetaka kusema -- (kunradhi -- simaananishi huyu mpiganaji wa kikwelikweli tunaye humu JF).

Kuna sababu nyingi zinamfanya Malecela asiweze kutamka yeye mwenyewe haya -- si unajua tena walivyo CCM? Ataambiwa hana shukurani kwani CCM ilimlea na kumpa vyeo kadha; anaendeleza makundi ya 2005 na matusi na kashfa nyingi nyingine.

Mimi ugomvi wangu na mama huyu -- kama utaitwa ni ugomvi -- ni kutofuatilia kwake ile kauli yake aliyotoa Bungeni kuhusu 'urejeshwaji' wa mapesa ya EPA. Alisimama kidete na kusema atahakikisha mapesa hayo yanarejeshwa halisi (physicallly) na siyo tunaambiwa tu au kuonyeshwa kwenye makaratasi.

Alisema angetaka mahela hayo yarejeshwe katika viroba, vionekane.

Jee viroba vililetwa na vilionekana? Au naye kanyamazishwa na mafisadi?
 
Kwa dhati nawaona wana jf mkitaka kumwamsha kama wetu fmes, nway, yetu macho
 
Huyo ni mfuasi wa Sultani CCM akiona kwamba safari hii sio mchezo ,kama wafuasi wa Sultani CCM watacheza na matokeo basi wajue kuwa hakuna atakae kubali ,tume ya uchaguzi imekwisha kupingwa ,Katiba nayo hali kazalika ,bila ya kuvisahau vyombo vya dola ambavyo havioni nchi nyingine vyombo kama hivyo havikufua dafu katika kuwalinda masultani , wananchi wameukataa Utawala wa Sultani CCM karibuni chaguzi zote ,kwa maana hakuna uchaguzi uliopita bila ya kulalamikiwa tume ya uchaguzi na vyombo vya dola ,kuvumilia kuna mwisho ambao si mzuri pale mwananchi wa kawaida atakapoamua liwalo na liwe ,tumeona Pemba bahati mbaya pemba hakuna sehemu nyeti za kuzipiga kiberiti lakini kwa hapa Tanganyika hata sigara tu inaweza kuiteketeza mbuga nzima.
Ni machafuko ambayo vyombo vya dola havitaweza kabisa kuyasimamisha ndani ya muda mfupi ,muda ambao unaweza kuwawacha midomo wazi na kila mmoja kuanza kumlaumu mwenziwe kama walivyozoea.

Kila siku wanaambiwa badilisheni katiba hawataki,badilisheni Tume hawataki sasa wanalolitaka ni lipi kama sio machafuko.

Kuwadhibiti watu waliotulia ni rahisi sana lakini kuwadhibiti watu waliocharuka wandugu si kazi rahisi chukulia miji mikuu yote ya Tanzania wananchi wamemjia juu Sultani CCM ,watu wanavunja magari,watu wanakwiba watu wanaripua vituo vya petrol watu wanachoma moto majumba ya wafuasi wa Sultani CCM ,ile ya kuelekea kwenye uwanja kwa kufanya mkutano itakuwa haipo kitu ambacho kinawarahisishia Polisi kazi ,hili litakuwa jambo la papo kwa papo upapatapo ndio hapo hapo hata ukirusha jiwe kwenye jumba la wizara basi imetosha.

Wacha wafuasi wa Sultani CCM wacheze na utulivu wa wananchi waliotulia wananchi ambao kwa kiasi fulani ni wapole hivyo natumai hasira za mtu mpole zinajulikana vilivyo hazina sumile.
 
Mama kilango anataka kututishia amani wakati yeye jimboni mwake amefanya madudu matupu -- inaudhi sana hii kiwango cha elimu jimboni mwake kimeshuka , ajira hajaongeza , kuna njaa na madudu mengine mengi tu sasa anataka kusema amani haitochafuka jimboni mwake kwanza kama yeye hajatimiza ahadi zake ?

Mkuu Shy; i beg to differ...

SIjui hayo madudu unayalinganisha vipi na wilaya zilizokuwa za mwisho kielimu, kilimo, biashara, ajira nk. yule mama katoa angalizo na hajatishia mtu amani. Umeshafanya analysis kujua ni wangapi wameleta positive impact na yeye ana-rank namba ngapi?

Alichosema kina uzito wake na ni muhimu kuwa makini kwani hali si swari mjomba!!!

Ma'adam imetoka kwako pia haishangazi...
 
MTM i beg to differ with u.. in the last election during the rivarly between her and Daniel Yona who happens kuwa shemeji yake and also ex-boyfriend... 2 people were killed baada ya vurugu kutokea. Huyu mama she is an opportunist. Hana any viable political stength except the fact that she is non-mtandao and due to the lack of reward expected from the JK regime, anaona bora anyee tuu kupata cheap popularity. As a matter of fact... she is a leech and the only reason she married that man was because she wanted to be the first lady to the extent of being depressed when he lost to JK. As she was quoted in Dodoma in early 2005 before the election:

"First Anna out, second Anna in"

We all know what the first Anna did to this country, I dont think I want to see the sequal. On aggregade the corruption done by her 'dear' husband Malecela is far greater than whatever is happening now (taking into consideration wakati wa Mwalimu kuiba was not soo easy)... When Nyerere spoke of '...kama ukoma..' we all know he was refering to him. Kama angekwua na hii integrity ambayo anajifanya kuwa nayo sasaivi asingejihusisha na watu kama mume wake. Sikuzote mbwa asie na chakula hubweka akiona yeye kafungwa kamba lakini wenzake wanakula chakula, be it chawizi.

I like her because she serves our purpose, lakini jamani naombeni tusiwe watu wakutongozeka kirahisi rahisi, mtu akisimama bungeni akamchamba Lowassa ni vizuri lakini that does not mean they are doing it for the right reason. JF is at the cutting edge of the sword of change and muamko, lakini ninapo onaga just how susceptible to populist rhetoric navunjika moyo sana. Perhaps it is a remnant of the Nyerere slogan era;

"Kilimo ni utiwamgongo" NO! it is not at the moment it is toe nails.. 80% ya uchumi wa wetu uko posta mjini pale... sasa sijui pale kuna mashamba ya kahawa na pareto?! Dont get me wrong... it should be but it really is not! tujiulize kwanini na sio kuendeleza KAULI MBIU which seems to be all that we do , " Ujamaa na kujitegemea".... Right!! Ndio haya yakina zitto sasa mnayaona! Tusitongozwe na maneno makali kwa maadui zetu tuu, tuangalie mambo mengine pia na sio sura kama mwalimu alivyotuambia... tumeweka sura sasa inaoa tuu wake sijui 7, sijui 8.. Muungwana anakimbizana na Nabii Suleiman (A.S) aka King Solomon aliefikisha 300 wives and 700 concubines. But as the latter lived for along time the former is on good track to beat his record. I often wonder what the CCM government of Dr. Salim would be like... NO RA, no EL no JK.. (awngepewa position but would ultimately be expendible I suppose, sijui)

Back to my pont, huyu mama she is really not who we need, sio kiongozi mzuri na hatufai lakini KELELE acha apige... kwasababu ata mbwa mwenye rabis akibweka akakuamsha ukamkamata mwizi ni jambo zuri, shida tuu pale ambapo baada ya kumweka mwizi chini ya ulinzi Mbwa huyo anaenda kumn'gata mwanao! TUWE WAANGALIFU
 
Huyu maza ana kimbele front, amesema nani kuna machafuko. sisi tuko safi tutaendelea kuwapigia kura of all the madudus they did. Kuna watu wanapenda sana showups za media ili wamjue yupo na anafanya kazi.

Heheeh kalaghabhaho!!! vita apeleke nyumbani kwake dom siyo tanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom